WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowasa, leo asubuhi amewataka waendesha pikipiki (bodaboda) wa wilaya zote za jijini Dar es Salaam ambazo ni Ilala, Temeke na Kinondoni kununua pikipiki zao badala ya kuendelea kutumia pikipiki zinazowatajirisha watu wengine ambao wanazimiliki. Lowasa ambaye ni Mbunge wa Monduli aliwataka waendesha bodaboda hao kuanzisha vyama vya kuweka na kukopa (Saccos) ambazo zitawasaidia kujiongezea kipato na kujinunulia pikipiki zao na kuachana na kuendesha pikipiki za matajiri.
↧