..................................................
NA DIANA BISANGAO WA MATUKIO DAIMA.COM, IRINGA
JESHI la polisi mkoani Iringa linawashikilia watu wawili kwa makosa mawili tofauti likiwemo la Wilson Mbilinyi (25) mkazi wa Barabara mbili kata ya Makorongoni wilaya ya Iringa kukutwa na madawa ya kulevya.
Akizungumza na mtandao wa www.matukiodaima.comofisini kwake Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Ramadhani Mungi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea januari 16 majira ya saa 5 kamili asubuhi.
Mungi alisema mtuhumiwa huyo alikutwa na kete 15 zinazozaniwa kuwa ni madawa ya kulevya aina ya kokeini.
Wakati huohuo jeshi la polisi mkoani Iringa lilimkamata raia wa Ethiopia Dasala Halute (20) kwa kosa la kuingia nchini bila kibali.
Kamanda Mungi alisema tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 16 januari mwaka huu majira ya saa 3:30 usiku maeneo ya Ipogolo kata ya Ruaha.
Credit: www.matukiodaima.com