Raisa Said, Korogwe;
Mjumbe wa Halmashauri kuu Ccm Taifa(MNEC}kupitia Korogwe vijijini Dk Edmund Mndolwa amewatahadhalisha viongozi wa kata na vijiji kutowateua wagombea wasiokuwa na mvuto lengo likiwa kujipanga kwa ajili ya ujao. 2014/2015.
Akizungumza na wajumbe wa Halmashauri kuu ya ccm kata ya mazinde na mkomazi Mndolwa alisema kama watawachagua wagombea wanao kubalika basi ccm itashinda tena kwenye uchaguzi ujao.
Dkt Mndolwa alisema kuwa chama hicho kinatakiwa kufanya kazi kwelikweli kuhakikisha kinashinda kwa kishindo kwa viongozi kujenga umoja upendo miongoni mwao na kukataa fitina inazosababisha kutoweka kwa umoja hasa katika chaguzi za mwaka 2014.
Alisema kuwa viongozi na wanachama wakishirikiana kwa pamoja wataweza kuimarisha chama na kuwa imara katika uchaguzi wa serikali za mitaa na vijiji pamoja na uchaguzi wa madiwani na wabunge nakwamba wataweza kukuza uchumi na maendeleo katika chama hicho.
Dkt Mndolwa ambae pia ni mwenyekiti wa Wazazi Ccm mkoa wa Tanga alisema kuwa sasa ni wakati wa kubadilika na kuwapitisha wagombea ambao wanakubalika ili kuepuka kupata wapinzani wengi wanaotokea ndani ya chama chao kwa sababu ya kutowachagua nawakati wananchi wanawapenda na wanaweza kuongoza.
"Jamani viongozi na wanachama wenzangu wapitisheni wagombea wanaokubalika ili kuepuka kufanya kazi kubwa ya kuwanadi wagombea wakati wakapeni" Alisema mjumbe huyo wa Nec
Kwa upande mwingine Katibu wa chama cha mapinduzi ccm wilaya ya korogwe vijijini Jumanne Kitundu aliwataka wanaccm kutengeneza chama bila kumuonea mtu ili kuepuka kasumba za migogoro ya hapa na hapale inayoweza kujitokeza ndani ya chama.
Kitundu aliwashauri viongozi wa ccm kutotumia muda mwingi kutatua migogoro isiyo kuwa ya lazima badala yake waimarishe jumuiya zote ili kuweza kudumisha uhai wa chama na badae waweze kuingia katika uchaguzi wa serikali za mitaa wakiwa imara .