↧
JOYCE KIRIA AFUNGUKA YAKE YA MOYONI, KAMA UNATAKA KUJUA SOMA HAPA KAELZA KILA KITU
"MAELEZO YANGU HAYA YATAONDOA UTATA WOTE NA HOPE MTANIELEWA"
1. Ndoa ya kwanza nilichangisha kama UTAMADUNI wa wengi kwenye jamii yetu...
2. Ndoa ya pili.(BOMANI/SERIKALINI)Mungu akanikutanisha na Henry Kilewo anaejua nini maana ya Mke, anaeniheshimu na kunitunza, anaenipenda na kunijali.
3.KUMUHUSISHA MUNGU KWENYE TENDO/ KUBARIKI NDOA..
Ningekuwa na mawazo mgando ningefanya sherehe ya kukata na shoka.. kwanza kutetea jina langu(umaarufu mavi) na kuwazodoa waliochonga sana kwamba kanisa nitalisikia kwenye tv na redio na magazeti)
Mimi Joyce Kiria namshukuru Mungu amenipa Akili za Maisha siyo za darasani za kukopi na kupesti. Nilizotumia wakati ule ikala kwangu!
HITIMISHO.
Kwa kuwa hatukufanya Sherehe na uwezo tunao, mwakani tutawapeleka Shule watoto kadhaa wenye uhitaji kwenye jamii yetu. Yule binti aliyeshindwa kufanya mtihani wa 4m4 kule rombo, tutampeleka private kwa sababu walisema hawana uwezo huo ndo maana alikuwa tayari kuendelea kusoma wakati mtoto akiwa na wiki kadhaa toka azaliwe, wale watoto 3 wa Stela aliyekatwa mkono huko dodoma kama unawakumbuka, watoto 2 wa Gati Chacha aliyekatwa mguu huko Tarime Mara n.k
↧