Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all 32622 articles
Browse latest View live

JE UNAJUA KWA NINI BONGO KUNA BARABARA INAITWA SHEKILANGO ROAD? SOMA HABARI YAKE KAMILI HAP-A TENA IKIWA LIVEEEE!!

$
0
0

JE WAJUA?

HUSSEIN RAMADHANI SHEKILANGO, SHUJAA ALIYEKUFA AKIIJENGA UGANDA

Jijini Dar es salaam kuna Barabara Mashuhuri kama 'Shekilango Road', ikianzia maungio ya Barabara ya Morogoro eneo la Nyumba za NHC mkabala na Kiwanda cha Urafiki, ikipitia Mitaa yote ya Sinza na kuishia Maungio ya Barabara ya Ali Hassan Mwinyi kituo cha Bamaga.

Ni watanzania wachache wajuao kuwa Barabara hiyo ya Shekilango imepewa jina Maalum kwaajili ya heshima ya Ndugu Hussein Ramadhani Shekilango, aliyekuwa Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, akishughulika zaidi na mambo ya Utawala, wakati wa Uongozi wa Rais Julius Nyerere na Makamo wake Aboud Jumbe Mwinyi.

Hussein Shekilango alichaguliwa na Wananchi wa kwao kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Jimbo la Korogwe Mjini, Mkoani Tanga katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1975, akiachia nafasi yake ya Zamani ya Meneja Mkuu wa Shirika la Usagishaji Nchini (NATIONAL MILLING CORPORATION).

Mwaka huo huo akachaguliwa na Rais Julius Nyerere kuwa Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Utawala) akiwa chini ya Makamu wa Pili wa Rais na Waziri Mkuu, ndugu Rashid Mfaume Kawawa.

Mwaka 1977 yalifanyika Mabadiliko makubwa ya Baraza la Mawaziri Nchini, aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kulinda Taifa, Ndugu Edward Moringe Sokoine aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu akichukua nafasi ya Kawawa, Shekilango akabakishwa katika nafasi yake lakini akiwa na bosi mpya.

MATATIZO YA UGANDA

Mara baada ya Mapambano ya Vita vya Kagera, Mwanzoni mwa mwaka 1979 Vikosi vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania vilifanikiwa kumng'oa Madarakani Dikteta Amin wa Uganda na kumpachika Ndugu Yusufu Lule kama Rais wa Muda wa Taifa hilo Jirani. Lule hakudumu sana madarakani kwa kuwa mwezi Juni, 1979 naye aling'olewa madarakani kwa kutofautiana na Baraza la Ushauri la Taifa la Nchi hiyo juu ya uteuzi wa nafasi za Mawaziri, na nafasi yake kuchukuliwa na Ngudu Godfrey Binaisa.

Miezi kadhaa baada ya kuchukua madaraka kwa Binaisa katika Serikali ya Uganda bado mambo ya kuendesha nchi hiyo hayakuonekana kwenda vizuri, Changamoto za kujenga upya nchi hiyo iliyoharibiwa na vita zilikuwa kubwa, huku Jeshi jipya la nchi hiyo likiwa na kashfa ya kufanya ukatili kwa wananchi na pia kushiriki kwenye uhalifu na uporaji. Ili kuimarisha mambo ya Kiutawala ya Nchi hiyo ilimbidi Rais Nyerere ambaye bado vikosi vya Jeshi lake vilikuwa havijaondoka Uganda, ampeleke Waziri Hussein Ramadhani Shekilango kwenda kusaidia mambo ya Kiutawala ya Nchi hiyo.

Mwezi Mei, 1980 ilizuka sintofahamu kubwa katika Utawala wa Uganda, Rais Godfrey Binaisa alimuondoa Jeshini Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Nchi hiyo (zamani akiitwa Chief of Staff) Ndugu David Oyite Ojok na kumteua kuwa Balozi wa Uganda Nchini Algeria, sababu kubwa ikitajwa kuwa ni nidhamu mbaya ya Jeshi la nchi hiyo hasa kwenye masuala ya Ukatili kwa wananchi na Uporaji.

Uamuzi huo wa Rais Binaisa haukumfurahisha Kiongozi huyo Namba 2 wa Jeshi la Nchi hiyo, hivyo alikataa Uteuzi mpya, na wanajeshi waliokuwa Watiifu kwake wakatangaza kumuondoa Madarakani Rais Binaisa aliyekuwa akilindwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania katika Hekalu la Rais la Entebbe. Misururu mirefu ya Magari ikaonekana katika Jiji la Kamapala, ambapo Wanajeshi watiifu kwa David Ojok walikuwa wakiyapekuwa magari yote yaliyokuwa yakitoka na kuingia ndani ya jiji hilo ili kuhakikisha hakuna silaha, huku pia wakikiteka Kituo cha Redio cha Taifa cha Nchi hiyo.

Wanajeshi wafuasi wa Ojok waliweka vizuizi katika barabara zote za Jiji la Kampala na kuamua kuyalinda majengo yote nyeti ya Serikali likiwemo Jengo la Nile Mansion Hotel ambalo ndilo lililokuwa na Ofisi nyingi za Wizara nyeti za Serikali ya Nchi hiyo.

Kung'olewa kwa Binaisa kulifanywa na Tume maalum ya Watu sita, ambayo ilikuwa ni sehemu ya Baraza la Ushauri la Taifa lililomng'oa Rais Lule, huku matendo ya Tume hiyo pamoja na Ojok kwenye wiki hiyo yakihusishwa zaidi na Rais Milton Obote aliyekuwa ughaibuni, ambaye aling'olewa Madarakani na Amin mwaka 1971. Obote alikanusha kuhusika na matendo hayo ya Ojok yaliyokuwa yakiteteresha hali ya ustawi wa nchi hiyo japo haikubadili ukweli kuwa marafiki hao lao lilikuwa moja.

katika hali ya matatizo yote hayo, Waziri Hussein Ramadhani Shekilango pamoja na Balozi Kilumanga waliamua kupanda Ndege kwenda kumpa habari za namna hali halisi ya mambo ilivyo nchini humo Rais Nyerere ambaye alikuwa kwenye Ziara ya Kiserikali Mkoani Arusha. Safari hiyo ndiyo ikawa mwisho wa maisha yao.

Ilikuwa siku ya huzuni mno kwa kumpoteza Waziri huyo damu changa, Tarehe 11 Mei, 1980, ndege ya Kijeshi iliyowachukua Shekilango, Balozi Kilumanga pamoja na Wanajeshi wanne wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ilianguka katika vilima vya Jiji la Arusha na Abiria wote kupoteza Maisha, wakiacha huzuni na majonzi mazito kwa Watanzania.

Msafara wa Rais ukakatisha ziara na shughuli ya Mapokezi ya Miili ya Mashujaa wetu hao ndiyo ikawa Ratiba rasmi, huku Rais Nyerere akionyesha kwa dhati namna alivyohuzunishwa kwa kumpoteza Waziri huyo Mchapa Kazi kwa Taifa. Majonzi zaidi yakiwa kwa Wanakorogwe waliopoteza Kijana wao Msomi wa Makerere aliyejitolea kuwatumikia kwa dhati.

Shekilango alizikwa Kijijini kwao Jitengeni, Korogwe, Mkoani Tanga, huku akisindikizwa na umati mkubwa wa watu, mpaka leo akibaki Mbunge kipenzi cha watu wa Korogwe na akisifika Serikalini kwa hatua yake ya kurudisha Madaraka Mikoani. Kwa kumuenzi kuna Shule yenye jina lake Jimboni Korogwe.

Mamlaka za Uongozi wa Jiji la Dar es salaam kwa kutambua mchango wa Shekilango kwa Taifa, ikaamua kuipa Barabara mpya iliyokuwa inajengwa wakati huo jina la Shekilango ili kumuenzi shujaa huyu.

Mola amlaze Pema Shujaa Hussein Ramadhani Shekilango

Pichani ni Ndugu Hussein Ramadhani Shekilango, Picha ni kwa Hisani ya Familia ya Shekilango, Ukurasa wa Watanzania Mashuhuri unatoa shukrani za dhati kwa Bi Ikupa Shekilango kwa Msaa wake kwa Ukurasa.


"Kalayi Boeing" FROM THE FULL DREAM TEAM THE BEST BAND THAT EVER LIVED IN CONGO-DRC HISTORY:- ALAIN PRENSE MAKABA + DOMINGUEZ + WERASON + JEAN BENDEL MPIANA MUKULU + DIDIER MATSELA + BLAIZE BULA + ROBERTO ATALAKU LIVE!!

LE BIG SHOW LIVE AT ACCRA/GHANA'S MARKET NA PICHA 10 ZA TASWIRA HASWA YA VITENGE VYA UKWELI KWENYE SOKO LA WAPOPO CHECK HAPA LIVE JANA MCHANA!!

$
0
0

Last Sunday live at the Accra Market Le Big Show na Machingazzzz!!



















HATIMAYE SUPER STAR LULU ACHOSHWA NA KIVULI CHA STEVE KANUMBA AAMUA KUUANIKA UKWELI WOTE NJE NJE SOMA HAPA LIVE!!

$
0
0


MWANGA umeanza kuonekana juu ya kesi inayomkabili staa wa filamu za Bongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ ya kumuua bila kukusudia staa mwenzake wa muvi, Steven Charles Meshack Kusekwa Kanumba ambapo safari hii aliamua kukiri vipengele kibao, Risasi Mchanganyiko lina habari yote.
Elizabeth Michael 'Lulu' aliyeambatana na Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’ wakiwa eneo la mahakama.
Akikiri mbele ya Mahakama Kuu ya Tanzania juzi (Jumatatu) wakati kesi hiyo ilipoanza kusikilizwa, nyota huyo aliweka wazi mambo ambayo hapo awali hakuwahi kuyakubali kortini jambo lililovuta hisia za wasikilizaji waliokuwa wamefurika ndani ya chombo hicho cha kutoa haki kujua kinachoendelea.
Mwendesha mashitaka wa upande wa serikali, Monica Mbogo alivitaja vipengele kadhaa ambavyo Lulu alitakiwa kuvikana au kuvikubali.
Katika kesi hiyo iliyoendeshwa kwa ustadi mkubwa wa wanasheria kuoneshana ujuzi wa kusoma na ‘kubugia’ vipengele vigumu vya sheria, Lulu alipata wakati mgumu wa mambo kiasi cha kumwita wakili wake, Peter Kibatala mara kwa mara.
MADAI YA KUMUUA KANUMBA BILA KUKUSUDIA
Lulu alikiri kwamba, mashitaka yake mahakamani hapo yalikuwa ya kumuua bila kukusudia, marehemu Steven Kanumba Aprili 7, mwaka 2012.

KUWEPO ENEO LA TUKIO NA KUTOKEA KWA UGOMVI
Katika maelezo yake, Lulu aliweka bayana kuwa siku ya tukio alifika nyumbani kwa marehemu maeneo ya Sinza ya Vatican jijini Dar saa 6 usiku na kuingia moja kwa moja chumbani.
Alizidi ‘kuchezesha taya’ kuwa, kulitokea ugomvi kati yake na marehemu licha ya kutotaja chanzo cha ugomvi huo.

Aliongeza kwamba, Kanumba alimvuta mkono na kumrudisha ndani wakati alipokuwa akijaribu kukimbia na kuufunga mlango, mwishowe alifanikiwa kutoka na kukimbia kusikojulikana.
KUKAMATWA KWAKE BAMAGA
Lulu aliweka wazi kuwa, siku ya tukio, saa 11alfajiri alikamatwa maeneo ya Bamaga- Mwenge jijini Dar es Salaam alipokuwa akijaribu kutorokea kusikojulikana.

KUHUSU UHUSIANO
Bila kupepesa macho wala kuchezesha kope, Lulu alikubali kuwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na marehemu Kanumba kwa muda ambao hakuutaja hali ambayo baadhi ya watu walionesha kuwa ‘sapraizidi’.

AMWAGA MACHOZI KORTINI
Awali, Lulu alipofika mahakamani hapo akiwa ameongozana na mama yake mzazi, Lucresia Karugila na staa wa muvi za Kibongo, Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’ alionekana kuwa na amani.

Msanii huyo alimudu kusoma Gazeti la Ijumaa Wikienda ambalo liliingia mtaani siku hiyo. Lakini baada ya kuanza kwa kesi, ilifika mahali alidondosha machozi hali iliyomlazimu kujifuta uso kwa kitambaa.
Baadhi ya watu walinong’ona kuwa, mrembo huyo alikuwa analizwa na kumbukumbu za tukio la kifo cha Kanumba na kwa sababu ya kuogopa kesi.

MAMA KANUMBA ASUSA
Habari nyingine zilidai kuwa, mama wa marehemu Kanumba, Flora Mtegoa hakutokea mahakamani hapo licha ya umoja na udugu alionao kwa sasa na familia ya  Lulu.

Ilidaiwa kuwa sababu kubwa ya kushindwa kufika kortini ni kukosa uamuzi wa upande gani angekaa kati ya mshtakiwa (Lulu) na mshitaki (Jamhuri) kwa vile kote kuna muhusu kwa sasa.
“Unajua mama Kanumba alipogundua kwamba anayetakiwa kujibu madai ni Lulu ambaye baada ya kutoka mahabusu alimtangaza ni mwanaye na anayelalamika ni serikali, alishindwa kujua akija leo (juzi) angekaa upande gani? Akaamua kutokufika kabisa,” kilisema chanzo chetu.
Risasi Mchanganyiko lilimsaka kwa simu mama huyo lakini bila mafanikio kufuatia simu yake ya mkononi kuita muda mrefu bila kupokelewa.
TUJIKUMBUSHE KIDOGO
Lulu alikamatwa kwa kosa la kumuua bila kukusudia aliyekuwa galacha wa filamu za Kibongo, marehemu Steven Kanumba mnamo Aprili 7, 2012 nyumbani kwake, Sinza Vatican jijini Dar.

Baada ya kukamatwa na kuswekwa mahabusu ya Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar, Lulu alipandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo hakutakiwa kujibu ndiyo au hapana.
Hata hivyo, ilielezwa kuwa mahakama hiyo haikuwa na uwezo wa kusikiliza kesi ya madai hayo.
Aliachiwa kwa dhamana Januari 29, 2013 na kuambiwa kwamba kesi yake itakaporudi, itakuwa chini ya mahakama kuu. Juzi ilianza kusikilizwa kwa mara ya kwanza

GET STRESS FREE LIVE FROM SINTAH JLO WA BONGO & UGLY UNFILTERED COMMENTS!!

$
0
0

CARA DELEVINGNE AND MICHELLE RODRIGUEZ CONFIRM THEY ARE DATING

daah
hii ndio dunia kila siku kukicha kuna vituko
kwa akili zangu huyu alievaa miwani ndio kidume huyu
tutembee tuone mengi ya dunia


Sijui wanasikia raha gani jamani ama nikujitoa fahamu


  1. Nawewe mpaka leo unashangaa mambo ya ushoga?? mbona ishakuwa kitu cha kawaida tu! Acha ulimbukeni
    Reply
    Replies
    1. Its normal in the whole universe. its a freedom of choice. na wewe fala huna habari za maana what does other ppls sex life has to do with you.
  2. Hatari kweli na vizazi vijavyo ata sijui watapokewa vipi Siku zao za kifo!
    Reply
  3. serikali ya Lesbihonest yaongezeka mwee hilo michelle miaka 35 ndio litakua limemshawishi huyo Cara hata maisha bado hayajayajua miaka 21 ushaanzwa kunyonywa kipapuchi na huyo ngurumbembe
    Reply
  4. Kwanini unatoa hizi habari na unakesha kuzitafuta kila siku?
    Inaonekana unataka kuhalalisha kitu. Acha ujinga wewe.
    Hizi habari ulipaswa usizisake kila siku, kwani watakaofanya huo mchezo wanaweza sema mbona hata fulani maarufu anafanya.
    KakaJ
    Reply
  5. mwee Baby ya Zeze nimetoka kuchungulia kwa Jestina hivi yule ndie weyee? kwenye mambo ya Valentine na Ommy nikasema Shuuut the froont door shouger ndio bomba kivile eeeh hiyo boobs manshaalahh wangu nimeonaje wivu hilo clevage naweza hata swipe kadi yangu ya tembo uwiii shouger nimefurahije kukufahamu sasa wageni washaondoka? miss Jabir? na wengineo khaaa wamajuu mnatokelezea hataree yule mwenye black kama super women kulikoni? mbona ataka kumbaka dimpoz stegini kwii kwii napenda kutuma salamu kwa mpenzi wangu mbuta nanga ujumbe krismas ilishapita tupo mwezi shabani wa valentine kwii kwii all in all nice to see you
    Reply
    Replies
    1. Kwa jestina wanaonekana bomba zaidi, lakini kule kwingine hawajatendewa haki, wanaonekana wako ovyo. Mm yule dada mwenye blauzi nyekundu minido yote nje, ndonini kile? Au sababu yakutengeneza kwahiyo lazima yaanikwe nje pesa iende kihalali. Baby ya..nido lake linaonekana ni original..afu sio mfupi kiivo kama wanavosema, but gym inamuhusu kidoogo.
  6. wewe sintah unacheza wewe........
    Reply
  7. nahc ni wakat wa kla mtu kufanya maamuz ayatakayo.....mi bnadsi naona kawaida sana tena n aim a lesbian too!!n raha ipo !!naomba ngedere yoyote asini attack kwa maneno nmesema wat I feel
    Reply
    Replies
    1. mimi ni bisexual, what i think sintah nae ni kundi moja mbona kila siku anaandika hizi habari? anapenda kuona watu tutareact vipii...sinta tumekustukia unasagana pia....kusagana raha jmn.
    2. I TOTALLY respect your love life, no one is to judge anyone, go for your happiness ladies. i got nothing negative with being attracted to the same sex.
  8. ila we sintah kila siku unauuliza hujui wanasikia raha gani siuje ujaribu na wewe utaijua tu hiyo raha.....mxwiiiiiiiii
    Reply
  9. KAZIKWELI DUNIA IMEGEUKA SIKUIZ.MAMBO YA BABY YA ZEZE HAYO.ANAPENDA SANA HIYO KITU YAKUKOBOANA.AU SIO BABY YAKE M.ALAFU HUFANANI HATA NAMAMBO YAKO.DU
    Reply
  10. hahahahahhhah wanasikia raha gan muulize mtoto wa mkubwa wa nchi anasikia raha gani anavyotoka na vitoto vidogo vya kiume........in lenshayo(insta)voices mkuu wa wakuu huyo ndo habari ya mji kijana gani wa mji huu hajapitiwa naye???shikamoooooooooo pesa
    Reply
    Replies
    1. Eeehee yule nae anageuza wenzie,Ni huyu huyu Ongea na mshua ama mwingine??
  11. ahahahahhaha ila sintah bana asa unaumiza kichwa chako kuwaza siumuulize tu shoga ako penseli huwa anasikia raha gani akiwasaga wenzie
    Reply
    Replies
    1. Heee kumbe hata penseli naye yumo, uwii
    2. ndo maana mama mkwe na mawidi walikuwa wanampenda, kwikwikwi
  12. tobaaaa penny masagaji muogopeni MUNGU JAMANI maisingizie binti wa watu jamani
    Reply
  13. We sinta umewaona hao tu mbona hawa wa bongo hauwasemi na wamejaa kibao na wengine ni maragiki zako
    Reply
  14. ehheeheheheh chezeaaaaa weye bibo na huyo len ndo king kong yaaaaaan ni balaaaa mbaba huyo kachakaza saaana ni hatar unaambiwa weka mbali na watoto.......sinta weka hizi mada kila siku manake ukiweka watu wanaumbuliwa na wanaacha
    Reply
  15. na kuna kibint kiko nje ya nchi siku hizi kile nacho ni kisagaji kikubwa tu hapa bongo
    Reply
    Replies
    1. Kipii hicho jaman maana vibinti huko nje vipo vingi,,hebu nin'gate kisikio kangu
    2. kipo kirefu cheusi nilishiriki nacho mashindano fulani hivi yale yakumpata mlimbwende na kinablog uchwara na chenyewe.....kama utakuwa mtoto wamjini nadhan utakuwa ushakielewa
  16. kwajinsi nilivyofwatilia blog yako ..inaonyesha jinsi gani unafwatilia sana maswala ya usagaji na ushoga.sasa swali langu ni je ..unapenda ushoga au ni nini haswa kinachokufanya huoni mambo mengine ...basi tu postie na wasagaji wa bongo au unawaogopaaa...
    Reply
  17. usiombe ukaujaribu huo mchezo,maana sometimes ukiumizwa unajaribu kwengine.wadada wanajua kuchezea kiharage na wanajua kuushuhulikia mwili mpaka unajisikia,once your in kutoka shuhuli.maana wakaka hawawafikii wadada kwa foreplay
    Reply
  18. Out of Topic hivi Lina Sanga na hvyo vinguo vifupi anakua kama Bizman ule wimbo ametoroka angekua anavaa nguo ndefu angependeza afu masongange huoni haya kutwa kupiga mapicha kazi ufanyi unatuwekea migold inshort tunakuzalau piga picha uko njian unaenda kazini Mesage ya Mwamvita Makamba ukuiona haya. Na matako yako umri unakwenda kalia hayohayo litakuchwea.
    Reply
  19. Msyuuuuu mnaosema penny msagaji wote nyie ndo mademu zake anawasaga.otherwise ucseme kitu usicho na uhakika nao.nyokost nyie.hao hapo wenyewe wameconfirm umbea wakizaman ckuiz hamna umbea wakisasa na uhakika juu.ee mumuache sintah ashangae kwasababu c kitu chakawaida kwa cc watz.so get ur basket mouth shut biatchhhss
    Reply
  20. sinta matege huyoooo anampenda lemutuz na lemutuz ampendi..kibibi kidude sintah,
    Reply
  21. We andunjee achakubana bana my comment!kabane. Mav ya uharo bac kama unajua kubana!mmscccheeeeeeeew cockmkubwa!#by  in boots
    Reply
  22. OUT OF TOPIC: Jamani kuna wakaka wa vodacomm wamenikera sana, jamani hivi nyie wakaka na wadada wa vodacom mbona hamjatulia wajameni? mnatia kichefuchefu
    Reply
  23. We sinta shoga yako anasutwa na mtu wa jf kuwa jana ujuzi na kuendeaha blog je wewe shoga mahojiano tbc now.

ONA MAMBO YA KISASA SULUHU YA MSONGAMANO WA MAGARI BONGO HII HAPA LIVE!!!

$
0
0


Mojawapo ya mabasi yanayotembea nchi kavu na majini. 
  • Kwa Afrika, Tanzania itakuwa nchi ya kwanza kuwa na aina hii ya mradi wa mabasi ya majini.;
  • Mabasi hayo yana uwezo wa kutembea nchi kavu na majini, hii ina maana kuwa yatasaidia kwa mfano kusafiri kutoka Posta kwenda maeneo mengine yoyote ya jiji ambayo yanafikiwa na bahari.
  • Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) inasema mradi huo unaweza kusaidia kuleta mapinduzi makubwa katika sekta ya usafirishaji nchini.

Serikali, mashirika binafsi na wadau wa usafiri ndani na nje ya nchi wamekuwa wakifanya jitihada mbalimbali kukabiliana na msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam.
Msongamano huo ambao unachangiwa kwa kiasi kikubwa na uduni wa miundombinu ikiwemo barabara, umekuwa ni kero kwa wananchi na Serikali kwa jumla.
Serikali imewekeza katika Mradi wa Mabasi Yaendayo Kasi (BRT) na usafiri wa treni ndani ya Jiji la Dar es Salaam kama njia mojawapo ya kumaliza tatizo la msongamano wa magari na foleni.
Msingi wa tatizo
Chanzo kikubwa cha foleni jijini Dar es Salaam si wingi wa abiria bali ni wingi wa magari binafsi na njia finyu zisizokidhi mahitaji ya watu walioko katika jiji hilo.
Njia muhimu ya kupunguza foleni na msongamano wa magari ni kupunguza wingi wa magari barabarani na kuweza kuzipanua barabara ili kuwe na uwezekano wa kupita kwa urahisi.
Kutokana na foleni na uduni wa huduma za usafiri wa umma watu wa kundi la kati, wamekuwa wakikimbilia kununua magari binafsi kwa ajili ya kwenda nayo kwenye shughuli zao kwa urahisi.
Aidha, katika kuendeleza harakati za kupambana na tatizo la usafiri, Kampuni ya Transevents Marketing ya Tanzania kwa kushirikana na Kampuni ya Dutch Amphibious Transport Vehicles (DATV) ya Uholanzi inaendelea na mchakato wa kuleta usafiri wa mabasi ya abiria yenye uwezo wa kusafiri nchi kavu na majini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Transevents, Peter Nzunda anasema teknolojia hiyo ya mabasi ya nchi kavu na majini (amphibious) ina lengo la kupunguza tatizo la foleni kwenye barabara za Dar es Salaam hususan katikati ya jiji kwa kuwa mabasi hayo huweza kupita nchi kavu na majini.
Hii ina maana kuwa hata katika maeneo yenye barabara zisizo nzuri au zenye tope, magari hayo huweza kupita hivyo kutosababisha foleni kama ambavyo hutokea sasa katika baadhi ya maeneo hasa mvua zinaponyesha na kuharibu barabara.
Anasema mbali na lengo hilo, mabasi hayo yatatumika kama vivutio vya utalii kwa kufanya utalii wa baharini ambao kwa Tanzania haujashika kasi, licha ya sehemu kubwa ya nchi kuzungukwa na maji.
“Mpango huo wa mabasi ya nchi kavu na majini unalenga kutoa ushawishi kwa watu wa kundi la kati ambao wanatumia magari binafsi waegeshe magari yao na kutumia usafiri huu ambao utakuwa wa hadhi yao na unaokidhi haja kwa ubora wake,” anasema Nzunda na kuongeza:
“Lengo ni kujenga maegesho ya magari maeneo mbalimbali kandokando ya bahari, watu wataegesha magari yao na kupanda mabasi yatakayopita majini kwenda Posta na baadaye kurejea kwa utaratibu huohuo na kuyachukua magari yao tena kwenye maegesho walipoacha magari yao”.
Shughuli za utalii
Nzunda anasema mbali na teknolojia hiyo kutumika kama usafiri wa umma Jiji la Dar es Salaam, mabasi hayo yatatumika kupeleka watalii kwenye hifadhi za taifa zinazozungukwa na maji kama vile Bagamoyo, Mbudia, Mafia na visiwa vingine ili kujionea mambo mengi zaidi ya kiutalii.
“Tunataka pia watu wanaokwenda kwenye fukwe wasiishie kulala na kucheza mchangani, bali wawe wanapanda mabasi haya na kutembelea sehemu  mbalimbali zenye vivutio baharini; hiyo itakuwa ni fursa ya watu kuzunguka baharini wakiwa ndani ya mabasi hayo yatakayokuwa katika miundo tofauti,” alisema Nzunda.
Mahitaji ya mradi
Nje ya Kampuni ya Dutch Amphibious Transport Vehicles (DATV) kutaka kuingiza teknolojia hiyo nchini, Serikali ya Uholanzi pia ipo tayari kuchangia  kwa asilimia 50 ya gharama za mradi wote ambao gharama zake zitajulikana mara baada ya kufanyika tathmini wa mradi.
Aidha, Serikali ya Tanzania, wawekezaji katika sekta ya usafirishaji wa abiria nchi kavu na majini na wadau wengine watatakiwa kuchangia asilimia 50 zilizobaki katika kufanikisha kuanza kwa mradi huo ambao mchakato wa kupata kibali umeshaanza.
Meneja Mwendeshaji wa Transevents Marketing, Mahamud Omari anaiomba Serikali kusaidia uharakishaji wa utoaji wa leseni ya uingizwaji wa teknolojia hiyo mpya ya mabasi.
“Mchakato wa kupata kibali umeshaanza na matarajio yetu ni kufanikisha hatua hiyo baada ya miezi sita kuanzia sasa,” anasema Omari.
Ofisa Uhusiano wa kampuni hiyo, Edna Rebecca anasema mradi huo wa ‘Mabasi ya Majini na Nchi Kavu’ utatengeneza ajira nyingi kwa vijana wengi na kuongeza fursa za kibiashara kwenye hoteli.
Pia mabasi hayo yataongeza pato la taifa kupitia utalii na maendeleo ya teknolojia hiyo kwa jumla, kwa ajili ya kizazi hiki na kijacho, ukizingatia takwimu za Shirika la Makazi Duniani, zinaonyesha miaka 50 ijayo, Jiji la Dar es Salaam litakuwa na wakazi wapatao milioni 18.
Mabasi hayo yatatumika kwa shughuli za harusi hasa kwa wanandoa ambao watapenda kufunga ndoa ndani ya maji.Pia yatatumika kwa safari za kitalii za wafanyakazi wa kampuni mbalimbali, wanafunzi, wanakwaya, wanavikundi na klabu za mipira.
“Usafiri huu utakuwa ni wa bei ya kati ambayo itaendana na huduma bora na utalenga kuziba changamoto zote ambazo zinapatikana sasa kwenye usafiri mwingine wa umma,” anasema Rebecca na kuongeza:
“Kuna watu wanapanda magari kwa kulipia Sh1,000 badala ya Sh400 kutoka Posta kwenda Mwenge ili kukwepa adha ya kubanana kwenye daladala zinazokaa muda mrefu kwenye foleni, kwahiyo unaweza kuona ni kwa namna gani watu wanahitaji huduma bora za usafiri wa umma.”
Katika mazingira ya kawaida familia nyingi jijini Dar es Salaam zinatumia magari matatu kwa wakati mmoja yaani baba, mama na mtoto, jambo linaloongeza masongamano barabarani.
Rebecca anasema usafiri huo utawafanya watu hao kuyaacha magari yao nyumbani au kwenye maegesho ya magari yatakayojengwa na hivyo kupunguza kabisa idadi ya magari barabarani.
Mabasi hayo pia yatapunguza gharama za maisha zinazotokana na matumizi ya mafuta kwani kama mtu anaweza kutumia lita 20- 50 kwa siku.
Serikali inasemaje
Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), David Mziray anasema teknolojia hiyo ya usafiri wa mabasi ya nchi kavu na majini imekuwa na msaada mkubwa kwa nchi nyingi Ulaya, kuja kwake Tanzania itakuwa ni habari njema hususan wakati huu ambapo jiji linakua kwa kasi.
 “Kazi yetu ni kupokea maombi na kuangalia kama yanakwenda sambamba na sheria na kanuni zetu na kama unavyojua hii ni aina mpya ya usafiri kwa hiyo lazima kutakuwa na mambo ya msingi ya kuyajadili na kuyapatia ufumbuzi kabla ya kuanza,” Anasema Mziray
Baadhi ya wananchi wanasema mradi huo unaweza kusaidia sana kuondoa kero ya usafiri Dar es Salaam.

LE MUTUZ LIVE NA MBEBEZ WA UKWHEEEZZZZ AT LAGOS SUPER ERNIE WALLAHI NIGERIA NAKO NI TAMBALALAEZZZZ U KNOW KAMA VIPI BONGO MJIPANGEZZZ!!

THE MAJANGAZ & LE MBURULAZZZ:- HAWA WASANII WOTE MGANGA WAO AMEKUFA ONA HUYU SUPER MBURULAZZ NOTHING BUT MBURULAZZ LIVE!!


NA HUU NDIO MUONEKANO LIVE WA MOVENPICK SERENA HOTEL KAMA YA BONGO AT DOWNTOWN ACCRA/GHANA LIVE!!

SUPER BLOGGER WA MBEYA YETU MWAISANGO NA MBEBEZ WAKE WA UKWHEEEZZZ WIFE U KNOW TENA WAMETOKELEZEA LIVE!!

KWELI MAJANGAZAA...KWA MAMEN MSIO JUA KUTONGOZA KUMBE UJANJA WA MABEBEZI NI MDOGO SANA CHEKI HAPA

$
0
0
https://www.facebook.com/brotherlucas
Jamaa: Hello mrembo, samahani, una mpenzi? Binti: Hapana. Sina mpenzi. Jamaa: Kitabu cha Mwanzo 2: 18 "Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye." Binti: Lakini mimi sikupendi jamani. Jamaa: Waraka wa kwanza wa Yohana 4:8 "Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo." Binti: Mh! Mi ntajuaje
kwamba na wewe unamaanisha hayo maneno? Jamaa: Injili ya Mathayo 12:34b "Maana, kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake." Binti: Jamani leo kazi. Mi ntajuaje kwamba we ni mkweli na mwaminifu? Jamaa: Injili ya Marko 13:31 "Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe." Binti: Wewe! Na kwanini umekuja kwangu? Wasichana mbona wako wengi tu! Jamaa: Mithali 31:29 "Binti za watu wengi wamefanya mema, Lakini wewe umewapita wote." Binti: We una mambo wewe! Sasa mimi kwangu umependa kitu gani? Jamaa: Wimbo Ulio Bora 4:7 "Mpenzi wangu, u mzuri pia pia, Wala ndani yako hamna ila." Binti: Mh! Huo uongo, mbona mimi hata sio mzuri kihivyo. Unaongeza chumvi tu! Jamaa: Mithali 31:30 "Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili; Bali mwanamke amchaye Bwana, ndiye atakayesifiwa." Binti: Nikisema nimekukubalia itakuaje? Jamaa: Mwanzo 2:24 " Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja." Binti: Jamani we mkaka. Inakuaje unajua maandiko kiasi hicho? Jamaa: Yoshua 1:8 "Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana." Binti: Wowwww! Naona unampenda sana Mungu. Jamaa: Zaburi 34:8 "Onjeni mwone ya kuwa Bwana yu mwema; Heri mtu yule anayemtumaini." Binti: Mh! Haya bwana. Basi nipe muda nifikirie ombi lako. Jamaa: Wafilipi 4:8 "Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini hayo." Binti: Mh! Jamani wewe, haya, nimekubali. Mpaka hapo nakupenda tayari!! Jamaa: Ufunuo wa Yohana 22:21b "Amina"

BACK FROM LAGOS AT ACCRA JANA CHAIRMAN JUMA PINTO WITH SUPER RICH BILIONEA KENPONG LIVE AT HIS COMPANY HQ LIVE!!

BAADA YA KUWA NA BIFU LA MUDA MREFU NA DIAMOND SASA BABY MADAHA ASALIMU AMRI NA KUAMUA KUACHA MUZIKI PAMOJA NA FILAMU, SOMA HAPA KUJUA ZAIDI

$
0
0
IKIWA imepita miezi kadhaa tangu anaswe katika mtego  wa kujiuza,  staa wa Bongo, Baby Madaha ametangaza kuachana na sanaa ya muziki na filamu kwa maelezo kuwa amechoshwa na  maisha ya presha. Akiongea  na 
mwandishi wetu  juzikati jijini Dar es Salaam, Madaha alisema ishu ile imemsababishia matatizo makubwa ya kifamilia na hata kibiashara, hivyo kujutia mchezo mzima ulivyokuwa.

Alisema filamu anayoisambaza kwa sasa na kibao chake cha mwisho kukitoa cha Mr. Dj ndizo zitakazofunga pazia la mambo ya sanaa kwa upande wake.

 “Nimeamua kuachana na sanaa kabisa, siwezi kuishi maisha ya presha yasiyo na uhuru. Nitarudi kwenye fani yangu niliyosomea (hakutaka kutaja), maana naishi maisha ambayo hayana amani kabisa,” alisema.

MBEBEZI SUPER STAR WA BONGO IRENE UWOYA HALI YAKE KIAFYA SIO NZURI...!ALAZWA AGHA KHAN....!!!

$
0
0
Taarifa zilizosemwa na rafiki wa karibu wa msanii Irene Uwoya ni  kuwa yupo katika hali mbaya zaidi na kufikia hatua ya kulazwa katika hospitali ya Agha Khan akisumbuliwa na Malaria.
Get well soon Irene....

KWA WALE MLIOKUA HAMMJUI MKE WA MWIGIZAJI AKI KUTOKA NIGERIA BASI, TAZAMA PICHA HIZI. NI YULE MWIGIZAJI ANDUNJE

$
0
0
 
You all know actor Chinedu Ikedieze's wife is a designer, right? Nneoma Ikedieze is the CEO of Nikiz Collection and unveiled her 2014 collection at Oriental Hall, Lagos on Sunday February 16th and her dear husband was there to support her. See more photos from the event after the cut...





 SHUKA CHINI KUTOA MAONI YAKO

HAYA NDIO MAKAO YA RAIS WA GHANA NA OFISI ZAKE YAANI IKULU ONA HAPA LIVE!!

TAARIFA YA IKULU YA UFAFANUZI KUHUSU BARAZA LA MAASKOFU WA KIPENTEKOSTE TANZANIA (PENTECOSTAL COUNCIL OF TANZANIA) KUTOKUWA NA UWALIKILISHI KATIKA BUNGE MAALUM LA KATIBA

BACK AT THE BILIONEA KENPONG MANSION IN ACCRA AFTER FLYING BACK FROM LAGOS WITH MY PEOPLE:- CHAIRMAN JUMA PINTO + JUMA MABAKILA + TEDY KARUA LIVE!!

$
0
0

The Mansion
Mr. Kenpong





The Maybach

The Maserati

The Jaguar







The Crysler


The Jeep

Mr. Kenpong + Chairman Juma Pinto






Juma Pinto + Juma Mabakila
























MY SUPER FRIEND JACKY MKAREEZ MBEBEZ TABATA IYO U KNOW KAMA VIPI MISS U SANA NA LOVE YAH MINGI BBY!!

MSAMALIA MWEMA KUTOKA UINGEREZA ATUMA MISAADA KWA MZAZI WA MAPACHA WA NNE MKOANI MBEYA

$
0
0

 




Misaada ya hali na mali imeanza kumiminika kwa ajili ya Aida Nakawala (25) mkaazi wa kijiji cha Chiwanda, Wilaya ya Momba, Mkoa wa Mbeya, ambaye alijifungua watoto wanne mapacha kwa mkupuo (Quadruplets) usiku wa kuamkia Mwaka mpya wa 2014 katika Hospitali ya Wazazi ya META jijini Mbeya. 
 Msamaria mwema wa Uingereza, Bi Gladness Sariah, ametuma maboksi mawili yenye nguo na vitu kadhaa vya watoto, ambavyo vimewasili salama katika ofisi za Michuzi Media Group (MMG) inayoendesha Globu ya Jamii jijini Dar es salaam baada ya kusafirishwa bure na Wazee wa Kazi, Serengeti Freight Forwarders ya huko Uingereza. 
 Hivi sasa MMG ikishirikiana na waratibu wa misaada kwa mama huyo, Mbeya Yetu Blog, wanaandaa utaratibu wa kumfikishia Mama Aida mizigo yake haraka iwezekanavyo. 
 Kwa niaba ya mzazi wa mapacha hao, Michuzi Blog na Mbeya Blog zinatoa shukrani za dhati kwa msamaria mwema Gladness Sariah kwa wema na upendo aliouelekeza kwa mzazi huyo. Huo ni mfano wa kuigwa, na tunatarajia misaada zaidi itatolewa na wasamaria wema ambao tunajua mko wengi kila kona ya dunia. 
 Kama umeguswa na hili na unataka kutoa msaada tafadhali wasiliana na issamichuzi@gmail.com ama j.mwaisango@tonemg.com nasi tutafikisha ubani wako. 
 Muhidin Issa Michuzi 


Aida Nakawala 25 mkazi wa kijiji cha Chiwanda Wilaya ya Momba Mkoa wa Mbeya, hivi karibuni alijifungua watoto wanne  mapacha kwa mkupuo(Quadliplets) katika usiku wa kuamkia Mwaka mpya anaendelea vizuri.

Mwanamke huyo ambaye kwa hivi sasa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Wazazi ya Meta akiwa na watoto wake wote wanne alijifungua majira ya saa 10 alfajiri usiku wa kuamkia Januari Mosi Mwaka huu katika Hospitali ya Wilaya ya Mbozi na watoto wakiwa na uzito wa kawaida tofauti na matarajio ya Wengi.




Viewing all 32622 articles
Browse latest View live




Latest Images