Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all 32622 articles
Browse latest View live

SEMINA MAALUM YA WASANII KUHUSU PENSHENI YAFANYIKA LEO LIVE!!

$
0
0


001Mkurugenzi  Mtendaji  Kampuni ya Chief Promotion Amoni Mkoga akitoa hotuba yake wakati wa semina ya wasanii wa Muziki pamoja na bongo movie iliofanyika katika ukumbi wa Vijana Kinondoni jijini Dar es Salaam 21 Februari-2014 lengo la semina hiyo ilikuwa kuzungumzia hakimili kwa wasanii pamoja na kujiunga na mifuko ya jamii ili kujiwekea akiba ya baadae (kushoto), Afsa Mwandamizi wa Huduma kwa Mlipa Kodi TRA, Msafiri Mbibo (watatu kulia), Kaimu Afsa Kumbumbuku COSOTA Bw Philemon Kilaka, na wakwanza kulia Kaimu Mwanasheria COSOTA Bw,Zephania Lyamuya.
002
Mkuu wa Mawasilano Promosheni na Uhamasishaji wa Mfuko wa Uthibiti wa Mfuko  Hifadhi Nchini (SSRA), akiwaelezea wasanii kuhusiana na
mifuko mbalimbali ya hifadhi ya  jamii kama NSSF,PSPF ,LAPF,GEPF,PPF,NHIF  juu ya faida pale wapofikia muda wakustaafu kazi  kisanii au kupatwa na matatizo mbalimbali (katika), Mwanasheria COSOTA Bw,Zephania Lyamuya (kusho), Kaimu Afsa Kumbumbuku COSOTA Bw Philemon Kilaka.003
Afsa Mwandamizi wa Huduma kwa Mlipa Kodi TRA, Msafi Mbibo akiwaelezea wasanii mwongozo wa utumiaji mashine maalumu za kodi za kielekitroniki (EFDs), wakati wa semina ya hatimiki kwa sanii mbalimbali wa bongo movie pamoja na muziki,004
Kaimu Afsa Kumbumbuku COSOTA Bw Philemon Kilaka.akiwaezea wasanii jinsi hakimiliki na mikataba katika kazi za sanaa.005
Afsa wa Mfuko wa Penseni (PSPF), Haji Jamadary nae akiwaelezea wasanii kuhusiana na uchangiaji katika mpango wa hiyari wakati wa kutegemea upatikanaji wa kipato cha ziada kwa ajiliya akiba.006
Mwenyeki wa Bongo Movie, Steven Mengeze akiwasisitiza wasanii wenzake kuhudhuria kwenye semina pamoja na  kujiunga na  mifuko ya hifadhi ya jamii na namna ya kufuatilia  upatikanaji wa haki za kazi zao za sanaa.
007
Wasanii mbalimbali wakifuatilia kwa umakini mada mbalimbali wakati wa semina hiyo.008
Msanii Aliy Mango akionesha umahiri wake wakucheza na nyoka wakati wa semina hiyo.
009
Msanii Aliy Mango akionesha umahiri wake wakucheza na nyoka wakati wa semina hiyo.
PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE DAR ES SALAAM

BAADHI YA MASUPER STAR WA DUNIA WALIOKUFA NA UKIMWI LIVE!!

$
0
0
Fela Kuti
Huyu alikua muanzilishi haswaa wa Afro-beat.Alikua Star wa kimataifa kutoka Nigeria  aliyeenda chuo  huko Los Angeles , Marekani kusomea udaktari akajikuta anaingia kwenye muziki. Kuti alifariki tarehe 3 ,August 1997 huku akiwa ni mwanaharaki mkubwa wa ukimwi na waziri wa afya wa zamani.Watu zaidi ya millioni moja walihudhuria msiba wake.
FELA-kuti
Rock Hudson
Rock alikua ni mchekeshaji wa miaka ya zamani na kifo chake cha Oct. 2, 1986 ndio kilishtua wengi kuhusu Ukimwi.Hapa ndipo rafiki yake na star mwenzake Elizabeth Taylor alipoamua kutumia maisha yake yote yaliyobaki kufanya research kuhusu ukimwi.
rock-hudson1
Freddie Mercury
Alikua mmoja kati ya waimbaji wa bendi maarufu kabisa duniani miaka ya 80 hadi 90, Queen. Mercury alikufa akiwa na miaka 45 ilikua november 24 mwaka 1991. Siku chache kabla hajafa Mercury aliamua kujitangaza kwamba ni muathirika wa ukimwi.
Freddie-Mercury
Arthur Ashe
Huyu alikua ni mcheza tennis maarufu sana duniani. Alipata ukimwi sio kwa njia ya kujamiiana kama unavyofikiria bali ni kwa kuchangia damu. Arthur alikufa akiwa na miaka 49, February 6 mwaka 1993.
Arthur-Ashe
Eric “Eazy-E” Wright
Alikua kwenye kundi la Rap lililoitwa  N.W.A. ambapo alikua pamoja na Ice Cube and Dr. Dre.Waliuza mamilioni ya albums marekani hadi hapo March 26 mwaka 1995 Eazy-E alipofariki kwa Ukimwi.
Eric-Wright
Kwa Bongo uwazi wa gonjwa hili bado haujawa mkubwa na kuna baadhi ya watu maarufu wameondoka kwa gonjwa hili lakini hakuna taarifa zozote.BAKI NJIA KUU  OGOPA MICHEPUKO !


INASIKITISHA:MWALIMU ALIYEMCHINJA KIKATILI MWANAFUNZI WAKE NAYE AUAWA MBAGALA...SOMA ZAIDI HAPA

$
0
0
Mwalimu wa madrasa ya Ali Munawar, ustaadhi Mohamed Ngulanjwa (36) wa Mbagala Mianzini jijini Dar es Salaam, ameuawa baada ya kumchinja mwanafunzi wake.
Ustaadhi huyo aliyekuwa mwalimu wa madrasa na shule ya awali ya Ali Munawar, alimchinja mwanafunzi huyo saa 12.10 jioni kwenye eneo la madrasa baada ya kutenganisha kichwa na kiwiliwili
(hudugu)




Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Temeke, Jonathan Shana, akizungumzia mauaji hayo , alisema tukio hilo la kinyama, lilishuhudiwa na wananchi waliomuua ustadhi huyo.

Alisema baada ya mwalimu kumuua mwanafunzi wake wa kiume alichukua kisu alichotumia pamoja na msahafu na kukimbia.


"Ilidaiwa kuwa alimchukua mtoto huyo , kumlaza chini kisha kumchinja kwa kutenganisha kichwa na kiwiliwili na kutelekeza vipande vya mwili wake kwenye varanda," alisema Kamanda Shana.
Baada ya mauaji hayo mtuhumiwa alianza kukimbia lakini wananchi walimvamia na kumshambulia kwa mawe na kila silaha iliyokuwa karibu na kumuua papo hapo.

Shana alieleza kuwa polisi walifika eneo la tukio na kuchukua maiti hizo na kuzipeleka hospitali ya Temeke.

 Hata hivyo alisema jina la mtoto huyo mwenye umri kati ya miaka 10- 12 halikufahamika na polisi inaendelea na uchunguzi

KAMA ULIKUWA HUJUI THE MIGHTY MBEYA CITY ONA KILICHOWATOKEA JANA LIVE KWENYE LIGI YA SOKA YA BONGO!!

$
0
0


Coastal union 2 Mbeya city 0
 
HERE COMES THE GAME CHANGER no. 10
MOHAMED MTINDI The MAX MAN The KILLER.
 
ANAINGIA MBADILISHAJI MCHEZO na. 10
MOHAMED MTINDI "MLENGA SHABAHA NA
MUUWAJI".

BILA KUJALI PESA JANETH JACKSONY AMPA TARAKA MUMEWE BILLIONARE

$
0
0
LIMAO TOKA KWA MDAKU WA ANGAZA TZ  ANASEMA KUWA CHANZO NI KUWA JAMAA HUYU RAIA WA QUA-TAR JINA ANAITWA WISSAM ALIKUWA NI MTU WA MASAFAFA KILA WAKATI BILA KUMJALI MKEWE JANETH AMBAYE NI MTULIVU SANA, KITU AMBACHO JANETH MWENYE KIU YA MAPENZI NA MWANAUME HUYO ALIYE MPENDA KILIMUUMIZA SANA KWANI HATA MUDA WA KUENJOY NA JAMAA HAUKUWEPO, MUDA WOTE MISHE KITU AMBACHO KILIMPA HOFU SANA MWANADADA HUYO WA RIP MKALI WA POP, BY THE WAY KILA CHENYE MWANZO KINA MWISHO ACHILIA MBALIA BINTI KAOKOKA ,AKAMTOSA JAMAA..


NA HAYA NDIO MAJINA 10 YA WASICHANA NA 10 YA WAVULANA BORA KITAIFA ON MATOKEO YA MITIHANI YA KIDATO CHA NNE 2013!! LIVE!!

$
0
0


Watahiniwa wa kike wamefanya vizuri kwa kuchukua nafasi saba kati ya 10 za juu, huku Shule ya Marian Girls ya Pwani ikiongoza kwa kuwa na wanafunzi wanne.

Mwanafunzi aliyeongoza ni Robina Nicholaus wa Shule ya Marian Girls, akifuatiwa na Magrath Kakoko wa St Francis (Mbeya) wakati wa tatu ni Joyceline Marealle kutoka Shule ya Canossa (Dar es Salaam).

Wengine ni Safarina Mariki na Abby Sembuche wa Marian Girls, wakati wavulana pekee kwenye wanafunzi 10 bora ni Sunday Mrutu kutoka Anne Marie (Dar es Salaam) na Nelson Rugola Anthony na Emmanuel Mihuba Gregory wa Kaizirege (Kagera).

Wanaofuata ni Janeth Urassa kutoka Marian Girls (Pwani) na Angle Ngulumbi wa St Francis (Mbeya).

Wasichana 10 bora
Wasichana waliofanya vizur kwenye mtihani huo wameongozwa na Robina Nicholaus (Marian Girls), Magrath Kakoko (St Francis), Joyceline Leonard Marealle (Canossa), Safarina W Mariki, Abby T Sembuche na Janeth Urassa (Marian Girls).

Wengine ni Angle Ngulumbi (St Francis), Getrude James Mande wa Precious Blood (Arusha), Violet Mwasenga wa St Francis na Catherine Swai kutoka Marian Girls.

Wavulana 10 Bora
Wavulana waliofanya Vizuri ni Sunday Mrutu wa Anne Marie, Nelson Rugola Anthony na Emanuel Mihuba Gregory wote kutoka Kaizirege, Razack Hassan wa St Matthew’s (Pwani) na Hamis Msangi kutoka Eangles (Pwani).

Wengine ni Joshua Zumba wa Uwata (Mbeya), Brian Laurent na Mohamed Ally wa Marian Boys (Pwani), Shahzill Msuya wa St Amedeus (Kilimanjaro) na Shabani Hamisi Maatu wa Mivumon Islamic Seminary (Dar es Salaam).

Shule za serikali hoi
Matokeo yanaonyesha kuwa shule kumi za kwanza ni za binafsi tu na shule za Serikali zimeanguka vibaya.

Shule bora ni St. Francis Girls ya Mbeya, Marian Boys ya Pwani, Feza Girls ya Dar es Salaam, Precious Blood ya Arusha, Canossa ya Dar es Salaam, Marian Girls ya Pwani, Anwarite Girls ya Kilimanjaro, Abbey ya Mtwara, Rosmin ya Tanga na Don Bosco Seminary ya Iringa.

Katika shule zenye watahiniwa chini ya 40 shule iliyoongoza ni Kaizirege ya Kagera, Alliance Girls ya Mwanza, Thomas More Machrina ya Dar es Salaam, Mwanza Alliance ya Mwanza na Queen of Apostles Ushirombo Seminary ya Geita.

Nyingine ni St Joseph Kiloc

GAZETI LA MWANANCHI LATAKA MBUNGE ALIYEFOJI KUINGIA NA MKEWE BUNGE LA KATIBA AONDOLEWE MARA MOJA!!

$
0
0

Mwenyekiti wa Chama cha National League for Democracy (NLD), Dk Emannuel Makaidi akichangia jambo kwenye kongamano siku za hivi karibuni 

  • Tanzania imekuwa taifa la ajabu na masikitiko yetu ni kwamba mporomoko wa maadili katika jamii yetu umeziba mitima na dhamira za viongozi wetu na jamii nzima kwa jumla kiasi cha kuyaona matendo hayo kama mambo ya kawaida.

Uzoefu wetu wa
muda mrefu umetuonyesha pasipo shaka kwamba mambo mengi yanayotendeka Tanzania hayawezi kutendeka katika nchi nyingine.
Tanzania imekuwa taifa la ajabu na masikitiko yetu ni kwamba mporomoko wa maadili katika jamii yetu umeziba mitima na dhamira za viongozi wetu na jamii nzima kwa jumla kiasi cha kuyaona matendo hayo kama mambo ya kawaida.
Tunayo mifano ya matukio lukuki ya ajabu na ya kushtusha yaliyowahi kutokea hapa nchini lakini yakaonekana kama ya kawaida.
Fikiria wafanyabiashara walioiba mabilioni ya fedha za Epa ambao muda mfupi kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2005 walikwenda Benki Kuu ya Tanzania (BoT) wakati wa siku za mapumziko na kukwapua mabilioni hayo kwa njia za udanganyifu. Fikiria wezi hao walivyoahidiwa kwamba iwapo wangezirudisha wasingechukuliwa hatua yoyote.
Ebu fikiria nchi ambayo kiongozi wake anakwenda ughaibuni na kutangaza kuwapo kwa majangili mapapa 40 na kusema kiongozi wao yuko mikoa ya Kaskazini, badala ya kusema hayo akiwa nchini, ikiwa ni pamoja na kuyakamata majangili hayo na kuyachukulia hatua.
Ebu fikiria matukio haya mawili ambapo Waziri Mkuu anatamka bungeni kwamba ni sawa tu kwa Jeshi la Polisi kuwapiga wananchi ‘wakorofi’, huku mkuu wa nchi akikiagiza chama chake cha siasa ambacho yeye ni mwenyekiti kuwapiga wapinzani anaodai wanafanya vurugu dhidi ya wafuasi wa chama chake. Ni nchi gani ambayo viongozi wake wakuu wanaweza kutoa amri hizo za hatari?
Tumesema yote hayo kutokana na kitendo cha ajabu na aibu kilichofanywa na Mwenyekiti wa Chama cha National League for Democracy (NLD), Dk Emannuel Makaidi cha kufanya ulaghai na kujiwezesha yeye na mkewe kuteuliwa kuingia katika Bunge la Katiba.
 Katika utetezi wake, ametoa hoja za kuchefua na kughadhabisha kuwa, kwa vile mke wake naye ni mwanachama wa chama hicho alikuwa na haki ya kuteuliwa kama ilivyo kwa Rais Kikwete na mke wake ambao wote ni wajumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM.
Tunasema uteuzi huo haukubaliki hata kidogo kutokana na kukiuka taratibu zilizowekwa kisheria kwamba vyama vya siasa lazima viwe na sura ya Muungano katika mfumo na uendeshaji wake.
Ni ujasiri na uthubutu wa kiwango cha juu kujiteua yeye na mkewe kama vile NLD ni mali ya kifamilia. Kudai kwamba aliteua majina ya wanachama wanne na Rais akamchagua yeye na mkewe ni uongo wa kupitiliza.
Hii inaonyesha kwamba zilikuwapo mbinu chafu katika mchakato wa uteuzi huo, vinginevyo wanachama wa Zanzibar wangenyimwa vipi uwakilishi? Hatua ya chama hicho upande wa Zanzibar ya kumtaka Rais Kikwete atengue uteuzi wa Dk Makaidi na mkewe lazima iungwe mkono.
Tatizo hapa ni hatua ya Serikali kuendelea kuvibeba kwa sababu za kisiasa vyama vya siasa vilivyokufa siku nyingi. Ukweli ni kwamba NLD na vyama vingine vingi ambavyo kwa mujibu wa sheria ya vyama ya 1992 vinapaswa kufutiwa usajili wa kudumu bado vinatambuliwa kiasi cha viongozi wake kuingizwa katika Bunge Maalumu la Katiba bila kuwa na sifa stahiki.
 Hivyo, wananchi wawe tayari kushuhudia vitimbi vya viongozi wa vyama hivyo ndani ya Bunge. Ndiyo maana tunasema mambo mengi yanayofanyika Tanzania hayawezi kufanyika katika nchi nyingine.

BREAKIN NEWZZ:- ILE ISHU YA POSHO NA WABUNGE WA KATIBA DODOMA SASA NI DEAD HAIPO TENA SOMA HAPA LIVE!!

$
0
0

ONGEZEKO LA POSHO LIMEKWAMA;
Binafsi namshukuru sana mungu!

Taarifa rasmi ambazo nimezithibitisha kutoka katika vyanzo muhimu na vya kuaminika vya bunge, serikali na wadau wengine zinathibitisha kuwa ishu ya ongezeko la posho imekwama na KUFA KIFO CHA MENDE.

Hii ina maanisha kwamba wajumbe wa bunge maalum la katiba watalipwa shs 300,000 tu kwa siku kama ilivyokuwa hapo awali.

Narudia tena kwamba jambo hili limekwama na halitakuwepo.

Leo saa 2.00 asubuhi nilipanga kuanzisha zoezi la kukusanya SAINI za wajumbe wote wanaopinga ongezeko la posho, ni kazi ambayo ingenigharimu siku tatu kuisimamia.

Natangaza rasmi kusitisha zoezi la kukusanya saini kwa sababu ULAFI huu wa posho uliopendekezwa na baadhi ya wabunge wa CCM umekatishwa kwa maslahi ya umma.

Nawaomba watanzania wote kuelekeza mijadala yetu kwenye rasimu ya katiba na tuondoke kwenye suala la posho ambalo limefika mwisho.

Nataraji leo, Mwenyekiti wa muda wa bunge maalum atathibitisha kuwa hakuna ongezeko la posho.

Nawashukuru sana Wabunge na Wawakilishi wa Chama cha Wananchi CUF ambao walinitia moyo na kuchangia gharama za mabango maalum yenye picha za kuonesha mateso ya kina mama wanapojifungua, na lile la kuonesha watoto wa shule walivyokaa juu ya mavumbi(ambayo yangetumika katika zoezi hili).

Namshukuru sana Prof. Ibrahim Lipumba na Zitto Kabwe kwa kuniunga mkono katikati ya jambo hili. Nawashukuru baadhi ya wajumbe wa bunge la katiba ambao walikuwa tayari kusaini PETITION leo hii na waliopinga ULAFI huu.

Mungu ibariki Tanzania.
 

THE MAJANGAZ & BONGO:- HABARI ZA AIBU YA WASANII WA BONGO MUVI HUKO DODOMA KWENYE BUNGE LA KATIBA MJUZI LIVE!!

$
0
0

WAKATI mchakato wa Bunge la Katiba ukianza leo mjini Dodoma, ishu hiyo imemtia kwenye tope Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba baada ya kukwaa skendo ya ‘kutoka’ na mwigizaji Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ walipotimba mkoani humo.
Yobnesh Yusuph ‘Batuli’.
Kwa mujibu wa staa wa filamu ambaye aliachwa katika safari hiyo ya kwenda kuhamasisha sanaa itambuliwe kwenye mchakato wa katiba mpya, Mwakifwamba alimteua Batuli ili akajiachie naye Dodoma kwa sababu hakuwa na vigezo.

“Akina Monalisa (Yvone-Cherry Ngatikwa) walistahili kwa ukongwe wao kwenye fani, sasa Batuli aliingiaje? Akili za kuambiwa changanya na zako,” alisema msanii huyo.
Akizungumzia skendo hiyo, Mwakifwamba alidai kuwa ameshasingiziwa vitu vingi hivyo anajua nyuma yake kuna kundi linalomchafua kila kukicha lakini ukweli ni kwamba hakumteua Batuli kwa lengo hilo.
“Sasa kama nimemteua kwa sababu hiyo, je, akina Monalisa nao niliwateua kwa kigezo hicho?” alihoji Mwakifwamba huku akikiri kuwa ameshaisikia sana skendo hiyo.
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba.
Kwa upande wake Batuli alifunguka: “Si kweli bwana, wameshatuzushia mambo kibao. Mara kuna fedha tumekula, mara sijui nini…sasa naona wamekuja na hili la mapenzi. Wabongo tuache majungu.Katika safari ya Dodoma, mbali na Monalisa, wawili hao waliambatana na wasanii wengine wa tasnia mbalimbali wakiwemo Dude, John Kitime, P-Funk Majani na Abdul Salvador ambapo ndani ya bunge hilo linalotarajiwa kutikisa, wanawakilishwa na Paul Mtendah.

WAZIRI WA CCM ASISITIZA KODI KULIPWA TU HATA KAMA NI KWA EFD AU ANYTHING KODI ITALIPWA TU!!

$
0
0

Waziri wa fedha: Serikali haitarudi nyuma matumizi ya mashine za EFD


Leo 22/02/2014 Waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya amesema kuwa Serikli haitarudi nyuma kwenye matumizi ya mashine za kielectroniki, EFD. Aliyasema hayo katika mahafali ya chuo cha TRA.

Waziri amesema wafanyaabiasha waache visingizio vinavyotokkana na wao kutokuelewa vizuri juu ya mashine hizo, pia amesisitiza kuwa sisi walaji tunaponunua biadhaa tudai risiti.

WATANZANIA inabidi tuelewe kwamba HATUWEZI kuendelea bila kuwa na mifumo dhabiti ya KODI!
MY TAKE.
TUJIULIZE,
Hivi kweli mfumo wa kulipishana kodi kwa kukadiriwa kwa kutumia busara na utaalamu wa mkadiriaji wa TRA uko sahihi au umepitwa na wakati?. Nadhani umepitwa na wakati na kuchochea kushamiri kwa vitendo vya rushwa.
Hivi endapo mfanyabiashara ananunua kwa gharama yake na anarejeshewa pesa yake kuipitia malipo yake ya kodi, si ni kama amepewa bure?, mathematically ni sawa na kusema umetoa nne ukapata nne mwisho wa siku unakuwa umetoa sifuri.

Hivi ELIMU ndugu zetu wa TRA si wamejitahidi kuitoa ya kutosha?. Katika baadhi ya mikutano ambayo TRA wamekuwa wakiifanya na wafanyabiashara, mahudhurio ya wafanyabiashara yamekuwa ni hafifu sana kiasi cha kusikitisha, je hapo TRA watalaumiwa hawajatoa elimu ya kutosha?, je lawama hii inawatendea haki TRA?, au wangewafuata kwenye biashara zenu kuwapa elimu huko?

Matengezo ya mashine, je si ilishafahaishwa na TRA kwamza matengenezo ya mashine ni BURE walau kwa mwaka wa kwanza wa matumizi ya mashine?, na baada ya mwaka wa kwanza kupita gharama ya matengezo ya mashine endapo itaharibika italipwa na mfanyabiashara na katika kipindi ambacho mfanyabiashara analipia kodi atarejeshewa kiasi alichotengeneza mashine ile kwani kimsingi mashine hizo ni za TRA.

UONGO UNAOENEZWA, kuna wanaoeneza uongo kuwa mashine hizi zinakata asilimia 18, hiyo siyo kweli. HAZIKATI KIASI CHOCHOTE. Kimsingi ni kuwa badala ya kutumia VITABU sasa tunkwenda kidigitali unabofya na risiti inatoka. Tafuteni majedwali ya KODI kwenye ofisi za TRA. Kwa kuwasaidia tu wanaotaka kujua.

Mfanyabiashara akiuza chini ya shilingi 0 na shilingi milioni 4 hakatwi KODI. Huyu anahitaji kukua kwa kutumia senti zake zote kujikuza kibiashara.

Kati ya shilingi 4Million na 7.5Million kodi ni shilingi 100,000/= kwa mwaka.

Kati ya shilingi 7.5Million na 11.5Million kodi ni shilingi 212,000/= kwa mwaka.

Kati ya shilingi 11.5Million na 16Million kodi ni shilling 364,000/= kwa mwaka.

Kati ya shiling 16Million na 20Million kodi ni shilling 575,000/= kwa mwaka.

Kiasi kinachozidi 20M, hairuhusiwi kukadiriwa ila mfanyabiashara atatakiwa na sheria aandae audited accounts, hapa mfanyabiashara atatozwa kodi kulingana faida aliyoipata, namna hii kitu inavyofanyakazi wasiliana na hii namba ya bure ya TRA 0713800333 au wasiliana na ofisi y TRA iliyo karibu nawe.

Kama tuliweza kuhama ANALOGIA na kuingia DIGITALI tunashindwaje KUHAMA kutoka kwenye kwenye VITABU na kuhamia kwenye EFD machine kwa ajili ya kutolea risiti?

WAFANYABIASHARA TUACHE UJANJA UJANJA, TULIPE KODI!

"Lisanga Ya Banganga" THE FIRST SONG PLAYED BY DUO FRANCO MAKIADI & TABU LEY AMBAO WOTE NI MAREHEMU SASA!!

HII PICHA YA BONGO MUVI STARS STEVE NYERERE NA SANDRA YAZUA KIZAA ZAAA NA MITANDAO YA KIJAMII KUNANI HAPO???

LEO KULE MWAKA-INSTAGRAM WALIANZA TOKA ASUBUHI ONA SASA ALICHOTUPIA SUPER STAR WOLPER ANAKULA MASAJI LIVE!!

$
0
0

MAKUBWAA...Jacqueline Wolper AJIANIKA LIVE AKIFANYIWA MASAJI...!!ATUPIA PICHAZ MTANDAONI SHUKA NAYO HAPA..

MAKUBWA! staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe amejianika akifanyiwa masaji laivu.
Wolper a.k.a Gambe ‘alifanya yake’ ndani ya saluni (massage parlor) moja iliyopo maeneo ya Mwenge jijini Dar.
Mara baada ya tukio hilo huku akiwa ‘amefotolewa mapicha’ ambayo aliyatundika kwenye ukurasa wake wa Instagram, mwanadada huyo alielezea jinsi alivyohisi raha ya ajabu wakati akifanyiwa masaji.
“Asante…(akitaja jina la saluni), kwa raha niliyopata leo…, mi siyo mchoyo kwa kweli karibuni nanyi mpate afya. Nimefurahia walah,” aliandika Wolper.

SUPER STAR LULU AKANUSHA UZUSHI DHIDI YAKE NA STEVE NYERERE LIVE!!

$
0
0

OOHOOO! Elizabeth Michael ‘Lulu’ amekwaa skendo ya kudaiwa kukuwadiwa na mwigizaji mwenzake, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ kwa mwanaume anayedaiwa kutoka naye kimapenzi kwa sasa anayetajwa kwa jina moja la Johnson.
Chanzo makini kilipenyeza ‘upupu’ huo ambao umefafanuliwa na Steve Nyerere kuwa ukaribu wa Lulu na bosi huyo umetokana na kazi kwani yeye na Lulu wameingia mkataba hivyo walitegemea kusikia manenomaneno.
Lulu alipotafutwa kuhusiana na ishu hiyo, alitiririka: “Wabongo wanapenda sana kuzusha mambo, sijawahi kuwa na mwanaume anayeitwa Johnson  zaidi ya kuwa bosi wangu.”

THE MAJANGAZ & BONGO:- MWANAUME ALIPOKUTA PICHA ZA UTUPU ZA MKEWE KWENYE SIMU YA BOSI WAKE LIVE!!

$
0
0
Dalitso Muweso(35) anayeishi na mkewe bibie Madaliso Kambwiri(32),Jana alizifumania picha za mkewe huyo kwenye usb-disk(flash) ya Boss wake ofisini baada ya kutumwa kwenda kuprint documents muhimu za Boss huyo.

Chanzo chetu cha Udaku kutoka Kenya(Wambui---Fan wa Udakubiz),kinasema kuwa Wanandoa hao ambao Ndoa yao imeingia Mwaka wa Tatu hivi karibuni,walikuwa wanaishi kwa furaha na Amani kiasi kwamba Mtaa mzima walikuwa wanawaonea wivu .
 

Inasemekana kuwa ilikuwa sio jambo rahisi kwa wanafiki na wambea kuongea uongo wowote either kwa Mume au Mke,kwani wanandoa hao walikuwa Wanapendana na kuaminiana na kila Mmoja alionyesha uaminifu kwa mwenzie.

Lakini Wahenga wenye Busara zao tokea shule ya msingi walishawahi kusema kuwa "Njia ya Muongo,ni Fupi",Pamoja na Mume wake kumuamini mpaka mwisho,lakini inasemekana kuwa Mwanamke huyo alikuwa sio Mwaminifu kwa mumewe,NA chanzo cha kumsaliti Mumewe ilikuwa ni kipato kidogo alichokuwa nacho mumewe.
 

Jana Wakati mumewe akiwa kazini,akapigiwa simu na Bosi aende ofisini,alipofika Bosi akampa flash akamuomba aende akaprint important documents kwa sababu alimtuma Secretary wake akamchukulie Breakfast kwenye Mgahawa uliokuwa mbali kidogo na Ofisi hizo,Zile Documents zilikuwa zinatakiwa kutumwa haraka kwenye email na secretary alikuwa anachelewa kurudi.
 

Jamaa akachukua,akaenda kwenye Internet cafe ambayo ipo nje kidogo,ilipochomekwa flash akakuta kuna mafolder mawili,moja limeandikwa 'Secret' lingine limeandikwa 'Confidential',akasahau kuwa aliambiwa kuwa documents zipo kwenye folder la confidential,yeye akafungua lililoandikwa 'Secret' ndipo hapo alipokutana na hizi picha za mkewe.
 

Bado mpaka sasa hatujajua kilichotokea kwenye Ndoa hiyo,Mdaku wetu wambui atafuatilia kisha tutawafahamisha.
 










WAZIRI WA CCM SITA AIWEKA WAZI NI KWA NINI ANAGOMBEA KUWA BOSI WA BUNGE LA KATIBA LIVE!!

$
0
0


Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta 

Hii ni mara ya kwanza kwa Sitta ambaye alikuwa Spika wa Bunge la Tisa kuweka wazi uamuzi wake huo. Mwingine anayetajwa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa zamani na Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge.


Dodoma. Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amesema atagombea uenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba kwa sababu anaamini kuwa ana sifa za kutosha.
Hii ni mara ya kwanza kwa Sitta ambaye alikuwa Spika wa Bunge la Tisa kuweka wazi uamuzi wake huo. Mwingine anayetajwa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa zamani na Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge.
Sifa za mtu anayepaswa kuongoza Bunge hilo ni kuwa na shahada ya sheria kutoka katika chuo kinachotambulika pia kuwa na uzoefu wa kuendesha mijadala kama ya Bunge.
Akizungumza na gazeti hili jana, Sitta alisema pamoja na propaganda chafu zinazoenezwa dhidi yake, hatakata tamaa na kwamba ataendelea na msimamo wake huo ili nchi ipate Katiba bora.
“Sheria ya Mabadiliko ya Katiba imeainisha sifa za mtu anayetakiwa kuwa mwenyekiti na mimi nina sifa na nina mipango mizuri ya kuwafanya Watanzania wapate Katiba bora kama ndoto ya Rais wetu (Jakaya Kikwete) ilivyo,” alisema.
Alipoulizwa kuhusu njama za kumzuia asigombee nafasi hiyo, Sitta alisema “Haishangazi watu hao kutumia mbinu chafu… Hawana maadili, ndiyo maana wananihofia lakini sishtuki hata kidogo.”
Sitta ambaye pia ni mbunge wa Urambo Mashariki (CCM), alisema wabaya wake wamekuwa wakieneza maneno ya uongo kwamba ikiwa atakalia kiti hicho, atasimamia mpango wa Serikali tatu.
“Wanasema Sitta ataruhusu Serikali tatu, sasa nashangaa maana wajumbe ndiyo wenye mamlaka hayo… wanaeneza propaganda kuwa nina mkataba na wapinzani ndiyo maana wananiunga mkono. Wanasema mambo ya ovyo kabisa,” alisema.
Sitta alisema wapinzani kama walivyo wajumbe wengine kutoka CCM na makundi mengine, wanamuunga mkono kwa kuwa wanaamini akikalia kiti hicho ataendesha Bunge hilo kwa misingi ya uwazi na haki.
“Mimi sina mkataba na wapinzani ila wao kama watu wengine wananiunga mkono kwa sababu wanajua nitatenda haki, nina rekodi nzuri katika kuliendesha Bunge la Tisa wala hiyo haina mashaka,” alisisitiza Sitta.
Sitta na Chenge
Kumekuwa na msuguano na kampeni za chini chini kati ya kundi la Sitta na Chenge, lakini habari zilizopatikana jana kabla ya Sitta kutangaza kuwania nafasi hiyo, zilisema CCM walikuwa wakikusudia kuwaondoa makada hao, na kumpendekeza Mathias Chikawe badala yao.
Ilielezwa kuwa hatua hiyo imefikiwa kutokana na mpasuko mkubwa ndani ya chama hicho unaotokana na wapambe wa makada hao kuanza kupakana matope.
Hata hivyo Chikawe alisema hana taarifa yoyote kuhusu mpango huo. “Ahaaa! Sina taarifa hiyo, sijawahi kufikiria kushika nafasi hiyo, wewe (mwandishi) ndiyo unaniambia na nimeshtuka sana, lakini nitafuatilia,” alisema Chikawe.
Kwa upande wake, Chenge juzi alisema hana sababu ya kulumbana na watu aliowaita kuwa hawataki kuelewa na kwamba tayari CCM kilikuwa kimetoa mwelekeo wake.
Hata hivyo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, alisema chama hicho hakijatoa msimamo wa mtu kinayetaka agombee nafasi hiyo kwani hakuna kikao chochote kilichojadili suala hilo.
“Kama uamuzi unafanywa, lazima vikao vya chama vikae, lakini hadi sasa kwa uelewa wangu hakuna kikao chochote cha chama ambacho kimeketi na kuamua suala hilo,” alisema Nnauye.
Kauli ya Nnauye iliungwa mkono na ile ya Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, William Lukuvi ambaye alisema chama hakijatoa mwongozo wowote kuhusu suala hilo kwa kuwa muda wake bado.
“Chama hakijatoa mwongozo wowote ingawa tunajua watu wameanza kuumana kwa hilo, wako kama saba,” alisema Lukuvi.
Lukuvi ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), alikuwa akijibu tuhuma zilizotolewa dhidi yake kwamba ndiye anayeshawishi Sitta asiwe mmoja wa wagombea katika kinyang’anyiro hicho ili kulinda mwonekano wa Spika wa Bunge, Anna Makinda.
“Wanahofia endapo Sitta atafanikiwa kupata uenyekiti na kuendesha vizuri Bunge na Makinda akaja kuendesha Bunge la Bajeti ataonekana kupwaya sana,” kilisema chanzo chetu.
Lukuvi alikanusha kuhusika na mpango huo akisema: “Mimi nahusika vipi kwenye hilo. Kwanza kama chama hatujatoa mwongozo lakini hatuwezi kutoa mwongozo kabla Bunge halijatoa kanuni za namna ya kumpata mwenyekiti.”
Lukuvi alikiri kufahamu kuwapo kwa vita ya uenyekiti, lakini akasema yeye haoni mantiki ya kuhusishwa kwake. “Mimi najua watu wameshaanza kuumana lakini kwa nini sasa, wakati hata kanuni hazijatoka na chama hakijatoa mwongozo,” alihoji.

BREAKIN NEWZZZ:- NA HII NDIO HABARI KAMILI YA MBONGO ALIYEBAKWA MPAKA KUFA HUKO CHINA KAMA ILIVYOKUWA LIVE!!

$
0
0





AMA kweli dunia hadaa, ulimwengu shujaa! Kumeibuka mchezo mchafu, kuna Watanzania wanawachukua warembo nchini na kuwapeleka China kwa ahadi kwamba wanakwenda kufanya kazi saluni, wakifika kule wanawanyang’anya paspoti na kuwauza kwa wanaume (ukahaba), sasa yamemkuta Mbongo aitwaye Sabrina au Habiba, Ijumaa Wikienda lina mkasa wa kusikitisha.
Habari za uhakika kutoka kwa chanzo chetu nchini humo zilisema kuwa, Sabrina (24), alifariki dunia Alhamisi iliyopita kufuatia kubakwa na wanaume watano, raia wa Nigeria ambao wamo nchini humo kibiashara.
Tukio hilo lilijiri kwenye hoteli moja iliyopo kwenye Mji wa Guangzhou ambao umejaa wageni wengi, wakiwemo Watanzania.

 
SIKU YA TUKIORafiki wa karibu wa Sabrina, Saada alisema siku ya tukio, marehemu akiwa katika harakati zake za kutafuta wateja alikutana na Mnigeria mmoja ambaye walipatana kulala wote kwa usiku mzima.“Kumbe yule Mnaigeria alikuwa na wenzake wanne. Usiku walimwingilia wote kwa nguvu kwa kumbaka mpaka akapoteza maisha palepale. Ni ukatili mkubwa.
“Wale watu walipogundua Sabrina amekufa waliuchukua mwili wake na kuutupa chini kutoka ghorofa ya tano,” alisema rafiki huyo.
 
MAITI YAKUTWA HAINA FIGO, MOYOHabari zaidi zilidai kuwa mpaka juzi (Jumamosi) madaktari waliokuwa wakiuchunguza mwili wa Sabrina waligundua hauna figo na moyo, jambo linalozidi kuzua hofu juu ya muaji yake.
 
NI BIASHARA ILIYOIBUKA CHINA?Ilidaiwa kuwa nchini China imeibuka biashara ya viungo mbalimbali vya binadamu ambapo ili vipatikane ni lazima mwenye viungo hivyo auawe kwa njia yoyote.
 
SABRINA AFA, MGANDA APOTEAMtoa habari wetu alisema wakati Wabongo wakiwa kwenye maombolezo ya kifo cha Mtanzania huyo, mrembo mwingine raia wa Uganda, nchi ambayo imo ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki amepotea katika mazingira ya kutatanisha nchini humo.
Baadhi ya watu wana wasiwasi kuwa kupotea kwa msichana huyo kunahusiana na kushamiri kwa biashara ya viungo vya binadamu.
 
SABRINA ALIKWENDAJE CHINA? Mwezi Julai, mwaka jana, Sabrina alikwenda nchini humo akidanganywa na mwanamke mmoja kwamba atapata kazi kwenye saluni ya wanawake lakini baada ya kufika alijikuta akiingizwa kwenye biashara ya ukahaba bila ridhaa yake mpaka alipokutwa na mkasa huo uliopoteza maisha yake.
 
TAHADHARI KWA WAREMBO WANAOKWENDA CHINA KUFANYA KAZI SALUNIImebainika kuwa, kumeibuka wimbi la Wabongo wanaofanya ‘uwakala’ wa kuwachukua wasichana wa Kitanzania kwa kuwadanganya kwamba wanakwenda kufanya kazi za saluni nchini humo.
Mara baada ya kufika, wasichana hao hunyang’anywa paspoti ili washindwe kuondoka nchini humo na kushinikizwa kujiuza (ukahaba) huku waliowapeleka wakipokea fedha kutoka kwa wateja.
 
KUIKOMBOA PASPOTI Habari zilisema kuwa mhusika hurejeshewa paspoti yake baada ya malipo yake kwa ‘wakala’ kufikia dola za Marekani 8,000 (kama shilingi milioni 12), ndipo huachiwa ‘huru’ kuendelea na maisha yake.
Wengi wakishaachiwa hushindwa kurejea Bongo na kujikuta wakiendelea kuuza miili katika mahoteli na klabu huku wakikutana na majanga mbalimbali.
 
MASOGANGE, KAJALA NA DIDAWatanzania waishio nchini humo wamewatahadharisha mastaa wa Bongo, wakiwemo Mtangazaji wa Radio TimesFM, Khadija Shaibu ‘Dida’, msanii wa filamu Kajala Masanja na Video Queen Agnes Gerald ‘Masogange’ ambao hupenda kwenda nchini humo kwa shughuli zao, kutokubali kuwa karibu na mawakala wa kuchukua wasichana Bongo kwa kuwadanganyia kazi ya saluni kwani wanaweza kujikuta pabaya siku moja.
 
DIDAIjumaa Wikienda lilimsaka Dida siku ya Jumamosi iliyopita na kumuuliza kuhusu kuwepo kwa mawakala hao ambapo alikiri kusikia huku akisema warembo wenyewe wanapaswa kuwa macho na udanganyifu huo.
“Najua wapo Wabongo wanaofanya shughuli hiyo, si China tu hata India, unapelekwa kwa ahadi ya kazi ya saluni, ukifika hamna cha saluni wala nini? Warembo wawe makini jamani, nenda China kama una uwezo wako mwenyewe kufanya ‘shoping’ lakini si kupelekwa,” alisema Dida.
 
BALOZI WA TANZANIA-CHINA Juzi, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Balozi wa Tanzania nchini China, Luteni Jenerali Mstaafu Abdulrahman Shimbo ili azungumze lolote kuhusu tukio la Sabrina, lakini simu yake ilionekana kutokuwa hewani kwa muda mrefu.
 
GLOBAL BADO KAZINIMagazeti Pendwa ya Global Publishers yanaendelea kuifuatilia habari ya kifo cha Sabrina na yatakuwa yakiwapa wasomaji wake kadiri kitu kipya kinapopatikana
 
na  GPL

TIZAMA MISS UNIVERSE TANZANIA 2013 NAYE ALIVYOJITUPIA HUKO FACEBOOK WALLAHI BONGO NI TAMBALALAEZZZ!!

$
0
0


Miss Universe Tanzania 2013
Betty Boniface

NBA STAR ALIYEJITOA KUWA NI SHOGA SASA AKUBALIKA ZAIDI NA WACHEZAJI WA TIMU YAKE KULIKO KWINGINE KOTE SOMA ABARI YAKE HAPA LIVE!!

$
0
0
.


Jason Collins arrives at a state dinner in honor of French President Francois Hollande at the White House on Feb. …
From the moment that Jason Collins' announcement sent shockwaves through the sporting world, the questions hung in the air, unavoidable. Who's going to sign him now? Is anyone going to sign him? What kind of team would sign him? Nearly 10 months later, we have our answer.


As first reported by Yahoo Sports NBA experts Adrian Wojnarowski and Marc J. Spears, someone did sign Collins, and it was the Brooklyn Nets. Collins then made history Sunday by becoming the first openly gay man to play basketball in the NBA after checking into Brooklyn's road game against the Los Angeles Lakers.

The Nets are a team in need of an extra big body on their bench, a team led by a coach, Jason Kidd, who spent 6 1/2 years playing alongside Collins and has supported Collins' revelation since the start. It's a team with a roster chock full of veterans experienced in separating the external and extraneous from what matters on the floor. It's a team of grown-ups. It took usa while to get here, but we're here, and it's just about perfect.

Word that there might be a match between team and player began to circulate last week after the Nets season-ending foot injury, and that has since gotten even smaller by moving little-used reserve rebounder Reggie Evans to the Sacramento Kings in exchange for shooting guard Marcus Thornton.
''We're going to bring in a basketball player,'' King said, according to Brian Mahoney of The Associated Press. ''It's not about marketing or anything like that.''

Whether marketing or public perception had anything to do with Brooklyn's decision-making, it's inevitable that adding Collins will draw an immense amount of media attention, both positive and negative, to a Nets team that has significantly underperformed its nine-figure salary sheet and (admittedly misguided) preseason expectations of title contention en route to a 25-28 record that has them clinging to the eighth and final playoff spot in the Eastern Conference heading into Sunday's action. In the past — including the very recent past— many have argued that such increased attention could serve as a chaos-inducing distraction that might segment a locker room and derail the focus of a team aiming to make a playoff push.
Nets point guard Deron Williams acknowledged that a Collins signing would spark a media frenzy, but suggested that Brooklyn was precisely the sort of team equipped to handle it, according to Newsday's Rod Boone:
"I think it's definitely going to be a media circus just because of the situation," Williams said. "It'd be a historic day and so we definitely have to deal with that. But I think with the type of team that we have, veterans who have played with him before and know him, it shouldn't be a problem." [...]
"It's not him being a distraction," Williams said. "It's just the media coming along with it, because every city you go to, it's not just like you answer a question once and then it's over with. It's a recurring thing. But like I said, I don't think it would be a problem for us."
The general tenor: No "distraction" is as powerful as an idea whose time has come. From Tim Bontemps of the New York Post:
“It’s 2014,” Deron Williams said Friday when asked if the NBA was ready for an openly gay player. "Michael Sam just came out, and his teammates welcomed him, and they’re in college. It’s time for the NBA, as well.”
Williams, the tip of the Nets' spear at the point guard position, wasn't the only Net to show support. Three other established veteran voices on the Nets roster — All-Star shooting guard Joe Johnson and future Hall of Famers Kevin Garnett and Paul Pierce, all of whom have played with Collins in the past (Johnson on the Atlanta Hawks from 2009 through 2012, Garnett and Pierce with the 2012-13 Boston Celtics) — also spoke out in favor of a prospective Collins signing. More from Newsday's Boone:
"We would accept it greatly and it shouldn't be a problem, man," Joe Johnson said. "We've got a veteran group and I think everybody is pretty comfortable in their own skin. It's about what he can do to help us out there on that court. That's what it's about." [...]
"I'm sure the distractions will be just that: distractions," Kevin Garnett said. "But I don't think there will be issues. We are all men here. We all understand. We are professionals. We know how to coincide with one another, which is very important when dealing with distractions."
And more from Bontemps:
“No, I don’t think it would be too big of an issue with our team,” Pierce said. “We have enough veterans in the locker room and really phase that out and understand we have a job to do, and to try and win games.
“We’re in the stretch run of the season, and that’s what’s most important to us.”
Garnett was even more strident, saying the only thing that should matter is whether or not Collins is still able to help a team win.
“I think it’s important that anybody who has capabilities and skill level to have a chance to do something he’s great at or one of the things he’s good at,” Garnett said.
“I think it’d be biased and, in a sense racist, if you were to take that opportunity from a person.”
“If he can help our team, I’m all for it.”"It's about what he can do to help us out there on that court." If you can play, you can play. Sing it.
Support from farafield is one thing, and it's a great thing — as TrueHoop's Kevin Arnovitz wrote Sunday, having everyone "from the White House to grassroots organizations [...] honoring [your] courage [is] about as validating as an experience can get as a human being." But it's not quite the same as receiving that same sort of recognition and validation from the people with whom you'll be working every day, with whom you'll be sharing locker rooms and team flights and shootarounds and pivotal possessions and everything else that goes into being a professional athlete competing at the highest level of your sport. If we take these veterans at their word, it appears that Collins will have that when he shows up to Staples Center to join the Nets as they take on the Los Angeles Lakers on Sunday night.

When Collins came out, we wondered, as surely he must have, if he'd find a landing spot where the people around him would be willing and able to accept and welcome, and let the game be the game. With these Brooklyn Nets, it seems he has. That matters. That's massive. That's how history is helped to happen.

Four months ago, Collins' twin, fellow long-time NBA big man Jarron Collins, was left with little more than hope that his brother would find himself wearing an NBA uniform again. On Sunday, his hope becomes firm, incontrovertible reality. That must feel pretty good.
Yeah, it should, Jarron. And good on the Nets' collection of clear-eyed, professional grown-ups for being willing to make it one.

MBUNGE FEKI WA KATIBA MPYA APIGWA STOP POSHO LIVE!!

$
0
0


Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Dk Thomas Kashililah 

Akizungumza na gazeti hili jana katika Ofisi za Bunge mjini hapa, Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Dk Thomas Kashililah, alisema Bunge limechukua hatua hiyo baada ya Mweta kuwajibu kuwa fedha walizompatia alikuwa ameshazitumia.

Dodoma. Ofisi ya Bunge la Katiba, imemwandikia barua mwajiri wa Amina Mweta, ambaye alisaini posho ya Bunge hilo ili akatwe posho aliyoichukua katika mshahara wake.
Akizungumza na gazeti hili jana katika Ofisi za Bunge mjini hapa, Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Dk Thomas Kashililah, alisema Bunge limechukua hatua hiyo baada ya Mweta kuwajibu kuwa fedha walizompatia alikuwa ameshazitumia.
“Yeye (Amina Mweta), ni mwajiriwa wa Halmashauri ya Mwanga, tulichokifanya ni kumwandikia barua mwajiri wake ili akatwe katika mshahara wake,” alisema na kuongeza: “Atajua mwenyewe kama atalipa kwa kukatwa kidogo kidogo ama yote, lakini lazima ailipe posho hiyo aliyoichukua, kwa sababu alichukua na kuweka sahihi.”
Gazeti hili lilikuwa la kwanza kuripoti baada ya kutokea utata huo wa majina mawili ya wajumbe kufanana huku ikielezwa kuwa wote walikuwa wamesaini fomu za fedha za posho ya kujikimu ya Sh80,000 kwa siku kwa muda wa siku 13 unaomalizika Februari 28 mwaka huu ikiwa na maana kwamba kila mmoja alilipwa Sh1,040,000.
Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge, John Joel, awali, alipoulizwa kuhusu utata huo alisema mjumbe halali ni yule aliyetoka Songea.
Hata hivyo, alisema kinachowashangaza ni kwamba yule mwenzake wa Mwanga alipotakiwa kurudisha fedha alizopewa kimakosa alisema ameshatumia sehemu kubwa na kubakiza Sh50,000 tu.
Akizungumza na gazeti hili, Mweta kutoka Mwanga alisema alipigiwa simu na Ofisi ya Bunge Maalumu la Katiba na kupongezwa kwa kuteuliwa na Rais kuwa mjumbe. “Mimi ni personal secretary (katibu muhtasi) wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga na nilipigiwa simu na Ofisi ya Bunge wiki iliyopita nikipongezwa kwa uteuzi huo,” alisema.
Alisema alipofika na kujisajili baada ya kutoa kitambulisho chenye jina lake, alipewa kitambulisho na kisha kupewa malipo yake ya posho.
Naye Mweta kutoka Songea alisema alipigiwa simu na Katibu Mkuu wa COTWU kwamba aliteuliwa na Rais kuwa mjumbe na kutakiwa kuripoti bungeni.
Tayari Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) limeeleza kusikitishwa na utata wa watu hao wawili wenye majina yanayofanana kuwasili katika Bunge Maalumu la Katiba mjini Dodoma kwa nafasi ya ujumbe wa Bunge hilo, huku likisema halimfahamu Amina Mweta wa Kilimanjaro.
Katibu Mkuu wa Tucta, Nicholaus Mgaya mapema alikaririwa na gazeti hili akisema kuwa mazingira ya tukio hilo yamewatisha, hivyo kulazimika kumwandikia barua Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue ili kumthibitisha mjumbe wao halali.
Viewing all 32622 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>