Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

WABUNGE WA CCM WAHAHA HUKU NA KULE WENGINE KWA WACHAWI NA UWAZIRI WA JAKAYA CHECK THIS OUT LIVE!!

$
0
0
 
 
Rais Jakaya Kikwete:-
 
WAKATI Rais Jakaya Kikwete akitarajiwa kutangaza mabadiliko ya Baraza la Mawaziri muda wowote kuanzia sasa, baadhi ya wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wanadaiwa kuishi kwa hofu huku kila mmoja akitaka kujua hatima yake.

Katika mabadiliko hayo yanayosubiriwa kwa shauku kubwa na Watanzania, Rais Kikwete, anatarajia kujaza nafasi zilizo wazi ambazo alifuta uteuzi wa mawaziri wake wanne, huku aliyekuwa Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa, akifariki dunia.

Hata hivyo, mawaziri waliong’olewa hivi karibuni ni kutokana na tuhuma za ukiukwaji wa haki za binadamu, zilizoibuka wakati wa Operesheni Tokomeza Ujangili.

Mawaziri ambao uteuzi wao ulifutwa na Rais Kikwete na kutangazwa bungeni na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ni Balozi Khamis Kagasheki (Maliasili na Utalii), Shamsi Vuai Nahodha (Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa), David Mathayo (Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi) na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi.

Tangu lilipotokea tukio hilo, baadhi ya wabunge CCM ambao imekuwa ikielezwa waliitwa Ikulu na Rais Kikwete kwa ajili ya mahojiano na wamekuwa wakiishi roho juu, huku kila mmoja akitaka kujua hatima yake kama ameingia katika Baraza la Mawaziri ama hajaingia.

Mbali ya nafasi za kundi hilo, Rais Kikwete anatarajiwa kuwatema baadhi ya mawaziri wanaodaiwa kuwa ni mizigo, hali iliyoilazimu Kamati Kuu ya CCM (CC), kuwaita na kuwahoji kutokana na utendaji wao unaolalamikiwa na wananchi.

Mawaziri hao walilalamikiwa na kuitwa mizigo katika ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.

Waliotajwa kuwa ni mawaziri mizigo ni Waziri wa Kilimo na Chakula, Christopher Chiza, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Hawa Ghasia na aliyekuwa Waziri wa Fedha, marehemu Dk. William Mgimwa ambaye hakuwapo katika kitimoto, hali iliyomlazimu Naibu Waziri wa Fedha, Saada Mkuya kwenda kwa niaba yake.

Katika mabadiliko hayo, Rais Kikwete anatarajiwa pia huenda akawatema ama kuwahamisha wizara mawaziri walio nje ya kundi la mizigo, kama njia ya kuleta ufanisi katika utendaji wa Serikali yake.

“Pamoja na kuitwa katika mahojiano na Rais Kikwete Ikulu, lakini hadi sasa hivi sijajua nini kinachoendelea maana kwa sasa ni balaa. Haijulikani maana sasa hali imekuwa tete, kila mmoja ana shauku ya kutaka kujua nani ameingia na nani anatoka,” alisema mmoja wa wabunge wa CCM ambaye hakupenda kutajwa jina lake gazetini.

Inadaiwa wabunge hao wamekuwa na hofu, baada ya kuona muda mrefu umepita baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Bunge uliosababisha kujiuzulu kwa mawaziri wanne.

Hata hivyo, ilielezwa kuwa wakati Rais Kikwete akiwa katika harakati za kusuka baraza jipya, ghafla alipata mtikisiko kwa kuondokewa na Dk. Mgimwa aliyefariki dunia Januari Mosi, mwaka huu, nchini Afrika Kusini alikokuwa akitibiwa.

Vyanzo vya uhakika vimelieleza gazeti hili kuwa, Rais Kikwete alitarajiwa kutangaza bazara jipya baada ya mapumziko ya Sikukuu ya Mapinduzi.

Pamoja na hatua hiyo, ilielezwa kuwa katika mapumziko hayo, Rais Kikwete aliyatumia kwa kukutana na Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwa ajili ya majadiliano ya kufanya uhakiki wa mwisho wa majina ya wanaotarajiwa kuingizwa katika baraza jipya.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>