Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all 32622 articles
Browse latest View live

SHILOLE ALIVYONOGESHA UBELGIJI‏

$
0
0
Shishi Baby akifanya mambo yake huku mashabiki wakiwa na midadi.

Msanii Shilole akiburudika vyema na dada yetu aliyekuja toka Norway kujumuika nasi katika kupata burudani ya Shishi Beibii.
 Wachaa weeee.PICHA KIBAO>>>

BOSS NGASA : HICHI NDICHO ALICHOKISEMA BAADA YA TAARIFA KUSAMBAA KUWA AMEKUFA BAADA YA KUPATA AJALI

$
0
0

Mmiliki wa Official Website (Boss Ngasa TZ) kupitia account yake ya Instagram ameandika kuhusiana na kuzagaa kwa Picha zinazo muonyesha yeye na marehemu wengine (Matei. Joshua na Chiddy Nyau) ....... Boss Ngasa amekanusha Taarifa zinazodai amefariki Dunia Baada ya Ajali mbaya walioipata Juzi na Kupoteza uhai wa Rafiki zake wawili Matei na Joshua.

THE MAGAZETI YA BONGO LEO WEDNESDAY /JUMATANO 3/12/2014 LIVE!!

VIDEO DIAMOND AMPA KIJEMBE ALLY KIBA...."HATA ALLY SIMUONI".NI SHIDAA

ZIARA YA KINANA YADHIHIRISHA CCM BADO IPO IMARA MIKOA YA KUSINI

$
0
0

Wakazi wa Mtwara mjini wakishangilia wakati wa mkutano wa hadhara wa CCM ukiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Mtwara mjini kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Mashujaa ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa kazi ya CCM ni kuisimamia Serikali kutimiza wajibu wake kwa wananchi.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Mtwara mjini na kuwaa
 Mbunge wa Mtwara Mjini Ndugu Hasnain Murji akieleza utekelezaji wa ilani ya CCM ulivyotekelezwa vizuri kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mashujaa ambapo pia alieleza changamoto zinazowakabili wananchi wa Mtwara mjini hivyo kumtaka Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kusaidia katika kufanikisha baadhi ya mambo ambayo yameonekana kukwamishwa na viongozi wa juu serikalini.

 Wananchi wakilizunguka gari alilopanda Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya kumaliza kuhutubia kwenye viwanja vya Mashujaa Mtwara mjini.

MAPOKEZI YA KINANA MTWARA MJINI
  Vijana wa Bodaboda wakiongoza msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati akiwasili Mtwara mjini ambapo alishiriki shughuli mbali mbali za kujenga na kuimarisha chama pamoja na kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2010.
     Msafara wa Katibu Mkuu ukielekea Mtwara mjini.


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Mikindani mara baada ya kukabidhi leseni kwa madereva 70 wa boda boda waliohitimu mafunzo chini ya udhamini wa Mbunge wa Mtwara mjini Hasnain Murji.
                                                   MTWARA VIJIJINI 

 Wananchi wa kijiji cha Kitaya mkoani Mtwara wakishangilia ujio wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye kijiji hicho kinachopakana na nchi ya Msumbiji.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha Kitaya kilichopo mpakani na nchi ya Msumbiji ikiwa sehemu ya ziara yake mkoani Mtwara ambapo anakagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi pamoja na kujenga na kuimarisha chama.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wakazi wa kata ya Nanguruwe ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa kuna sheria zinazomkandamiza mkulima inabidi zitazamwe upya kwani zisipobadilishwa mkulima atakuwa anakandamizwa kila siku na kutoona faida ya kuwa mkulima wa korosho.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Ndugu Nape Nnauye akiwasalimia wakazi wa kata ya Nanguruwe wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa CCM kwenye wilaya ya Mtwara Vijijini,tarehe 28 Novemba 2014.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye mnara wa shujaa Ahamad Mzee aliyepambana na Wareno waliokuwa wanataka kuivamia Tanzania mwaka 1972 mpakani mwa Tanzania na Msumbiji.
                                                          TANDAHIMBA 

  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Tandahimba ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa zao la korosho lina hadithi nyingi sana na njia pekee ya kuleta ukombozi kwa mkulima ni kujenga kwa viwanda vya kutosha vya kubangulia Korosho nchini pia aliwataka wazazi wa Tandahimba kusisitiza elimu kwa watoto wao kwani ndio mkombozi pekee atakayekuja kuwakomboa kwenye maisha yao.
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Tandahimba ambapo aliwaambia wasihadaike na wapinzani ambao muda wao wa ujana wameutumia wakiwa CCM na uzeeni kuingia upinzani na kuanza kuhadaa watu walioishi kwa amani kwa muda mrefu.
  Wananchi wa Tandahimba mkoani Mtwara wakifuatilia kwa makini hotuba za viongozi wa CCM wakiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye anazunguka nchi nzima kukagua na kuimarisha uhai wa Chama.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa kata ya Mndimba wakati waujenzi wa ofisi ya CCM kata ya Mdimba wilayani Tandahimba.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha kadi zilizorudishwa na wapinzani kata ya Mdimba wilaya ya Tandahimba.
                                                   NEWALA 

  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwaonyesha wananchi wa Mkwedu kadi ya CUF iliyorejeshwa kwake na Hakika Ibrahim ambaye alirudisha kadi hiyo baada ya kuona na kuelewa utekelezaji wa ahadi za CCM unavyokwenda vizuri.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionnyesha kadi juu zilizorudi kutoka upinzani ambapo wanachama hao kutoka upinzani wameahidi kushirikiana na CCM kwa ajili ya kuleta maendeleo yaTengulengu wilayani Newala.
 Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Newala Ndugu  Adam Lawi Nangwanda Sijaona akivua nguo za Chadema mbele ya Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Ndugu Nape Nnauye.
 Wananchi wakishangilia kurejea kwa  Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Newala Ndugu  Adam Lawi Nangwanda Sijaona kwenye mkutano wa hadhara uuliofanyika kwenye viwanja vya Mahakama ya mwanzo Newala
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Newala kwenye viwanja vya Mahakama ya Mwanzo ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa Serikali lazima itafute namna ya kuhakikisha uzalishaji wa korosho wote unafanyika nchini kwa kujenga viwanda vya kutosha vya korosho.
Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Newala Ndugu  Adam Lawi Nangwanda Sijaona akiwa amekabidhi kadi yake na ya mkewe kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana .
                                                       NANYUMBU 

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Mangaka  wilaya ya Nanyumbu ambapo aliwaambia CCM ya sasa itakuwa kali kuliko wakati wowote na itaisimamia serikali na kuipongeza inapofanya vizuri na itakapofanya vibaya itasemwa.
  Wananchi wakimfurahia kumuona mkuu wao mpya wa mkoa.
                                                          LULINDI 

  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wananchi wa kijiji cha Machombe ambapo alipita kukagua ujenzi wa Bwawa la maji litakalo saidia kaya 150 kata ya Marika jimbo la Lulindi wilaya ya Masasi mkoani Mtwara.
 Wananchi wa Kijiji cha Machombe wilaya ya Masasi mkoa wa Mtwara wakishangilia wakati wa mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana anayetembea nchi nzima kukagua miradi mbali mbali ambayo zilikuwa ahadi za CCM.
 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana (katikati) akikagua maendeleo ya ujenzi wa Bwawa la maji akiongozana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mtwara Ndugu Mohamed Sinani (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mh. Farida Mgomi pamoaja na wanakijiji cha Machombe kata ya Marika.
 Kadi zilizorudishwa kutoka kwa wananchama wa vyama pinzani ambao kwa hiyari yao leo wamerudi na kujiunga na CCM kwenye mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana uliofanyika kwenye kijiji cha Chiungutwa wilayani Masasi.
 Wanachama wapya waliojiunga na CCM pamoja na jumuiya zake wakinyoosha kadi zao juu wakati wa kula kiapo cha uanachama mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye uwanja wa mikutano Chiungutwa wilayani Masasi mkoa wa Mtwara.
                                                      MASASI MJINI 

 Wanachama wapya waliojiunga na CCM pamoja na jumuiya zake wakinyoosha kadi zao juu wakati wa kula kiapo cha uanachama mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye uwanja wa mikutano Chiungutwa wilayani Masasi mkoa wa Mtwara.
 Wana CCM wakishangilia kuwasili kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye uwanja wa fisi wilayani Masasi.
 Katibu wa NEC itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa wilaya ya Masasi kwenye uwanja wa Fisi na kuwataka Watanzania kukiamini chama chao .
  Sehemu ya wananchi wakifuatilia kwa makini mkutano huo mjini Masasi.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Masasi ambapo aliwaambia viongozi wajenge utaratibu wa kuwaeleza wananchi maendeleo yao na yapi yamefanikiwa na wapi hawajafanikiwa, wapi yanakwamishwa.
                           MKUTANO WA HADHARA  LINDI MJINI

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Lindi mjini ambapo aliwaambia wananchi hao CCM ni chama pekee chenye mfumo ulioanzia chini hivyo watu waache unyonge Serikali hii ni ya CCM.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Lindi mjini kwenye uwanja wa michezo wa Ilulu wilaya ya Lindi mjini ambapo aliwaambia wananchi wa Lindi ni muda wa kuwaondoa wapinzani kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mwezi Desemba mwaka huu kwa kuipigia kura CCM.
                                                       RUANGWA 

 Mapokezi ya Kinana jimbo la Ruangwa
 Wananchi wa Ruangwa wakionyesha furaha yao wakati wa kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM kwenye uwanja wa mkutano Ruangwa Likangara.
 Wananchi wa Ruangwa wakiwa na mabango yaliyobeba ujumbe wakati wa mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kujenga na kukiimarisha chama,Katibu Mkuu wa CCM ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye .
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa wilaya ya Ruangwa
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wakazi wa wilaya ya Ruangwa waliojitokeza kwa wingi kumsikiliza,Kinana amekuwa Katibu Mkuu wa kwanza wa CCM kuzunguka nchi nzima ,kushiriki kwenye miradi mbali mbali ya maendeleo,kukagua ilani ya uchaguzi ya CCM 2010 pamoja na kutoa elimu kwa wananchi hasa ya kujiunga na mfuko wa afya ya jamii.
  Mbunge wa Jimbo la Ruangwa Majaliwa Kassim Majaliwa akihutubia wakazi wa Ruangwa ambapo alielezea katika kipindi chake tangu alipochaguliwa kuwa Mbunge ameshiriki shughuli mbali mbali za maendeleo jimboni kwake.
                                                        LIWALE  

  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa Liwale mkoani Lindi ambapo aliwaambia kuwa wapinzani kwenye mikoa hiyo hawajai hata kiganjani hivyo wananchi wasipoteze muda kwa wapinzani.
 Wananchi wa Liwale wakiwa wamejitokeza kwa wingi kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa wilaya ya Liwale mkoani Lindi ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa kuna haja ya kubadilisha taratibu za ajira badala ya kuwa za kudumu ziwe za mikataba kwani itasaidia kufanya kazi kwa ufanisi                                                      NACHINGWEA
  Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Nachingwea ambapo aliwaambia upinzani umepotea kabisa hivyo wasipoteze muda wao kushabikia
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Nachingwea ambapo aliwaambia kuwa CCM itakuwa wakali pindi serikali inapokosea mambo na kuchelewa kuchukua hatua, kwani maumivu na mateso wanapata wananchi, akizungumzia kusikitishwa kwake kwenye viwanda vya korosho ambavyo vimegeuzwa kuwa maghala na hakuna mtu serikalini amestuka kwa zaidi ya miaka kumi sasa.
                                                  MTAMA 

 Katibu wa NEC Itiakdi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Chiuta ambapo aliwaambia Chiuta ni nyumbani na aliwataka watu wachukue tahadhari na vyama visivyo na sera wala dira
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa Chuta ambapo aliwaambia kuwa maendeleo yanakuja kwa kufanya kazi na kujituma, ambapo aliwaambia kila nchi itaendelezwa na watu wake.
                                                               MCHINGA 

 Katibu wa Itkadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa Mchinga mkoani Lindi
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo wakati akihutubia wananchi wa Mchinga.
                                                 KILWA KUSINI 

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Kilwa Masoko ambapo aliwaambia watendaji wa serikali kutoa elimu ya kuwafahamisha wavuvi kabla ya kuchukua maamuzi ya kuchoma vifaa vyao vya kazi,pia aliwaambia wananchi hao kuwa Chama Cha Mapinduzi kitajirekebisha makosa yake na kuhakikisha kinashinda kwa kishindo kwenye chaguzi zijazo kwani jimbo la kusini Kilwa limepotea kutokana na migongano ndani ya CCM, hivyo basi uchaguzi ujao tujipange vizuri na kurudisha jimbo.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Kilwa Masoko ambapo aliwaambia kuwa wapinzani hawasemi ukweli unaoendelea kwenye vyama vyao havisemi kama vimekufa.
Mwananchi akishangilia jambo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika Kilwa Masoko kwenye uwanja wa Bustani ya Mkapa.
                                                         

  Umati wa wakazi wa kata ya Chumo wakiwa tayari kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kata ya Chumo kwenye viwanja vya shule ya msingi Chumo na kuwaambia kuwa huu si muda tena wa kuwasikiliza wapinzani kwani upinzani ulishaisha nchini hivyo .



Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa kata ya Chumo kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Chumo ikiwa siku ya kwanza ya kuanza ziara yake ya mikoa miwili ya Lindi na Mtwara.

BAADA YA KUONA MAPOKEZI YA DIAMOND DAR RAPPER AKA ATOA KAULI YAKE

$
0
0
AKAAKA ni rapper maarufu kutoka Afrika Kusini ambae alishinda tuzo moja kwenye tuzo za Channel O 2014 hapa Johannesburg Afrika Kusini ambako Diamond alishinda tuzo tatu kwa mkupuo.Baada ya kuziona picha na video za jinsi Watanzania walivyompigia shangwe Diamond Platnumz kwenye mapokezi yake kuanzia Airport Dar es salaam, A.K.A ilibidi aandike haya maneno.>
Kaandika >>> ‘Diamond alirudi Tanzania baada ya ushindi wa tuzo tatu za Channel O, jaribu kufikiria watu wa South Afrika wangeguswa na Wasanii wao kama hivi, kwenye nchi yangu mapokezi kama haya ni kitu ambacho kimehifadhiwa kwa ajili ya kina Justin Bieberna Chris Brown…. hongera Diamond’BOFYA KUSOMA ALICHOANDIKA>>

KAFULILA ALIVYOIBUA UFISADI AKAUNTI YA ESCROW

$
0
0
Fidelis Butahe, Mwananchi
Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila ameeleza namna alivyoibua sakata la uchotwaji wa Sh306 bilioni kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow na kudokeza kuwa kitendo cha baadhi ya watuhumiwa kugoma kujiuzulu, kinaonyesha kuna watu zaidi wanahusika.
Kafulila (32), ambaye alikuwa akiulizia suala hilo kila mara bungeni hadi uamuzi wa kulijadili ulipofikiwa, amesema ataendelea kulifuatilia hadi aone mwisho wake.
Akaunti hiyo ilifunguliwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuhifadhi fedha za malipo ya tozo ya ufuaji umeme baada ya Tanesco kuingia kwenye mgogoro na Kampuni ya IPTL na suala hilo kupelekwa mahakamani.
Kwa mujibu wa masharti ya uendeshaji wa akaunti za escrow, fedha hizo zilitakiwa zitolewe baada ya Mahakama kutoa uamuzi wa mgogoro huo, lakini wakati ilitaka pande hizo mbili zikutane na kukokotoa viwango vya tozo hizo, fedha hizo zilitolewa na kulipwa kwa mmiliki mpya wa Kampuni ya Pan African Power Solutions (PAP), jambo lililosababisha kuibuka kwa kashfa hiyo.
Akizungumza kwenye mahojiano maalumu na gazeti hili jana, Kafulila alisema alilinasa suala hilo kwenye vyombo vya habari na baadaye kupewa kurasa nne za maelezo ya sakata hilo, lakini baada ya kuliingiza kwenye chombo hicho cha kutunga sheria, wabunge wenzake waliendelea kumwongezea nyaraka hadi zikafikia kurasa 604.
"Lilikuwa ni jambo la furaha kwangu kuona kwamba wabunge wenzangu wamenipa nyaraka nyingi pamoja na kwamba walishakuwa nazo awali, lakini hawakuwa wametaka kuzitoa hadi nilipoingiza suala hili bungeni," alisema Kafulila ambaye aliingia bungeni kwa mara ya kwanza mwaka 2010... "Nyaraka hizi zilinisaidia sana."
Kupata ufahamu wa suala hilo kulikuwa kama bahati kwa mbunge huyo. "Nilianza kulifahamu suala la escrow nikiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakati nikienda Uswisi. Lilikuwa limeandikwa katika gazeti (jina tunalo) ambalo katika ukurasa wake wa kwanza walikuwa wamechora skendo mbalimbali za IPTL, kuanzia mwaka 1995 hadi 2014," alisema.
Aliongeza kuwa alipotoka safari aliikuta habari hiyo ikiwa imeandikwa kwa kina katika gazeti The Citizen na hivyo kumfanya ajenge hamu ya kutaka kujua undani wake. Alisema alianza kulifuatilia suala hilo kwa kuwasiliana na mmoja wa mawaziri wa Wizara ya Nishati na Madini ambaye awali alikuwa na utaratibu wa kumjulisha kila jambo linalofanywa na wizara hiyo.
"Nilimweleza mambo ambayo wizara inatakiwa kuyajibu kuhusu wizi wa fedha hizo ambao unaandikwa katika magazeti. Alinijibu kuwa wanaoandika habari hizo ni wababaishaji na wanaandika vitu wasivyovijua," alisema.
Alisema kutokana na unyeti wa suala hilo na sifa walizokuwa wakipewa watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini, hakukata tamaa na kuamua kulipeleka suala hilo bungeni ili litolewe ufafanuzi wa kina.
"Kabla ya mkutano wa Bunge kuanza nilimtafuta mtu mmoja (anamtaja jina) ambaye alinipa kurasa nne tu kuhusu IPTL na escrow tena kwa siri kubwa. Nilipozisoma nilielewa suala hilo. Mei mwaka huu wakati nikichangia hotuba ya Waziri Mkuu bungeni niliibua sakata hilo na kutaja majina ya wahusika," alisema.
Chanzo:Mwananchi

MTUNISI WA BONGO MUVI AKIONA CHA MOTO MAHAKAMANI!

$
0
0

Msanii nyota wa filamu Bongo, Nice Mohammed maarufu kama Mtunisi. Mtunisi alipandishwa katika Mahakama ya Mwanzo Manzese Sinza jijini Dar es Salaam Jumatatu iliyopita, ambapo baada ya kusomewa shtaka lake la kushambulia mwili, mtuhumiwa alikana na hivyo hakimu kuahirisha kesi hiyo hadi Desemba 15 mwaka huu itakapotajwa
tena.Hata hivyo, Mtunisi alishindwa kupewa dhamana baada ya hakimu kutoridhishwa na afya ya mwanamke huyo, Aziz ambaye anaugulia nyumbani.Katika hali nyingine, walinzi wa mahakama hiyo walionyesha mizengwe mikubwa kwa waandishi wa habari hizi, kwa kuwazuia kuingia ndani ya chumba cha mahakama wala kupiga picha, kwa madai kwamba sheria zao haziruhusu. SOMA ZAIDI>>>

DR SHEIN AKUTANA NA MABALOZI MICHEWENI ZANZIBAR LEO

$
0
0
unnamedRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba Mzee Mberwa Hamadi Mberwa   mara alipowasili  leo katika Viwanja vya Skuli ya Kiislamu ya Kiuyu  Wilaya ya Micheweni leo kwa madhumuni ya  kuzungumza na   Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani katika mkutano  wa kuimarisha  Chama  cha Mapinduzi (CCM) .[Picha na Ikulu.]unnamed1Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar akisalimiana na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi alipofioka katika Viwanja vya  Skuli ya Kiislamu ya Kiuyu  Wilaya ya Micheweni  leo kuzungumza na   Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani katika mkutano  wa kuimarisha  Chama  cha Mapinduzi (CCM) .[Picha na Ikulu.]
unnamed4Baadhi  ya WanaCCM  wa Wilaya ya  Micheweni  Pemba wakimsikiliza    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein  alipokuwa  akizungumza na Mabalozi na Wenyeviti wa   Maskani  wa  Wilaya hiyo  leo katika ukumbi wa  Skuli ya Kiislamu ya Kiuyu  Micheweni  akiwa  katika ziara ya kuimarisha  Chama  cha Mapinduzi (CCM) .[Picha na Ikulu.]unnamed6Wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa CCM (NEC) Dkt.Mauwa Daftari (kulia)  na Khadija Hassan Aboud wakifuatilia kwa Makini taratibu za Mkutano wa na Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani Wilaya ya Wete uliohutubiwa na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar leo katika ukumbi  wa Skuli ya Kiislamu ya Kiuyu  akiwa katika ziara ya kuimarisha Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kaskazini Pemba.[Picha na Ikulu.]
unnamed7Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar alipokuwa akizungumza na  Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani katika Mkutano wa Kuimarisha Chama cha Mapinduzi CCM katika   Ukumbi wa Skuli ya Kiislamu ya   Kiuyu Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba leo akiwa katika ziara ya kuimarisha Chama.[Picha na Ikulu.]unnamed8Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba Mzee Mberwa Hamadi Mberwa   alipokuwa akimkaribisha  Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai kuzungumza na machache katika Mkutano wa Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani   ili nae akmaribisha  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar kuhutubia Mkutano huo katika ukumbi wa Skuli ya Kiislamu ya Kiuyu  akiwa katika ziara ya kuimarisha Chama cha Mapinduzi  Mkoa wa Kaskazini Pemba leo .[Picha na Ikulu.]unnamed65Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar akiteta jambo na  Naibu  Katibu Mkuu wa  CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai  wakati wa Mkutano wa Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani katika Wilaya ya Micheweni  katika ukumbi wa Skuli ya Kiislamu ya Kiuyu  akiwa katika ziara ya kuimarisha Chama cha Mapinduzi  Mkoa wa Kaskazini Pemba leo.[Picha na Ikulu.]

MDOGO WAKE ZARI APONDA UHUSIANO WAKE NA DIAMOND

$
0
0
Mdogo wake na Zari Hassan aka The Bosslady, aitwaye Karim ametumia Facebook kumkosoa dada yake kwa kuwa na uhusiano na Diamond Platnumz ambaye anamzidi miaka 9.Kwenye post hiyo, Karim aliandika: You are ashaming us, how can you date a boy my age. You moved from one man to another in less than 3 days.”Akitumia akaunti yake binafsi ya
Facebook yenye jina ‘Zarinah Tlale’, kujibu post hiyo ya mdogo wake huyo ambaye hapendezwi na kitendo cha dada yake kuwa na uhusiano na mtu mwenye umri kama wake, Zari alisema si Karim aliyeiandika.
“Diamond is just a friend of mine. It’s never been written that female and male can’t be friends, it’s just the backward people that use that kind of perspective to blow things out of proportion,” aliandika.BOFYA KUSOMA KAULI YA MDOGO WAKE ZARI>>>

KUHUSU BALAA LA MAFURIKO JIJINI MWANZA

$
0
0

 

Askari wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji akishuka baada ya kumuokoa mtoto eneo la Mabatini, jijini Mwanza lililokumbwa na mafuriko baada ya Mto Mirongo kufurika kutokana na mvua iliyonyesha jana. Picha na Michael Jamson  

Baadhi ya wakazi wa Kata ya Mbugani, Mtaa wa Mbugani A na B wameathiriwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha jana kwa saa nne.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wakazi hao walisema mvua hiyo imesababisha vitu vyao kusombwa na maji na nyumba kubomoka.
Esther Misanga, mkazi wa mtaa huo, alitaja baadhi ya vitu vilivyoharibiwa na mvua hiyo kuwa ni magunia 20 ya mahindi, magunia 10 ya daga na mifuko 20 ya unga wa sembe, vyote vikiwa na thamani ya jumla ya Sh2 milioni.
“Nimepoteza magunia 50 ya mahindi na unga wa dona. Nimepata hasara kubwa sana. Sikutegemea yangetokea mafuriko makubwa kama haya,” alisema Misanga.
Alisema Serikali iliwaahidi kuwahamisha maeneo hayo kutokana na kupata adha ya mafuriko ya mara kwa mara, lakini hadi sasa utekelezaji huo haujafanyika.
“Serikali ilituahidi kutupatia maeneo kule Kisesa, lakini tangu wazungumze hadi sasa mwaka umepita hawajatuonyesha maeneo hayo. Tunaiomba Serikali ifanye kila liwezekanalo ituhamishe katika eneo hili tunusuru maisha yetu,” alisema Misanga.
Akizungumza kwa simu, mtendaji wa Kata ya Mbungani, Baruani Hawadhi alisema maafa hayo siyo makubwa kwa kuwa hajapata taarifa za vifo vya watu zaidi ya uharibifu wa mali za watu

GARI LAPAGONGA UZIO WA OFISI ZA SUMATRA, DAR

$
0
0
Waswahili walisema ajali haina kinga ila hii tunaweza kusema imesababishwa na uzembeee... ni pale dereva wa gari hili alipokuwa mwendo wa kasi huku akijaribu kumkwepa dereva wa bodaboda na kujikupa amevamia uzio wa ofisi za SUMATRA zilizoko barabara ya Ali Hassan Mwinyi na kujikuta amepenya ndani kupitia uzio.

Vijana wakijaribu kumkwamua aweze kutoka.
CHANZO:KAJUNASON BLOG

ZITTO AMTAMBULISHA MCHUMBA WAKE KIGOMA

$
0
0

TAARIFA MPYA KUHUSU MAUAJI YA KIKATILI YA WANAWAKE JIJINI DAR!

$
0
0

Picha kutoka #DARYETU @Daryetu on Instagram Kama ulisikia kuhusu mauji ya Wanawake mbalimbali kwenye jiji la Dar es salaam utakua ulitamani kujua wanaohusika manake stori zilikua zinaripotiwa tu na taarifa zinazoambatana nazo ni kwamba uchunguzi unaendelea.
Sasa mpaka sasa unaambiwa ni zaidi ya Wanawake 11 wameuawa Dar es Salaam katika kipindi cha miaka miwili na kutupwa barabarani au mitaroni huku miili yao ikiwa imefanyiwa vitendo vya unyama na udhalilishaji.Kutokana na mauaji kuendelea, Polisi wamefanikiwa kuwakamata watu wawili akiwemo ABOUBAKAR KASSANGA Mkazi wa Mwenge na EZEKIEL ASENEGALA mkazi wa Tandika Dar es Salaam ambao wamekiri kuhusika na vitendo hivyo ndani ya kipindi cha miaka miwili.

Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam SULEIMAN KOVA amesema baada ya kuwahoji watuhumiwa hao ambao pia wamekiri kuwauwa wasichana wawili hivi karibuni waliotajwa kwa majina ya WANZE MAKONGORO na JACKLIN MASSANJA wamesema wamekuwa wakiwalaghai wasichana kimapenzi na badae kuwaua.

Katika hatua nyingine Kamishna KOVA ametoa tahadhari kwa wasichana kuacha tabia ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi wa ghafla na watu wasiowafahamu ambapo tukio la mauaji ya wasichana hao wawili lilitokea Novemba 19 mwaka huuambapo baadhi ya vitu vinavyosadikiwa kuwa vya wasichana hao vimekutwa mahala wanapoishi watuhumiwa hao.

Kamishna KOVA amesema upelelezi bado unaendelea ili kuunasa mtandao mzima wa uhalifu huo.

SIRI YA MTUNGI SEHEMU YA PILI YAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
6Maofisa kutoka kampuni ya John Hopkins University For Communication Programs (JHU CCP) ambao moja wa wadhamini wa tamthilia hiyo katika picha ya pamoja.7Le Mutuz akiwa na mmoja wa waigizaji wa Tamthilia ya Siri ya Mtungi awamu ya pili Richa Adhia, Msemaji wa Umoja wa Vijana wa CCM, Paul Makonda na Muigizaji mkongwe nchini, Mwita nao walikuwepo katika uzinduzi huo
8
Le Mutuz akiwa na Msemaji wa Umoja wa Vijana wa CCM, Paul Makonda
9Waigizaji wa Tamthilia ya Siri ya Mtungi wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya uzinduzi rasmi kwenye ukumbi wa Cinemax Century
1Muongozaji wa Tamthilia ya Siri ya Mtungi, Jordan Riber akizungumza katika uzinduzi wa tamthilia hiyo Sehemu ya pili  kwenye ukumbi wa Cinemax Century jijini Dar es salaam.
3MC wa shughuli ya uzinduzi wa Siri ya Mtungi 2, Ambi Lusekelo akimtambulisha muigizaji nyota wa tamthilia hiyo, Cheche4Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Nchini, Joyce Fisoo Katikati na wadau wa Filamu Tanzania waliohudhuria katika uzinduzi huo  wakifuatikia hotuba bali mbali zilizotolewa wakati wa uzinduzi wa Tamthilia ya Siri ya Mtungi awamu ya pili.
…………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi wetu
Bodi ya Filamu Tanzania imewataka waandaaji wengine wa fani hiyo kuiga mfano wa waandaaji wa tamthilia ya Siri ya Mtungi, Shirika Lisilo la Kiserikali (NGO ya Media for Development International Tanzania (MFDI-TZ) kwa kutoa filamu yenye mafundisho mbali ya kuburudisha.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce Fissoo kupitia kwa mwakilishi wake, Beatrice Sumari kwenye ukumbi wa Cinemax Century wakati wa uzinduzi rasmi uliowashirikisha wadau wa fani hiyo, wadhamini na waandaaji.
Sumari alisema kuwa Tamthilia ya Siri ya Mtungi Msimu wa Pili mbali ya kuburudisha, pia imetoa ajira kwa Watanzania wengi, pia imeleta changamoto kuhusiana na mabadiliko ya tabia kwa jamii.
“Filamu imetengenezwa kwa ubora wa hali ya juu, hii ni fursa kwa wadau wa fani hiyo kuiga MFDI-Tanzania kwa kuleta katika jamii filamu yenye ubora huu, naomba wengine wafuate nyayo zao,” alisema  Sumari.
“Filamu hiyo ina ubora  wa picha, sauti, maudhui na mfuatano wa matukio wa kipekee na kuleta burudani ya aina yake.. ni tamthilia ambayo ukianza kuangalia, hauta kinai na kuwa na hamu ya kufuatilia kile kinachofuata,” alisema.
Afisa kutoka Taasisi ya Misaada ya Wamarekani kupitia (Usaid), Ana Bodipo alisema kuwa wanajisikia furaha kudhamini tamthilia hiyo ambayo imezungumzia maisha halisi ya Mtanzania.
Bodipo alisema kuwa alisema kuwa tamthilia hiyo inaelekeza jamii kuhusiana na ugonjwa hatari wa Ukimwi na kwa wao ni moja ya nyenzo ya kushiriki katika masuala ya afya katika maeneo mbalimbali nchini.
“Matukio mengi katika tamthilia hii yana akisi taswira ya kweli katika jamii na na kuwafanya wafuatiliaji kupata somo halisi kutokana na changamoto mbalimbali,” alisema Bodipo.
Mtayarishaji wa tamthilia hiyo, Louise Kamin kutoka taasisi ya Media for Development International Tanzania (MFDI-TZ) alisema kuwa wamefuraishwa na mapokeo ya tamthilia hiyo pamoja na kuhitimisha na kufichua kilichopo katika mtungini.
alisema kuwa sehemu ya pili ya tamthilia hii inakamilisha Siri ya Mtungi kufuatia msisimko mkubwa wa msimu wa kwanza.
Kamin alisema kuwa kukamilika kwa hatua ya pili kunatokana na udhamini mnono wa the John Hopkins University Centre for Communication Programs (JHU CCP) ambao walitoa uongozi wa elimu na mkakati katika tamthilia, taasisi ya Misaada ya Wamarekani kupitia (Usaid), Wizara ya Afya Ustawi wa Jamii na MFDI.
Mwisho….

MASHABIKI WA DIVA WA ALA ZA ROHO WAMJIA JUU MENEJA WA CLOUDS FM!

$
0
0
Mashabiki wa kituo cha redio cha Clouds FM wiki hii wameungana na watu wengi mbalimbali kukipongeza kwa kutimiza miaka 15 tangu kianzishwe, lakini kuna kundi moja la watu halina furaha – mashabiki wa kipindi cha Ala za Roho kinachoendeshwa na Loveness aka Diva the Bawse. 
Kuna taarifa kuwa mtangazaji huyo mwenye mashabiki wengi, amesimamishwa kazi. Awali wasikilizaji wake waliambiwa kuwa Mrs GK, yupo likizo lakini baada ya kuona likizo ya mwezi mmoja inakuwa miezi, walianza kuhisi kuna kitu hakipo sawa. 
Kwa muda mrefu wamekuwa wakikitaka kituo hicho kuwapa majibu ya kwanini hawamsikii malkia wao bila kupata majibu. Wengine wamefikia hadi hatua ya kwenda kwenye kituo hicho kuuliza kunani na bado wanadai wahusika wamekuwa wakiwakwepa. 
Na sasa, mashambulizi yao wameyahamishia kwa meneja wa vipindi wa kituo hicho, Sebastian Maganga ambaye post yake ya juzi katika birthday ya Clouds FM iligeuka uwanja wao wa kumwaga malalamiko yao. 
“Brother @sebamaganga turudishiee #alazaroho na mrembo wetu @divathebawse tutaandamaanaa MZEE tujee mjengoniiii tumemis saut ya kumtoa nyoka pangonii please tunampenda @divathebawse yuko wapiii bnaaaah brother,” aliandika Young wa Leo. 

MKAO WA KULA! ALIKIBA AENDA CAPE TOWN. SOUTH AFRICA KUSHOOT VIDEO MPYA!

BINTI WA KIGOGO AFANYIWA MBAYA COCO, DAR

$
0
0
 
ULEVI noma! Ndivyo unavyoweza kusema kuhusu kilichomtokea mtoto wa kigogo mmoja aishie Masaki ambaye alijikuta akifanyiwa kitu mbaya ndani ya maji kwenye ufukwe wa Bahari ya Hindi, eneo la Coco jijini Dar, Jumamosi iliyopita.Binti akijiachia na njemba huyo baada ya kupiga urabu wa kutosha.
Kabla ya tukio hilo, inadaiwa kuwa dada huyo ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja, alikesha katika klabu moja iliyopo ufukweni hapo, akipiga ulabu yeye pamoja na kampani yake.Ilipofika asubuhi, inadaiwa kuwa, ili kupunguza ulevi aliokuwa nao kichwani, aliamua kwenda kuogelea, ili akae sawa.

Chanzo kilichoshuhudia tukio hilo kilishadadia maneno kwa mpigapicha wetu kwa kusema kuwa, wakati mrembo huyo anaenda kuogelea ndipo alipoangukia kwenye mikono ya njemba mmoja aliyekuwa akifanya mazoezi pembeni mwa ufukwe huo ambapo pia alikutana na wachezaji wa Azam FC waliokuwa wakifanya mazoezi mambo yakaharibika.SOMA ZAIDI>>>

HUYU ZARI NI NANI?! MFAHAMU KWA KINA HAPA..PIA KAMA ULIMISS DIAMOND KUWA MGENI RASMI

$
0
0

RAIS AKATAA MTU YEYOTE KUTUMIA JINA LAKE

$
0
0
 
Mwaka mmoja kabla ya kiongozi wa taifa la North Korea Kim Jong Un kuchukua mamlaka agizo lilitolewa kwa mtu yeyote aliye na jina kama lake kulibadilisha ili kuendeleza utamaduni wa utawala wa familia ya Kim.
Kulingana na nakala za kimataifa zilizopatikana na Runinga ya KBS nchini Korea Kusini zilizo na maagizo ya utawala wa Kim Jong wa Pili vitengo vya polisi na jeshi vilitakiwa kuhakikisha kuwa agizo hilo linatekelezwa.
Agizo hilo lilitolewa mnamo mwezi January mwaka 2011 mda mfupi baada ya Kim Jong Un kuteuliwa kama mrithi wa babaake.
Kim Jong wa Pili alifariki mwezi Disemba mwaka huohuo.
''Vitengo vyote vya chama na mamlaka ya usalama ni sharti viweke orodha ya watu walio na majina ya Kim Jong Un na kuwafundisha vile watakavyobadilisha majina yao'',ilisema nakala hiyo ambayo baadhi yake ilitangazwa moja kwa moja na runinga ya KBS.
Mpango huo ulishirikisha kubadilisha majina katika stakhabadhi rasmi,ikiwemo katika kadi za usalama wa jamii na vyeti vya masomo.

Maafisa pia waliagizwa kukataa vyeti vya kuzaliwa vya watoto wachanga walio na majina ya Kim Jong Un.

Vilevile Mamlaka ziliagizwa kuhakikisha kuwa hakuna mtu anayelalamika ama kueneza uvumi.
Chimbuko la agizo hilo rasmi halikuweza kuthibitishwa huku wizara ya Seoul ikikataa kuthibitisha iwapo madai hayo ni ya ukweli.

Lakini Afisa mmoja wa utawala wa Pyong yang alidai kwamba Utawala huo uliwapiga marufuku raia wake kutumia jina la rais wa kwanza wa taifa hilo Kim wa pili Sung na mwanawe Kim jong wa Pili.

via>BBC
Viewing all 32622 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>