Mwili wa kijana Paschal Jumbe ukiwa kitandani baada ya kujiua
Akizungumzia tukio hilo mwenyekiti wa mtaa huo Juma Kajala amesema kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo ambapo saa 2.30 asubuhi alipigiwa simu na watu wanaoishi naye kwenye nyumba hiyo.
Amesema baada ya kufika hapo alikuta dirisha likiwa limefunguliwa na marehemu akiwa amelala kitandani ndipo alipiga simu polisi na walipofika polisi walivunja mlango na kumkuta akiwa amekufa .
Naye dada wa marehemu Nyanyama Jumbe alisema kuwa mdogo wake alikuwa na ugomvi wa kifamilia na mke wake Reticia Jumbe ambaye walipogombana alikwenda kuishi eneo la Nyankumbu nje kidogo ya mji na huenda ndicho chanzo cha mdogo wake kujinyonga.
Kamanda wa polisi mkoani hapaJoseph Konyo amethibitisha kutokea kwa tukio na kwamba uchunguzi zaidi kuhusu tukio hilo unaendelea
Na Valence Robert-Malunde1 blog-Geita