KITENGO Cha Usalama wa Taifa Nchini kinatarajia
kuogeza nguvu katika kuimarisha ulinzi katika
viwanja vya ndege nchini ili kukabiliana na wimbi
kubwa la usafifirishaji wa dawa za kulevya pamoja
na madini hapa nchini hususani katika kiwanja cha
ndege cha kimataifa Mwalimu Julius Nyerere (JNA)
kilichopo jijini Dar es Salaam.
Akiongea na menejimenti ya Mamlaka ya Viwanja
vya ndege katika ofisi za uwanja wa kimatifa
Mwalimu Julius Nyerere jana ,Waziri wa Uchukuzi
Dk Harrison Mwakyembe alisema mipango mikakati
ni pamoja na kushirikisha vyombo vingine, kama
vile uhamiaji,polisi , kitengo cha dawa za kulevya
nchini,polisi jammii na raia wema wa kawaida
watakaotoa taarifa zitakazofanikisha kukamatwa
kwa matukio ya kupitisha maidini na dawa za
kulevya .
DK. Mwakyembe alikwenda katika viwanja hivyo
kufuatia kuwepo na taarifa ya kukamatwa kwa
mwanamke mmoja akiwa na hati ya kusafiria
AB548424 aliefahamika kwa jina la Salama Omary
Mzala (30) mkazi wa Mbagala jijini Dar es Salam,
aliekamatwa akiwa amemeza pipi 67 za dawa aina
ya heroine.
Vyombo vya usalama Kumtilia shaka na kuweza
kufuatilia hadi katika ndege aliotakiwa kupanda ya
Ethpoia Airline tayari kwa kuelekea Maccau Nchni
China na kumuweka katika ulinzi ambapo kwa
mujibu wa taaarifa toka kwa kamanda wa kikosi cha
kuzuia na kupamabana na dawa za kulevya nchini
Godfrey Nzowa hadi kufikia saa 7.30 mchana
,Mzala alikuwa ametoa pipi 28 kwa njia ya haja
kubwa ambapo naendelea kutoa kadri muda
unavyozidi kwenda .
Akitoa takwimu za kupitisha dawa na madini kupitia
kiwanja hicho Dk. Mwakyembe alisema vitendo vya
kutorosha madini kuanzia Oktoba hadi December
kesi 14 zililipotiwa wakati kuanzia August hadi
Desemba mwaka jana matukio nane ya dawa za
kulevya yaliripotiwa ambapo watano wa wahusika
katika matukio hao ni watanzania.
Akiongea kwa njia ya simu kamanda Nzowa alisema
kukamatwa kwa binti huyo kunatokana na kupeana
taarifa kiulimwengu ambapo kuligana na teknolojia
iliopo hivi sasa mtu anaweza kukamatwa mahali
alipo hata kabla ya kusafiri kwende nchi nyigine.
Aidha anaunga mkono jitihda za Rais Jakaya
Kikwete za kuleta maadiliko makubwa katika vita
vya kuthbiti na kupambana na dawa za kulevya
nchini ili kukomesha biashara hiyo.
Alitoa agalizo kwa wananchi kutojiusisha na kilimo
cha aina yoyote ya dawa za kulevya bdala yake
wageukie kilimo cha mazao ya biashara na chakula.
Alitoa takwimu ya dawa za kulevya zilizokamatwa
nchini Kamanda Nzowa alisema Mwezi wa saba
pekee kilo 182 za heroine zilikamatwa na hadi
kufikia mwisho wa mwaka jana jumla ya kilo 1482
za heoroine zilikamtatwa kitu ambaho na hatari.
“tunaendelea kupambana hadi kukomesha kwa
biashara hizi kwani watu hawa (wafanyabiashara ni
wajanja sana hubadilisha mbinu kila wakati na sisi
hatulali”alisema Kamanda Nzowa.
Mwishoo……………………………………