Mafanikio! Taarifa ikufikie kuwa staa wa Bongo Fleva, Estalina Sanga ‘Linah’ amekanusha stori za madai ya kuhongwa gari jipya analosukuma mjini kwa sasa aina ya Toyota Mark X.
Akizungumza na mwanahabari wetu, Linah ambaye hivi karibuni alitokea nchini Afrika Kusini kufanya video ya wimbo wake mpya alisema mkoko huo amepewa na kampuni anayofanya nayo kazi ya NFZ.
“Nani kasema nimehongwa gari? Siwezi kuhongwa gari kwani najituma sana kwemye kazi yangu,” alisema Linah.Mbali na kumiliki ndinga hilo, miezi kadhaa iliyopita aliwajengea nyumba wazazi wake na sasa anajenga ya kwake.