Ujumbe wa Viongozi wa dini wakiangalia mojawapo ya visima vya nchi kavu vya kusafisha gesi katika eneo la Mnazi Bay, Mtwara.
Viongozi wa dini wametembelea Bomba Jipya la Gesi asilia la Mtwara- Dar es Salaam, mtambo wa kusafisha umeme wa Mnazi Bay na maeneo mengine mbalimbali ya uendelezaji wa gesi asilia katika Mkoa wa Lindi na Mtwara.
Viongozi hao wamefanya ziara hiyo ikiwa ni maandalizi kabla ya kufanyika Kongamano la Viongozi wa dini linalotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam tarehe 21 na 22 mwezi Januari, 2014.
Mafundi wa Kampuni ya China Petroleum Pipline (CPP) wakiendelea na kazi ya kuunganisha mambomba ya gesi katika kambi ya Madangwa.