Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Kabwe, akionekana mwenye wasiwasi mara baada ya Jaji John Utamwa wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, kutoa hukumu katika shauri lake la zuio la kutaka kutokujadiliwa na Kamati Kuu ya chama hicho, Dar es Salaam, ambapo katika shauri hilo aliibuka mshindi.
Zitto Kabwe, akipeana mikono na Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lisu ndani ya Mahakama Kuu
Wafuasi wa Zitto Kabwe wakishangilia na kuonesha ishara ya kushinda katika shauri hilo.
Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lisu, akiwatuliza wafuasi wa chama hicho baada ya kushindwa katika shauri hilo na Zitto Kabwe.
Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), wakiwa katika ulinzi mahakamani hapo
Mashabiki wa Zitto Kabwe, wakishangilia ushindi wake baada ya kuubwaga uongozi wa Chama chake cha Chadema.Picha Kwa Hisani ya michuzi Blog