Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

NA HAYA NDIO MATOKEO YA MCHEZO WA JANA WA LIGI MBEYA CITY NA KAGERA SUGAR LIVE!!

$
0
0

Na Faustine Ruta, Bukoba
TIMU ya Mbeya City leo imeanza msimu wa pili vyema baada ya kuifungia Kagera Sugar kwenye uwanja wao wa nyumbani kaitaba bao 1-0. Kipindi cha kwanza kilimalizika kikiwa hakuna timu iliyokuwa imeziona nyavu za mwenzake hivyo zikalazimika kwenda mapumziko zikiwa 0-0, Huku kipa wa Kagera Sugar Hannington akiwa hoi kwa kuumia mguu baada ya kuachia frii kiki na kushtuka mguu na kulazimika kutolewa nje katika kipindi hicho cha kwanza. Kipindi cha pili dakika ya 72 Mbeya City wamepata bao kupitia mchezaji wao Richard Peter aliyekuwa amevaa jezi no. 13 mgongoni.
Kikosi cha timu ya Kagera Sugar kilichoanza

Kikosi kilichoanza cha Mbeya City
Taswira ya watazamaji Kaitaba leo hii
Patashika zikiendelea uwanjani

Patashika kuutafuta mpira
Richard Peter akipongezwa na mwenzake baada ya kufunga bao na kuiwezesha Mbeya City kuwa mbele ya bao 1-0 dhidi ya wenyeji Kagera Sugar.
Ubao Wenyeji kagera Sugar 0-1 Mbeya City
Baada ya mtanange kumalizika wachezaji wote wa Mbeya City wakifanya mazoezi kama vile mtanange ndio unaanza
Kocha wa Mbeya City Juma Mwambosi akiongea na mwandishi wa TBC1 kwenye uwanja wa Kaitaba baada ya mpira kumalizika Kagera Sugar wakiwa hoi kwa kichapo cha bao 1-0.
Mashabiki wa Mbeya City nje ya uwanja usiseme angalia walivyokuwa wanatupia....kanyaga ...chinja!!

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>