Marehemu Kenneth Kidago Lyanga enzi ya uhai wake.
Mbunifu Msaidizi na Mtangazaji wa Habari za Michezo wa East Africa Radio Kenneth Kidago Lyanga amefariki dunia nyumbani kwake Mwenge Mlalakua, Jijini Dar es Salaam.Mipango ya mazishi ya Kenneth Lyanga inafanywa na familia yake. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu Kenneth Kidago Lyanga Mahala Pema Peponi, Amina.