Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred hajui Kiswahili? Well, tuliowahi kukaa naye kidogo tunaweza kumtetea kuwa anakijua haswaa, sema hupendelea zaidi kuongea kimombo. Pengine ndio maana mbunge wa viti maalum kutoka Zanzibar, Rukia Ahmed anahisi mrembo huyo haijui lugha yake ya taifa.
Akiongea bungeni leo, Bi. Rukia amesema Brigitte Alfred hafai kuiwakilisha Tanzania kwakuwa hawezi kuzungumza Kiswahili. Mbunge huyo alienda mbali zaidi kwa kupendekeza mashindano ya Miss Tanzania yafutwe na badala yake yawekwe mashindano ya Sayansi kwa manufaa ya taifa.

Akijibu kauli hiyo, Brigitte amesema: Meanwhile as our county suffers from 3rd world problems this is what is being discussed bungeni. I would love to meet this this woman! Asante mama,” ameandika mrembo huyo kwenye Instagram. “All of your comments give me hope that there’s still sensibility out here,” aliongeza.
“Mh.Rukia amekosa mada bungeni?*rollingmyeyesoutloud*,” alitweet.
“Anko in the office must be jumping for joy right now-they love to say ‘I told you so’-In Kiswahili ofcourse.”
Hata hivyo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara alisema serikali haiwezi kuyafuta mashindano hayo kwakuwa yana umuhimu mkubwa kwa taifa na yamekuwa yakiitangaza nchi na shughuli za utali