Wema Sepetu akiwa ameacha mgongo wake wazi.
Beautiful Onyinye wa Bongo, Wema Sepetu hivi karibuni ameachia picha tata kwenye akaunti yake ya Mtandao wa Instagram zikimuonesha akiwa ameacha mgongo wazi, jambo lililotafsiriwa na wengi kuwa ameamua kufunga mwaka huu kwa staili hiyo ya kuacha mgongo nje, Showbiz inakudondoshea. Katika picha hizo, Wema anaonekana kujichora tatoo kibao kuanzia shingoni na kumfanya aonekane tofauti na alivyozoeleka jambo lililofanya wengine wamsifie huku wengine wakimponda mbaya. “Sasa Wema kujichora hivyo mgongoni ndiyo nini? Bora ungeuacha mgongo wako kama ulivyokuwa zamani,” alichangia mmoja wa wadau na kuungwa mkono na wenzake. Showbiz ilipomvutia ‘waya’ Wema ili kumuuliza kulikoni ameamua kupiga picha za kuuanika mgongo wake, simu yake ilikuwa ikiita bila kupokelewa.