Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

SASA WAMEPORA MPAKA KIWANJA CHA FAMILIA YA MWALIMU NYERERE THE MAFISADI SOMA HAPA LIVE!!

$
0
0

FAMILIA ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, imeporwa kiwanja ilichokuwa inamiliki na anayedaiwa kuwa mporaji ameanza ujenzi ambao unafanyika chini ya usimamizi wa walinzi wa miraba minne. Mtoa habari kutoka familia hiyo (jina limehifadhiwa), amesema kiwanja kilichoporwa kiko Msasani Beach karibu na makazi ya mjane wa Mwalimu, Mama Maria na ni namba 778.
Mtoa habari huyo ambaye alifika katika ofisi za gazeti hili, alibainisha kuwa waporaji hao wameonesha kiburi kiasi cha kukaidi agizo la Polisi la kuwataka waache kuendelea na ujenzi katika eneo hilo mpaka litakapopatiwa ufumbuzi.

Uporaji Kutokana na taarifa hizo, gazeti hili lilitembelea nyumbani kwa Mwalimu kuthibitisha taarifa hizo na kukutana na mwanafamilia mwingine, ambaye ni mkwe wa Mwalimu.
Mkwe huyo wa Mwalimu alimtaja mmoja wa wavamizi hao (jina limehifadhiwa) na amekuwa akidai kuuziwa kiwanja hicho na mtoto wa Mwalimu.
"Huyo mtoto wanayesema amewauzia hicho kiwanja anaumwa, hata kisheria haruhusiwi kuingia mkataba kwa hiyo tunarudi pale pale kuwa ni matapeli tu hawana jingine lolote," alisema.
Baada ya kuvamia kiwanja hicho, mtoa habari alisema waporaji hao wamefanya ujanja na kukigawa viwili; kimoja kina namba 778 na kingine 782, wakati awali kilikuwa na namba moja 778. Alidai hata nyaraka wanazodai kuuziana na mtoto huyo wa Mwalimu zimeghushiwa, kwa kuwa mtoto mwenyewe alipoulizwa, alikana kuuza kiwanja hicho na kuongeza kuwa hata saini inayoonekana katika nyaraka hizo si yake. Mwalimu ni nani?
Katika kuonesha kiburi cha waporaji wanaodaiwa kuwa wafanyabiashara, mtoa habari huyo alisema wamekuwa wakitamba kuwa hakuna mtu wa kuwafanya chochote huku wakihoji Mwalimu ni nani?
"Wanatamba hakuna mtu anayeweza kufanya chochote...wanafikia hatua ya kuhoji Nyerere ni nani, eti alikuwa zamani, lakini kwa sasa hana chochote. Hizi kashfa zinatukera," alisema. Alisema pamoja na kukerwa na hali hiyo, wameamua kuacha suala hilo kwa vyombo husika, ili vichukue hatua na wamemteua wakili awasaidie.
"Sisi tunashindwa kuelewa, kwa sababu anafanya vile anavyotaka. Kuna kipindi alianza kumwaga kifusi, tukaenda kwa OCD (Mkuu wa Polisi wa Wilaya), akaja akamwambia aache kuendelea kumwaga kifusi,” alisema.
Alisema pamoja na agizo hilo la OCD, mfanyabiashara huyo ameendelea kumwaga kifusi katika eneo hilo ili kuanza ujenzi na shughuli hiyo hufanyika usiku chini ya ulinzi wa mabaunsa hao.
Alibainisha kuwa mkesha wa Januari 22 mwaka huu saa 7 usiku, mtuhumiwa alifika eneo hilo na mabaunsa wapatao 30 ambao walikuwa wakirandaranda, ili kusimamia umwagaji kifusi na kusawazisha, huku mmoja wa waporaji hao (jina tunalo) akiwa ameshikilia bastola.
Wakili wa familia hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Banzi, alipozungumza na gazeti hili, alisema alipata taarifa za uvamizi wa Jumanne usiku lakini hajachukua hatua za kisheria.
Alisema alichelea kuchukua hatua za kisheria, kwa kuwa alikuwa na ahadi ya kukutana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana, hivyo alikuwa akisubiri aone suala hilo litakapofikia na kama ikishindikana, achukue hatua zaidi.
"Niko na familia kwa karibu katika suala hili, haya ni mambo ya kusikitisha hata kibinadamu, haiwezekani familia ya muasisi wa Taifa hili inafanyiwa mambo kama haya," alisema Banzi.
DC akiri, ashituka Rugimbana alipoulizwa kuhusu suala hilo, alikiri kufikishwa ofisini kwake na tayari ameanza kulishughulikia kwa kuamuru Manispaa ya Kinondoni kumpelekea nyaraka zote zinazohusu kiwanja hicho.
"Watu wa Manispaa wameniomba niwape muda ili wafuatilie suala hilo huko Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, lakini tayari tumekutana na upande wa walalamikaji na sasa tunasubiri kukutana na upande unaolalamikiwa," alisema Rugimbana.
Alisema wanachotaka kujiridhisha, ni kama kweli huyo mtu ameuziwa kiwanja hicho na mtoto huyo. "Kwa kweli mambo yaliyoko pale ni ya kisheria zaidi ndiyo maana nataka kutumia vyombo vyote ili tujiridhishe."
Alipoulizwa kama watu hao wanaendelea na ujenzi huo, Rugimbana alisema kupitia Polisi Mkoa wa Kinondoni, wamemwamuru mdaiwa huyo asimamishe ujenzi hadi suala hilo litakapopata ufumbuzi.
"Hilo la kuendelea na ujenzi sina taarifa nalo, kwa kuwa pamoja na mtu huyo kudai eneo hilo ni lake, lakini tumemsimamisha ujenzi ... hiyo haraka ya kujenga inatoka wapi?” alihoji Rugimbana na kusisitiza kuwa atafuatilia kuona kama kweli ujenzi huo unaendelea.
Alisema lengo la kumsimamisha mtuhumiwa ni kutoa fursa kwa Manispaa kutafuta na kuwasilisha kwake vielelezo vyote vya eneo hilo. Alisema atatoa ufafanuzi zaidi suala hilo litakapopatiwa ufumbuzi na ofisi yake.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>