SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), imepanga kuwafikia wajasiriamali wapya zaidi ya milioni 22 walio katika sekta isiyo rasmi. Hayo yamesemwa na Meneja wa Mafao wa shirika hilo, James Oigo wakati wa Semina ya kukuza mitaji kwa njia ya ubia katika sekta zisizo za kibenki iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na kuwashirikisha wadau mbalimbali. Semina hiyo ilidhaminiwa na NSSF, TPSF.
Akichangia mada katika semina hiyo, Oigo alisema kuwa NSSF inatoa mafao ya muda mrefu na muda mfupi yakiwemo mafao ya ya matibabu.
'Watu wengi wanatumia gharama kubwa kwenye matibabu na kuwaongezea umaskini kwa sababu ya gharama kubwa za matibabu".
“Mafao yetu yamejikita kusaidia wateja wa sekta binafsi na wa serikali, lakini pia hata wale wanaofanya kazi kwa kujitegemea kama atakuwa mwanachama wetu atapatiwa fao hilo kama wengine tena katika hospitali atakayochagua yeye mwenyewe katika zile ambazo tumeingia nazo mkataba na kupewa fao hilo”. alisema.
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSS) inatoa Mafao ya Pensheni ya uzee, Mafao ya pensheni ya ulemavu, Mafao ya pensheni urithi, Mafao ya mazishi, Mafao ya uzazi, Mafao ya kuumia kazini na magonjwa yatokanayo na kazi na Mafao ya matibabu.
Meneja wa Mafao wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), James Oigo akitoa mada kuhusu wafanyabiashara wadogowadogo, kujua maana ya kuwepo kwenye hifadhi ya jamii kwa ajili ya maisha yao ya baadae, katika semina ya kukuza mitaji kwa njia ya ubia katika sekta zisizo za kibenki iliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Katikati ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Dk. Reginald Mengi. Semina hiyo ilidhaminiwa na NSSF.