Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

THE MAJANGAZ:- JANA HUKO MAMBELEZZ ILIKUWA SIKU YA KUTOKUVAA SURUALI KWA WAKE KWA WAUME LIVE!!

$
0
0

Wapanda treni za mijini ulimwenguni walikuwa na siku nyingine ya kutoka na kusherehekea siku ya kuacha sehemu za miili yao wazi kuanzia kiunoni kwenda chini kwa kutokuvaa suruali jana, ikiwa ni kuadhimisha kwa mwaka wa 13 maarufu kama “No Pants Subway Ride”

Siku hiyo husherehekewa tarehe 12 januari kila mwaka kwa nchi zenye usafiri wa treni mijini.

Wasafiri na watumiaji usafiri huo wa mjini katika miji mikubwa ya Sydney(Australia), Beijing na Hong Kong(China) waliingia kwenye usarifi wa treni na tram waliushangaza ulimwengu wakiwa hawana suruali, jambo ambalo limeanza kuenea katika miji mingi duniani tokea ianzishwe na kundi la Wamarekani linalojiita Improve Everywhere in New York (imarisha kila kitu New York) 2002.

Kwa mujibu wa mtandao wa Yahoo News, miaka 12 iliyopita, ni watu 7 tu ndio walishiriki katika kuzindua tukio hilo lakini sasa hivi ni maelfu ya watu katika miji mikubwa duniani wanashiriki katika kinachoitwa “mahadhimisho ya upumbavu”


Utaratibu ni mrahisi tu, washiriki wanakutana katika njia maalumu waliyo kubaliana kila mwaka bila kuwa na suruali na kuanza safari kwa kutumia reli au barabara na kushtua watu huku wakicheka

Chupi lazima zivaliwe, pamoja na kwamba chupi za mitindo mbalimbali zinakubalika, waandaaji hupenda kukagua wahusika wote mapema angalau kuanzia kiunoni kwenda juu ili kuhakikisha watu hao wamevaa kama siku za kawaida.
PICHA ZAIDI...

Sare za kazini pamoja na suti za maofisini hukubalika zaidi ili kuonesha zaidi tofauti katika miili yao na haswa wakiwa na baskeli, mikoba ya ofisini(briefcase), mifuko ya shoping na kadhalika.


Washiriki pia hawaruhusiwi kusemeshana na washauriwa kuwa na kitu cha kufanya ukiwa kwenye treni mfano kusoma magazeti, vitabu, kufuma n.k.

"washiriki hamtakiwi kufahamiana au kuonesha mnafahamiana. Ukiulizwa jibu ni kwamba ulisahau kuvaa suruali” mwaandaaji alitoa masharti kwa washiriki kabla ya shughuli nzima kuanza huko Sydney, Australia.

"sisitiza kuwa imetokea tu kwamba na mwenzio pia alisahau kuvaa suruali kama wewe, kuwa mcheshi na mpole” aliongeza

 Washiriki wa siku ya kutovaa suruali Beijing, China

 Washiriki wakiwa kwenye treni Hong Kong


Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles