Sunday, January 19, 2014
MAJI YANAVYOMKARIBIA SHINGONI MANJI YANGA
KUNA tawi moja la Simba SC pale Magomeni, linaitwa Mpira Pesa, maana yake soka ni mchezo wa fedha. Wenye tawi hilo waliamua kuliita hivyo kupingana na dhana ya viongozi hohe hahe kupewa dhamana ya kuongoza klabu, wakiamini hawawezi kumudu gharama za uendeshaji klabu.
Kweli, mpira unahitaji wenye fedha. Klabu zinahitaji fedha kujiendesha. Fedha za udhamini wa Tuzo zimeifufua Gor Mahia ya Kenya. Fedha za udhamini wa Mumias Sugar zimeifufua AFC Leopard na sasa soka ya Kenya imerejea kwenye ladha ya wapinzani wa jadi, Gor na Leopard.
Fedha za Sheikh Mansour zimeifanya Manchester City iwe miongoni mwa klabu maarufu duniani. Fedha za Roman Abramovich zimetufanya leo tuishuhudie Chelsea tofauti na ile ya miaka 1990.
Fedha za Moise Katumbi zimeifanya TP Mazembe iwe klabu tishio Afrika. Fedha ndiyo mambo yote katika soka na ninaungana kabisa na usemi wa lile tawi la Simba SC Magomeni, kwamba mpira pesa.
Kwa wenzetu, fedha inafanya kazi kwenye soka na matunda yanaonekana, lakini hali ni tofauti na hapa nyumbani, ukithubutu kuweka fedha zako kwenye mpira zitateketea kwa moto na lolote usipate.
Wapi Merey Balhaboub? Yu hai, basi tu havumi tena, baada ya Moro United kuchoma moto fedha zake. Alex Kajumulo alikuja Tanzania akajaribu kuwekeza, lakini mwisho wa siku alivunja timu na kuwapa wachezaji kiinua mgongo dola za Kimarekani 1,000 kila mmoja mwaka 2000, baada ya kushitukia anachoma moto fedha zake.
Azim Dewji na Murtaza Dewji nao vipi tena? Wamejitoa kwenye mpira baada ya kuchoma fedha zao na sasa wapo kando wanaendesha biashara zao na hawana hamu kabisa.
Kuna tajiri Kigoma aliwekeza fedha nyingi akaanzisha timu inaitwa Mmbanga FC, naye akachemsha. Thomas Molel ‘Askofu’ alijaribu pia kupitia Pallson, naye akatokota.
Mohamed ‘Mo’ Dewji alianza kuiokoa Simba SC mwaka 1998 kwa udhamini mzuri akaenda nayo hadi mwaka 2004 akaamua kauchana nayo. Mo ni Simba damu na katika kipindi chake alishawishi makampuni mengine pia kusaidia Simba SC, benki ya NBC na Simba Cement waliingia.
Lakini Mo alipenda kuona Simba SC inajitegemea siku moja kwa kuwa ina rasilimali kubwa, ambayo ni mashabiki wake. Hata hivyo, wazo lake zuri la kuifanya klabu ijitegemee lilipata upinzani, naye akaamua kuachana nao.
Kwa kuwa alipenda sana soka, Mo akaamua kununua timu iitwayo Mbagala Market na kuibadilisha jina kuwa African Lyon. Mo aliwekeza fedha nyingi katika timu hiyo si chini ya dola 300,000, lakini baada miaka miwili akaiuza kwa dola 40,000 tu kwa mjanja wa mjini mmoja anaitwa Rahim Kangezi ‘Zamunda’.
Zamunda naye baada ya kuwa na timu hiyo kwa miaka mitatu jasho linamtoka na watu wanasema anamtafuta mtu wa kumpa bure tu apumzike zake.
Yussuf Manji alianza kama mdhamini Yanga mwaka 2006 kabla ya mwaka juzi kuwa Mwenyekiti wa klabu. Katika kipindi chote hicho, Manji amewekeza fedha zake nyingi sana, lakini hadi sasa hakuna faida zaidi ya kero tupu.
Yanga imezidi kuwa kibonde wa Simba SC, inafungwa 5-0 na 3-1, ikijitutumua inatoa sare ya 3-3. Matokeo hayo yanakuja wakati kila mchezaji mzuri anayeonekana Simba SC anasajiliwa Yanga.
Kila mchezaji mzuri ambaye Simba wanataka kumsajili, Yanga watamuwahi wao na kumrubuni hata kama alikuwa amekwishachukua fedha na kusaini kwa wapinzani wao, watambadili mawazo na watampata. Hivyo si ndivyo ilivyotokea kwa Mbuyu Twite? Lakini wakikutana uwanjani, mwendo ule ule, Simba kidedea.
Mara ya mwisho Manji alipozungumza na Waandishi wa Habari alisema hatagombea tena uongozi atakapomaliza muda wake. Na unaweza ukadhani alikuwa anatania, lakini hata ukitazama sura yake inaonyesha ameanza kuchoka. Yuko njiani kutoka, ameshindwa. Na akitoka, atatoka moja kwa moja. Yuko wapi Mo Dewji mwingine Simba leo?
Ukweli ni kwamba, Yanga wanamchosha Manji. Wanamfanya buzi, kila dirisha la usajili atoe fedha kusajili wachezaji wa bei kubwa. Kila msimu aajiri kocha mpya, kila mechi ya Simba na Yanga atoe mamilioni ya kambi timu ikafungwe na Simba SC.
Natafakari wachezaji waliopo Yanga ya sasa namna ambavyo walikuwa bora, lakini kufika pale Jangwani viwango vimeshuka kwa sababu tu ya matatizo ambayo yanaanzia katika uongozi.
Leo Yanga wamemuajiri kocha Johannes Franciscus ‘Hans’ van der Pluijm, kisa tu eti aliwahi kuifundisha Berekum Chelsea ya Ghana na ikazitoa jesho TP Mazembe na Al Ahly ya Misri mwaka jana katika Ligi ya Mabingwa
Narudia, huyu babu si kocha mzuri na ni mzee hawezi kufundisha, na kwa kuwa hajui Kiswahili hawezi hata kutoa ushauri Kevin Yondan akamuelewa. Kule Ghana alikuwa anasikiliazana na wachezaji ambao wamekulia kwenye kuzungumza Kiingereza na bado hakuwahi kutwaa Kombe.
Kocha mzuri ni ambaye ameshinda mataji, ikibidi kushinda tuzo yeye mwenyewe binafsi na asiye na rekodi ya kufukuzwa fukuzwa, zaidi ya hapo mwenye elimu nzuri ya ufundishaji mpira, aliyesomea katika vyuo vyenye kuheshimika na kupewa leseni za bodi kubwa za soka kama UEFA.
Historia ya Franciscus Johannes ‘Hans’ van der Pluijm inasema alizaliwa Januari 3 mwaka 1949 na alianzia kwenye kucheza soka akiwa kipa.
Enzi zake aliidakia kwa miaka 28 klabu ya FC Den Bosch akicheza mechi 338 ndani ya misimu 18 na alipostaafu baada ya kuumia goti akawa kocha wa timu hiyo.
Alianza vyema ukocha akiiwezesha FC Den Bosch kutwaa ubingwa wa Daraja la Kwanza na kupanda Ligi Kuu na ndiye aliyempa nafasi ya kwanza mshambuliaji Ruud van Nistelrooy akiwa kinda wa miaka 17 tu kucheza kikosi cha kwanza cha timu hiyo.
Aprili mwaka 1995, alisaini Mkataba wa miaka miwili na SBV Excelsior kabla ya kutimuliwa Januari 1997 na nafasi yake ikachukuliwa na Msaidizi wake, John Metgod.
Hiyo ilifuatia timu hiyo ya Rotterdam kushinda mechi mbili tu na sare tatu katika mechi 17 za msimu mzima.
Baada ya kuboronga Ulaya, ndipo akahamia Afrika mwaka 1999, alipokwenda kufundisha Ashanti Gold SC ya Ghana, akianza na Mkataba wa mwaka mmoja.
Ajax ya Uholanzi ikanunua hisa katika klabu hiyo Ijumaa ya Juni 18, mwaka 1999 asilimia 51 naye akatupiwa virago na kuhamia Saint-George SA ya Ethiopia kabla ya mwaka 2010 kujiunga na B-juniors Feyenoord ya Ghana, ambayo ni tawi la timu hiyo ya Rotterdam.
Mwaka 2012 alijiunga na Berekum Chelsea ambako pia alifukuzwa mwaka jana na kuhamia Medeama ya Ghana pia ambako nako alifukuzwa baada ya mechi saba tu, kufuatia matokeo mabaya mwanzoni mwa msimu, akivuna pointi nane kati ya 21.
Akiwa Madeama alikuwa analipwa mshahara wa dola 1,800, lakini haitakuwa ajabu ukiambiwa Yanga wanamlipa zaidi ya dola 5,000. Ndiyo, fedha za Manji si zipo tu kwa ajili ya kuchoma moto na hakuna mtu mwenye uchungu nazo.
Leo mtu anafanya kampeni kwenye vyombo vya habari na viposho posho anatoa vimsifie kocha mbovu, lakini akae akijua ndiye yeye mwenyewe atakayelazimika kesho ‘kununua mechi’ si mimi Bin Zubeiry.
Tuna matatizo Watanzania, watu wanajitolea kutusaidia, lakini sisi tunawamaliza. Hata hayo mapenzi tunayodai tunayo kwa timu zetu yako wapi, ikiwa hatuwezi kutumia fedha za wafadhili kwa manufaa ya klabu?