Mambo ya nyoka ©australianbusinesstimes |
Ndege moja ya abilia ilikua imepakia abilia wapatao 240 na mizigo, lakini katika baadhi ya mizigo ndege iliyokua imepakia kukawa na nyoka wapatao 2000 waliokua wakisafirishwa kutoka Harare zimbambwe kwenda ulaya kwaajili ya kutumika kutengeneza bidhaa kama mikanda na mikoba ya akina mama
Lakini wakati wa kupakia mizigo ile wale nyoka hawakufungiwa vizuri, na ndege ilipofika juu wale nyoka wakaanza kutoka ili kutafuta hewa( Kadiri unavyopanda kwenda juu mgandamizo unaongezeka na oksijeni inapungua)
Wale nyoka wakafanikiwa kufika mpaka sehemu ya abilia, abilia walipowaona wale nyoka wengi wakaanza kupiga kelele na kuhangaika, ndipo rubani wa ile ndege alipokuja kuangalia nini kinaendelea, alipoaangalia akawaona wale nyoka wametoka na wamewazunguka baadhi ya abilia.
Yule rubani akawasiliana na kituo cha ndege kilichokua karibu ili aweze kutua kwa dharura, cha kushangaza alipowasiliana na mwongoza ndege wa mahali pale akapewa maelekezo ambayo hakuyategemea
Yule mwongoza ndege akamwambia hutakiwi kutua chini, unachotakiwa kufanya ni kwenda juu zaidi, kwasababu wale nyoka wametoka chini kwenye mizigo kuja kwa abiria kutafuta oksijeni, akitua chini wale nyoka watapata hewa nzuri na watawadhuru watu wote katika ile ndege lakini akienda juu zaidi watakosa hewa na wakakuwa dhaifu na mwisho watakufa.
Yule rubani aliafanya kama alivyoelekezwa na akafanikiwa kuwakoa watu wote
Katika maisha kuna maadui wengi wanaoweza kutaka kukuvunja moyo katika jambo unalofanya ambao wako kama hao nyoka unachotakiwa kufanya sio kujibishana nao unachokitakiwa kufanya ni kwenda juu zaidi kwa JINA LA YESU
Profesa, Mchungaji Ole Nasioki Edward
Ufufuo na Uzima.