King MajutoDar es Salaam, Tanzania. Msanii nguli wa filamu za vichekesho anayedaiwa kuwa mwenye mvuto zaidi katika kuigiza, King Mjuto ameingia mkataba na kampuni ya kusambaza filamu ya Steps ambao kuanzia sasa unambana kuonekana kwenye filamu za kushirikishwa. Kwa mujibu wa meneja wake, Hamza Majuto ni kwamba msanii huyo kwa sasa atakuwa akifanya filamu zake mwenyewe.