Dar es Salaam, Tanzania.Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimesema kwamba mwanachama yoyote anayetangaza nia ya kuwania urais kabla ya muda mwafaka kutangazwa anapoteza sifa ya kuwa mgombea.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Mnauye amesema kwamba chama hicho kinaamini katika umoja na mshikamano na kwamba wanaotangaza nia ya kugombea urahisi kabla ya muda wamepoteza sifa kwa kuwa ni kama wanakigawa chama tawala.
Juzi Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa alitangaza nia ya kugombea urais kiana kwa maana kwamba hakuweka wazi, lakini wengi walitafsiri kwamba alitangaza kugombea urais.