Rais wa bendi maarufu mjini ya Jahazi Modern Taarab al – maarafu kwa jina la Mzee Yusuph amejikuta akiingizwa mjini na matapeli maarufu kwa jina la WAPIGAJI na kukalishwa katika ofisi zao za kupigia zilizopo maeneo ya salender Bridge jijini Dar es salaam.
Habari kutoka mtaani zinasema kwamba matapeli hao waliojifanya wanajishughulisha na masuala ya utoaji wa tenda walimpigia simu Mzee Yusuph kisha kumueleza ishu nzima ya kutaka kumpa tenda ya kuweka mabango barabarani, baada ya Mzee Yusuph kukubali wakamwambia aende kwenye ofisi zao zilizopo maeneo ya Salender Bridge Upanga – Magharibi kwa ajili ya kusainishana mikataba ya kupata hiyo tenda.
mtonyaji anaendelea kunyetisha kwamba siku ya Jumatatu Mzee Yusuph alifika katika ofisi hewa hizo kisha kutoa kiasi kinachokadiriwa kufikia takribani milioni 10 na kuwapitia wapigaji hao ndipo walipomwambia awasubiri nje ya ofisi ili waweze kuongozana nae kwa minajili ya kwenda kusainishana mikataba lakini cha ajabu na kushangaza wapigaji hao walimweka nje ya ofisi hizo bila wao kutoka hata alipojaribu kuwaangalia tena akakuta ofisi zimefungwa na jamaa hao kutokomea mahali kusipojulikana.,
Taarifa zinadai kwamba Mzee Yusuph amewafungulia jalada la kesi ya utapeli dhidi ya matapeli hao na yupo katika msako mkali wa kutaka kurudishiwa mkwanja wake huo na kuwakamata watu hao.
Source:- Umbeya Blog