Mkurugenzi wa NIMR Tabora Dr.Joseph Swila akionesha baadhi ya vifaa vya kisasa katika chumba cha maabara hiyo ambayo inatajwa kuwa huenda ikasaidia mikoa yote ya kanda ya magharibi. |
Jengo la maabara ya utafiti katika kituo cha utafiti wa magonjwa ya binadamu lililogharimu zaidi ya shilingi milioni.297.8 |
Mkurugenzi wa NIMR Tabora Dr.Joseph Swila akisoma taarifa ya ujenzi wa jengo la maabara ya Tabora |
Mkurugenzi mkuu wa NIMR Dr.Mwele Malecela wakati akisoma taarifa fupi tangu kuanzishwa kwa maradi wa Jengo hilo la maabara ya kisasa. |
Mwenyekiti wa Bodi ya NIMR ,Prof.Samwel Masele Akizungumza wakati wa sherehe fupi ya ufunguzi wa jengo la maabara ya kisasa. |
Mkurugenzi wa tume ya Sayansi na Teknolojia Dr.Hassan Mshinda akisoma hotuba kwa niaba ya naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia ambapo alipongeza kazi kubwa inayofanywa na NIMR katika kuhakikisha inakabiliana na magonjwa mbalimbali kwa kufanya utafiti wa magonjwa na kupata ufumbuzi wake. |
Mwandishi wa habari mkongwe wa Redi Tanzania Bw.Benkiko ambaye alipata fursa ya kusalimiana na mgeni rasmi wakati wa sherehe za ufunguzi wa jengo hilo |
Wadau mbalimbali wa afya walihudhuria katika sherehe za ufunguzi wa Jengo hilo.Picha zote na KAPIPIJhabari.COM |