Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

MDAU NAMBA MONA WA TWANGA PEPETA SUGU ALIPOZIKWA LIVE!!

$
0
0

DADDY BROWN WA TWANGA PEPETA ALIVYOZIKWA JANA JIONI

MDAU mkubwa wa Twanga Pepeta na muziki wa dansi kwa ujumla, Daddy Brown (pichani juu) aliyefariki ghafla juzi jijini Dar es salaam, alizikwa jana jioni nyumbani kwao Kibaha Misugusugu kata ya Miyomboni.

Daddy Brown ambaye jina lake kamili ni Ismail Mohamed Hamis alikuwa ni mmoja wa viongozi waandamizi wa camp ya Usher Family ya Temeke ambayo majuzi ilisherehekea miaka 14 ya kuzaliwa kwao.
Usher Family ni moja ya nguzo kubwa ya Twanga Pepeta kwa eneo lote la Temeke.
Marehemu ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 42 ameacha mtoto mmoja wa kike.

Mwili Daddy Brown ukifanyiwa sala ya mwisho
Daddy Brown alifahamika kama mmoja wa wanaharakati wa muziki wa dansi aliyekuwa mpiganaji na bingwa wa mikakati.
Alisifika zaidi kwa kucheka na kila, muda wote tabasamu lilikuwa halibanduki usoni mwake.
Mirinda nyeusi (mwenye cheni) akishiriki mazishi
Daddy Brown ni mmoja wa wadau ambao wamekuwa wakitajwa katika nyimbo nyingi za Twanga Pepeta kama moja ya njia kutukuzwa kwa harakati zake.
Usher Family iko chini ya meneja wa Twanga Pepeta Muddy K ambaye ni rafiki mkubwa wa marehemu – urafiki wao ulipitiliza, ni kama pete na kidole, mara chache sana kuwakuta hawako pamoja. Wamekuwa hivyo kwa zaidi ya miaka 14.
Muddy K (mwenye fulana nyeusi) rafiki mkubwa wa marehemu
Marehemu alikuwa akiishi Temeke lakini mauti yalimkuta Kimara kwa dada yake alipokuwa amekwenda kusalimia.
Akiwa huko alishikwa na malaria na kupelekwa hospitali ambako alitundikiwa drip lakini baadae akaruhusiwa kurudi nyumbani (kwa dada yake) kabla ya hali kubadilika tena na kufariki.
Katika mazishi hayo yaliyohudhuriwa na wadau na wanamuziki wengi, Twanga Pepeta iliwakilishwa na mmoja wa wakurugenzi wake, Omar Baraka.
Omar Baraka
Saluti5 inawapa pole ndugu, jamaa na marafiki wa Daddy Brown kwa msiba huu mzito. Pumzika kwa amani Daddy Brown.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>