Kwa mujibu wa Sheria hairuhusiwi kufunga gari la mtu wakati yumo ndani ya gari
.Zaidi ya hapo ni Rushwa tu
.Usawa wa kijinsia uzingatiwe pia
Askari wa Manispaa ya Ilala wakiwa wanafunga gari aina ya Rav 4 huku mwenye gari akiwa ndani ya gari bila hata ya kumpa nafasi ya kujitetea kama walivyokutwa na (Mpiga Picha Wetu) katika makutano Morogoro Road na Mali Street.
Wakazi wengi wa jiji la Dar es Salaam wamekuwa na malalamiko ya muda mrefu kwa askari na wafanyakazi wa manispaa ya Ilala kwa kuwa wasumbufu endapo tu wataegesha magari yao.
Watu mbalimbali walihojiwa na MOblog bila kuwa tayari kutaja majina yao wameeleza kwa masikitiko makubwa usumbufu mkubwa wanaopata kutoka kwa askari hao wa manispaa kwa kuombwa rushwa kwa kila kosa wanalotenda wakati manispaa haina nafasi ya kutosha kwa ajili ya maegesho ya magari ya wakazi wanaoingia na kutoka kati kati ya jijini la Dar es Salaam hasa maeneo ya mjini.
Bila hata aibu na huruma jamaa akiendelea kulifunga gari la mwanadada huyo ambaye jina lake halikweza kupatikana mara moja.
Bila hata aibu na huruma jamaa akiendelea kulifunga gari la mwanadada huyo ambaye jina lake halikweza kupatikana mara moja.