Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

JINSI MAMA MARIA NYERERE ALIVYOFUNIKA MZISHI YA MADIBA SOUTH LIVE!!

$
0
0


           Quru,Afrika Kusini
WAKATI Dunia ikishuhudia mazishi ya aliyekuwa Rais wa kwanza mweusi nchini Afrika Kusini,ambaye pia alikuwa mpigania Uhuru wa nchi hiyo,Hayati Nelson Madiba, Tata,Mandela,yanayoendelea hivi sasa katika kijiji alichozaliwa cha Quru nchini Afrika Kusini, Mama mjane wa Rais wa kwanza wa Tanzania na mwasisi wa Taifa hilo,Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Mama Maria Nyerere, amefanikiwa kuteka umati wa watu katika mazishi hayo.
Umati uliokuwa ukishangilia kila jina la Mama Maria Nyerere ikijatwa ni zaidi ya umati ulioripuka kwa furaha pale ambapo Rais wa Marekani Barack Obama, Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, Rais wa Malawi Joyce Banda,Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete, pamoja na watu mbalimbali waliopewa nafasi ya kumzungumzia Maandela, tangu alipofariki dunia mpaka leo hii anapozikwa, huku Rais wa Afrika Kusini akiendelea kupata aibu katika uso wa dunia baada ya kuzomewa kila anapo pata nafasi ya kuzungumzia maisha ya kiongozi huyo.
Mzee Nelson Mandela,(kushoto) akimsalimia Mama Maria Nyerere,pamoja na Mwl Baba wa Taifa
Maria Nyerere akiwa katika mazishi hayo hivi sasa, ameshangiliwa na umati mkubwa wa watu na kuwa Mwanamke wa kwanza, kushangiliwa katika mazishi hayo,awali siku ya ibaada ya kimataifa iliyofanyika mapema wiki hii, Rais wa Marekani pamoja na Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ndiyo viongozi pekee waliopata heshma kubwa ya kushangiliwa katika mazishi hayo huku,Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma akizomea na umati wa Raia wa nchi yake.
Katika kile kilichoonyesha kwamba Mama Maria Nyerere alikuwa ni mtu muhimu mbele ya wana Afrika Kusini,hata wakati Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete akizungumzia uhusiano wa Tanzania na Afrika Kusini na kumtaja Mama Maria Nyerere bado umati ulishangilia uliposikia jina la Mjane huyo ambaye ndiye Mama wa Taifa la Tanzania.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>