Source:- millardayo
:
Majambazi kumi wanaodaiwa kumuua Dr. Segondo Mvungi wamefikishwa kwenye Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu na kusomewa shitaka la kumuua Dr. Mvungi.
Kesi imesomwa na Hakimu Mkazi Sundi Fimbo ambapo Watuhumiwa hawakutakiwa kujibu chochote kutokana na Mahakama kutokua na uwezo wa kusikiliza kesi ya mauaji hivyo wanarudishwa Segerea mpaka tarehe tano December kwa ajili ya kesi kutajwa.