Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

‘Mtanzania’ akamatwa kesi ya utumwa Uingereza'

$
0
0


Polisi wakiwa nje ya moja kati ya majengo yanayohisiwa kutumika kama makazi ya mke na mume waliokamatwa Alhamisi kwa tuhuma za kujihusisha na utumwa. Mmoja kati ya watuhumiwa hao ametokea Tanzania. 
PICHA | LEON NEAL-AFP 
London. Mmoja kati ya watuhumiwa wawili wanaoshutumiwa kuwashikilia wanawake watatu katika mazingira ya utumwa kwa miaka 30 mjini London anatokea Tanzania, polisi Uingereza wamesema Jumamosi.
Kamanda wa polisi wa London Steve Roadhouse amesema watuhumiwa hao, ambao ni mke na mume wenye umri wa miaka 67, ni wahamiaji waliokwenda London kwenye miaka ya 1960 kutoka India na Tanzania.
Polisi wanahisi watuhumiwa hao walikutanishwa na wanawake hao watatu katika “harakati za kisiasa” zilizopelekea waanze kuishi “kijamaa” kwenye nyumba moja.
Haijulikani hali ilibadilika vipi, lakini inaelekea kwenye miaka ya 1980, kibao kilibadilika, na wanawake hao watatu wakajikuta wakigeuzwa vitwana wa timu hiyo ya mke na mume.
“Tumeanza kuwachunguza wahusika wote katika kikundi hiki cha kijamaa,” Kamanda Roadhouse alisema mapema Jumamosi na kuongeza, “Tunatazama jinsi walivyofanya kazi.”
Kesi hiyo ya utumwa ambayo imezigusa nyoyo za mamilioni dunia nzima ilianza kurindima Oktoba 25 baada ya mmoja kati ya watumwa hao kupiga simu kituo cha wahisani akiomba msaada, jambo lililopelekea polisi kuanzisha uchunguzi uliofanikisha kuokolewa kwao.
Wanawake hao walioishi katika mazingira ya utwana wa kutisha kwa miongo mitatu, ambao majina yao hayajawekwa wazi, wanatokea Malaysia, Ireland na Uingereza. Taarifa ya polisi inasema umri wa watumwa hao ni miaka 67, 57 na mdogo kabisa ni mwanamama wa miaka 30.
Mke na mume waliokamatwa Alhamisi katika sakata hili la utumwa walishawahi kunaswa katika mtego wa polisi kwenye miaka ya 1970, ingawa polisi hawakuweka wazi walitenda kosa gani.
Vilevile, wanahisiwa kuhusika katika kile polisi walichokiita “makosa ya uhamiaji,” na katika kutoa “huduma za kazi za shurti.”  Wote wameachiwa kwa masharti hadi Januari 2014 huku uchunguzi ukiendelea.
Chanzo Gazeti Mwananchi 

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles