Bao la ushindi na Ivanovic
Manchester City ilikuwa imeshinda mechi zote 11 ilizokuwa imecheza nyumbani kabla ya kukutana na Chelsea.
Kadhalika hii ndiyo imekuwa mara ya kwanza Manchester City kushindwa kufunga bao katika mechi za nyumbani tangu mwaka 2010.
Bao la Chelsea lilifungwa na Branislav Ivanovic katika kipindi cha kwanza .
Kocha Pellegrini wa ManCity
Kutokana na mechi hiyo Manchester City na Chelsea zina alama sawa lakini Mancity imefunga mabao mengi.
Liverpool iko katika nambari ya nne, Everton ni ya tano ilhali Tottenham ni sita huku Manchester United ikishikilia nafasi ya saba.BBC
CHELSEA YAIKALISHA MANCHESTER CITY ETIHAD
BAO: Ivanovic akipiga shuti lililoipatia Chelsea bao pekee la ushindi dhidi ya Manchester City.
FURAHA: Ivanovic (kushoto) akishangilia baada ya kuifungia Chelsea.
THE SPECIAL ONE: Kocha wa Chelsea Jose Mourinho akifurahia ushindi wa timu yake.
HAPITI MTU: Kipa wa Chelsea, Petr Cech na Gary Cahill wakimdhibiti Alvaro Negredo wa Man City.
TIMU ya Chelsea imeibuka na pointi tatu muhimu katika Uwanja wa Etihad baada ya kuilaza Manchester City bao 1-0 kwenye mechi ya Ligi Kuu ya England usiku huu.
Bao pekee la Chelsea limewekwa kimiani na Ivanovic dakika ya 32 ya mchezo. Kwa matokeo hayo, Chelsea sasa wana pointi 53 wakiwa nafasi ya tatu huku Manchester City wakiwa nafasi ya pili na pointi 53 wakitofautiana na Chelsea kwa mabao ya kufunga na kufungwa.
Arsenal wanaendelea kubaki kileleni wakiwa na pointi 55 kibindoni baada ya kucheza michezo 24