Hashim Donode mzee wa Oldies akitoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band sambamba na Digna Mbepera pamoja na Winnie kwenye show yao ya Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.
Divas: Mary Lucos na Winnie wakiwapa raha fans wa Skylight Band.
Sam Mapenzi akifanya yake jukwaani.
Happy Birthday to you...... Happy Birthday dear Joti..........Happy Birthday to you....Shabiki wa Skylight Band anafahamika kwa jina la Joti (mwenye shati la kaki) alijumuika na marafiki zake kusheherekea siku yake ya kuzaliwa ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.
Skylight Band wakiendelea kutoa burudani na staili yao ya "Yachuma chuma".
Birthday boy Joti akijimwaga na marafiki zake na sebene la Skylight Band.
Warembo wakionekana kuchizika na Skylight Band.
Rappa Joniko Flower akitoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band.
Umati wa mashabiki wa Skylight Band ukisebeneka ndani kiota Thai Village.
Digna Mbepera sambamba na Winnie wakitumbuiza mashabiki wa Skylight Band.
Mary Lucos akicheza na kuimba na mashabiki wa Skylight Band.
Ilikuwa full mzuka kwa mashabiki wa Skylight Band....Usipime na sio ya kukosa leo jioni pale pale muda ule ule....,mpango mzima.
Rappa Joniko Flower akioyesha zawadi ya kinywaji cha PATRON kwa mashabiki wa Skylight Band ambapo mwanadada atakaye sebeneka vizuri atajishindia kinywaji hicho.
Kutokana na mapenzi kwa makubwa kwa mashabiki wa Skylight Band Mmiliki wa Band hiyo Dr. Sebastian Ndege a.k.a JEMBE aliamua kutoa kinywaji chake hicho kama zawadi kwa mwanadada atakayecheza vizuri staili za bendi hiyo.
Mzigo huu hapa kazi kwenu....Vijana mate yanawatoka.
Vijana wa Skylight Band wakionyesha staili zao kwa mashabiki wao.
Mashabiki wakiangalia kwa umakini staili hizo.
Warembo wakionyesha makeke yao kwenye jukwaa la Skylight Band.
Mchujo ukiendelea.... Wakaona hawaelekei ikabidi Aneth Kushaba AK 47 awaonyeshe manjonjo yake.
Hapo je.....vijana wameiva sasa....
Mashabiki wa Skylight Band ambao ghafla waligeuka kuwa mashabiki wa kuamaua nani mshindi..kwa umakini wakifuatilia burudani hiyo.
Sony Masamba akionyesha staili mpya ya Skylight Band kwa mashabiki.
Warembo wakifanya yao jukwaani.
Mwishowe hawa ndio waliotinga fainali......na kutoka ngoma droo..tofauti ni maumbile tu lakini wote wakali.
Walipatikana washindi wawili waliotoka ngoma droo kutokana na majaji ambao ni mashabiki...Pichani Sony Masamba akipata Ukodak na washindi hao huku Aneth Kushaba AK 47 (aliyeipa mgongo camera) akiwa hana mbavu.
Baada ya zoezi hilo burudani iliendelea ni mwendo wa mduara tu....mambo ya kuzungusha nyonga wadada mpooo pale kati...???
Aneth Kushaba AK47 na shabiki wake.
Petit Man na Winnie wakishow love ndani ya kiota cha Thai Village.
Hashim Donode na Digna Mbepera wakipata Ukodak back stage.
Wadau wa ukweli ndani ya Skylight Band Ijumaa iliyopita kwenye kiota cha maraha Thai Village.