Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

MBUNGE MAARUFU WA CHADEMA ZITTO ALIPOMJIBU DR. SLAA LIVE BILA CHENGAZZZ!!

$
0
0


Kufuatia ONYO alilopewa Zitto kutoka CHADEMA, kupitia kwa katibu mkuu wa chama hicho, la kutaka maandamano yanayo fanywa kwa ajili ya Zitto kusitishwa mara moja, kwa kuwa inadhaniwa kuwa ni Zitto ndiye mwenye kuratibu maandamano hayo. NOW GUESS WHAT, Zitto atoa ya moyoni kuhusu hilo.

Zitto katika kumjibu Dr Slaa kwanza alishangazwa sana na ufahamu wa mzee huyo (Dr Slaa) kuhusu katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania. 

Zitto alisema hivi, "katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania  inatoa ruhusa kwa Mtanzania yeyote kutembea ndani ya mipaka ya JMT na kuonana na mtu/watu uwapendao", kisha aliendelea, "na hivyo ndivyo mimi nafanya, nawatembelea wananchi na kujadiliana nao mambo mbalimbali ikiwemo yanayohusu maendeleo yao na ya nchi kwa ujumla", pia aliongeza, "na suala la wao kuandamana ni haki yao ya kikatiba, hivyo nashangazwa na wanaotaka kuizuia haki hiyo".


Nimekuja kuzungumza nanyi wanakigoma kwa Mujibu wa katiba ya chama,kama Katibu Mkoa alivyoeleza na katibu wa chadema hapa Kigoma mjini.Hivyo msithubutu kusikia propaganda zozote zile eti nitawajibishwa kwasababu ya kufanya mikutano nje ya Kigoma kaskazini,katiba ya chama inaniruhusu na katiba ya nchi inaniruhusu pia kwenda popote na kufanya chochote bila kuvunja sheria.Wote mnakumbuka nilichukulia kadi kwenye uwanja huu mwaka 1993 nikiwa na miaka 16,Nimepata Ubunge nikiwa na miaka 29 kwenda kuwawasilisha wananchi wangu wa kigoma kaskazini na nchi nzima.Mnakubaliana nami namna nilivyokuwa kiongozi bora ndani ya bunge,Kuanzia hoja ya Buzwagi,Kumng'oa waziri mkuu na sasa Mabilioni ya Uswis.Pia namna nilivyopigania ujenzi wa rami mkoa wa Kigoma,Lakini lengo langu ni kutaka siku zote wanakigoma mjivunie kutaja kuwa ww ni mzawa wa kigoma,na nimeshaijenga heshima hiyo.
Lakini ndugu zangu Ng'ombe akiumizwa malishoni anakimbilia zizini,Nimekuja Nyumbani kuzungumza na wananchi wangu,Ndani ya chama nimeumizwa,Nimevumilia sana kwa mikuki ninayopigwa na wenzangu ndani ya chama.Uchaguzi wa ndani ya chama wa Uliopita nilijitosa kugombea Uenyekiti,Lakini wazee wa chama wakaniita nimuachie mwenzangu awe mwenyekiti,NIKAKUBALI.Lakini kunavijana wamesurubiwa ndani ya chama kwasababu tu wamekuwa wakiniunga mkono,Mchange Habib alishinda uchaguzi wa Umoja wa Vijana,Lakini matokeo yake yakafutwa na kupewa mtu mwingine,Kwasababu yangu.Akina Kafulila pia walishughulikiwa ndani ya chama kwasababu ya Kudai haki,Bahati mbaya sana Kafulila akaondoka kwa hasira chadema,MIMI NITAPIGANIA HAKI YANGU kwa sababu ndani ya chadema kuna jasho langu,Kunanguvu na mali zangu nilizopigania,Kuna watanzania waliopigwa risasi,mabomu na wengine kufariki kwasabau ya kupigania chadema,KUONDOKA CHADEMA NIKUWASALITI WAPIGANIA HAKI,KUWASALITI WALIOKUFA KWASABABU YA KUIPIGANIA CHADEMA ISIMAME HADI HAPA ILIPO.












Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>