Mwanza, Tanzania. Diwani wa Chadema, Kata ya Nyamanoro, Aboubakary Kapera jijini Mwanza Amemfungia Ofisini Kwake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela, Zuberi Mbyana kwa hoja kwamba anachelewesha shughuli za maendeleo.
Awali Aboubakary na madiwani wenzake wanne wa Chadema walikuwa kwenye ofisi ya Mkurugenzi huyo, lakini alitoka nje ya ofisi hiyo na kurejea na kofuli na kuwafungia ndani ya ofisi hiyo.
Updates..
Madiwani wa Chadema waliokuwa wanashiliwa katika Kituo cha Polisi Kirumba Wameachiwa Huru, akiwamo Mbunge wa Ilemela, Highnes Kiwia.
Wamechiwa Huru baada ya Wafuasi na Wanachama wa Chadema kufurika kwa wingi katika kituo hicho ili kushinikiza waachiwe huru.
Mashabiki, Wafuasi na Wanachama wa Chadema nje ya kituo hicho walikuwa wakiimba 'Mungu Ibariki Chadema na Viongozi Wake.'
Kutokuelewana Kati ya madiwani hao na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ilemela kulianza LEO saa 4.45 asubuhi na madiwani walifika katika ofisi za halmashauri ya wilaya ya Ilemela kwa ajili ya kushiriki kikao maalum cha kupitisha bajeti ya mwaka 2014/15.
Baada ya kufungiwa kwa mkurugenzi huyo, mgambo wa halmashauri walimshikiza Diwani Kapera kumfungulia mlango mkurugenzi na hali ilibadilika na diwani huyo kurushiana ngumi na Mstahiki Meya wa Ilemela, Henry Matata.
UPDates:
KIKAO CHA BAJETI 2014/15. : Madiwani warushiana makonde Mwanza
Vurugu kali zimezuka katika kikao cha cha mapitio ya bajeti ya manispaa ya Ilemela kwa mwaka wa fedha 2014/15.
Vurugu hizi zimeambatana na hatua ya madiwani wa Chadema kumfungia ndani ya ofisi yake Mkurugenzi wa manispaa ya Ilemela Zuberi Mbyana wakishinikiza kurejeshwa kwa madiwani waliofungiwa kushiriki vikao katika manispaa hiyo.
Wakati huo huo Kufuatia kuikataa bajeti ya mwaka wa fedha 2014/15 baraza la Madiwani wa halmashauri ya jiji la Mwanza limewasimamisha watendaji wanne wa idara ya mapato ya jiji kwa upotevu wa shilingi milioni 28.
Mbali na watumishi hao mweka hazina wa jiji la Mwanza amepewa onyo la miezi mitatu huku akichunguzwa muenendo wake katika utumishi.
UpDates:
Hali si shwari katika manispaa ya ilemela mkurugenzi yuko chini ya ulinzi baada ya ofisi yake kupigwa kufuli na madiwani wa Chadema hali inayopekea tafrani mahali hapa.
Hatimaye hali inatengemaa,kati ya madiwani 13 walio katika kata hii ni madiwani watano pekee wanafanikiwa kupitisha bajeti hii kabla ya kikao kufikia tamati.
Kando baada ya kikao cha baraza, Chama cha Demokrasia na Maendeleo Kinakiri kufanya kitendo hicho ili kufanikiwa azma yao ya kurudishwa kwa madiwani wa kata za Ilemela,Kirumba na Nyamanoro.
Kamati ya Fedha ya baraza la madiwani jiji la Mwanza inalazimika kukutana tena kujadili hoja ya ukusanyaji mapato kabla ya kukutana na kisanga cha kuwepo kwa ubadhilifu.
Baada ya masaa takribani 6 huku vikao vya kamati za fedha na nidhamu vikishika hatamu baraza linakutana na kutoa maazimio haya.