Unaambiwa wiki moja baada ya staa wa muziki Kenya (Jaguar) kuonyesha gari lake jipya aina ya Jaguar ambalo alionekana nalo alipokwenda kufanya show, zimetoka picha za nje ndani za gari analotembelea rapper CMB Prezzo wa Kenya ambae mara kadhaa waliingia kwenye headlines na Jaguar kwa malumbano mbalimbali ikiwemo kutambiana muziki, mali na uwezo wa kifedha.
Gari la Jaguar lenye thamani ya shilingi Milioni 16 za Kenya ambalo liko mwisho wa hii post, aliiingia nalo kwenye uwanja pembeni kabisa ya jukwaa alipokwenda kufanya show ambapo alishuka kwenye gari wakati time yake ya kupanda jukwaani ilipofika, alikua kalipaki karibu kabisa na ngazi za kupandia jukwaani.
Hili hapa chini ndio gari jipya la Jaguar.