Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

MBUNGE WA CHADEMA ATUHUMIWA KUIBA NYARAKA ZA HALAMASHAURI SOMA HAPA LIVE!!

$
0
0
MWENYEKITI wa Halmashauri ya Mji wa Babati, Mohamed Farah ameibuka na kukiri kumnyang’anya nyaraka za kikao Mbunge wa Viti Maalumu, Paulina Gekul (Chadema). Kuibuka kwa mwenyekiti huyo, kumekuja baada ya mbunge huyo kufungua mashitaka polisi akidai kuwa aliporwa fedha na kuchaniwa nguo yake akiwa ndani ya kikao.


Taarifa ya Mkurugenzi wa Halmashauri, Omari Mkombole kwa vyombo vya habari ambayo MTANZANIA Jumamosi linayo nakala yake, imemnukuu Farah akitoa ufafanuzi wa tukio hilo.

Katika taarifa hiyo, Mwenyekiti wa Halmashauri, Farah anakiri kumnyang’anya mbunge huyo kutokana na kile alichodai amekuwa na tabia ya kutoka na nyaraka nje ya vikao.

“Nilifanya hivyo kutokana na tabia yake anapeleka taarifa kwenye vyombo vya habari na mikutano ya wananchi kinyume cha kanuni namba 51 ya vikao vya ndani vya Kamati mbalimbali.

“Hata baada ya kufanya juhudi za kumshawishi arudishe, aligoma ndipo nilimnyang’anya nyaraka na kumkabidhi Mkurugenzi hapakuwa na purukushani, kupigwa wala kuchukuliwa kitu chochote,” alinukuliwa Farah katika taarifa hiyo.

Taarifa hiyo iliendelea kueleza kwamba, hata baada ya mkurugenzi huyo kutangaza kuwa wajumbe wote wasitoke na nyaraka hiyo, Gekul aliendelea kukaidi huku wengine wakitii agizo hilo.

“Wajumbe wote walitii agizo na kurudisha nyaraka baada ya kikao kumalizika, isipokuwa Gekul alikataa kurudisha na kudai anaondoka nayo na hakuna mtu atakayemzuia,” ilisema taarifa hiyo.

Ilisema baada ya kunyang’anywa nyaraka hiyo, alikimbilia polisi kumshitaki mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Babati na mkurugenzi wa mji kuwa wamemfanyia fujo, kumpora pesa na kumdhalilisha, jambo ambalo si la kweli.

“Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Babati, amesikitishwa kuwepo kwa taarifa ambazo zimepotoshwa katika vyombo vya habari.

“Anadai amepigwa na kudhalilishwa kwenye kikao cha Kamati ya Mipango Miji na Mazingira kilichofanyika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Babati, wakati si kweli,” iliendelea kusema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi, iliweka wazi kwamba kikao cha Kamati ya Mipango Miji na mazingira, baada ya kumalizika kulikuwa na nyaraka zilizotumika katika kikao hicho, ambazo hazikutakiwa kuchukuliwa na mjumbe yoyote.

“Gekul anawajibika kama kiongozi kutii kanuni za vikao, ili kulinda heshima ya halmashauri na wananchi anaowawakilisha, vitendo vya kufanya fujo katika vikao havitaijenga halmashauri hii,” ilisema taarifa hiyo ya mkurugenzi.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>