- Wakati tukiadhimisha siku ya Ukimwi Duniani hapo Desemba 2, lazima jamii ijue kuwa , Ukimwi si kifo bali walioathirika wanaweza kuishi kama watu wengine.
Jumapili hii ya Desemba Mosi, Tanzania inaungana na nchi nyingine duniani katika kuadhimisha Siku ya Ukimwi, ambayo pamoja na mambo mengine hutumika kuwatambua wale wote waliopoteza maisha kwa ugonjwa huo na kutathmini juhudi za nchi husika katika kupambana na Ukimwi.
Kulingana na taarifa za Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) Ukimwi umesababisha vifo vya watu milioni 25 na wengine 35.3 walikuwa wakiugua ugonjwa huo mwaka 2012, huku sababu kuu za maambukizi ikiwa ni ngono isiyo salama, maambukizi toka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa kuzaliwa au kunyonyesha na kuongezewa damu iliyokuwa na vijidudu vya ugonjwa huo.
Hapa Tanzania maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) ni ya kiwango cha juu miongoni mwa wanawake asilimia 6.6 kuliko wanaume 5.6 katika maeneo ya mijini na vijijini. Wakazi wa mijini ni mara mbili zaidi ya wakazi wa vijijini. Ingawa Lucy Lawrance ni mmoja wa waathirika wa VVU lakini ukimwangalia kwa haraka huwezi kufahamu ukweli wa afya yake. Ni mchangamfu, ,mkarimu na ni mwepesi kuzungumza naye hata kwa mtu asiyemfahamu .
Hana hofu ya kueleza ukweli kuwa anaishi na VVU tena kwa muda wa miaka 11 sasa. Kwake yeye kuwa na virusi si mwisho wa maisha bali ni mwanzo wa maisha mapya ya kujilinda na kujithamini. Anasema aligundua hali yake mwaka 2002 baada ya kuamua kupima kwa hiari kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya mara kwa mara. Lucy anasema kwa wakati huo uelewa wa watu juu ya ugonjwa huo ulikuwa mdogo, hivyo pindi tu jamii ilipofahamu kuwa ameathirika alianza kunyapaliwa na kutengwa,hata na wale jamaa zake wa karibu.
“Kwa kweli kwa kipindi kile hali haikuwa nzuri, tayari nilikuwa naumwa na jamii haikunielewa nilijiona mpweke”alisema.
Lucy anasema siri kubwa ya yeye kuwa na afya nzuri na kuendelea kuendesha maisha yake hadi leo ni hatua yake ya kujikubali kuwa ana tatizo na kuamua kuchukua hatua. “Baada ya kupimwa nilishauriwa nianze kutumia dawa za kufubaza makali ya virusi vya ukimwi(ARV’S) mara moja,na kwa kuwa wakati huo mpango wa kugawa dawa hizo bila malipo haukuwepo nilikuwa nanunua”alisema.
Anaongeza “Nashukuru serikali ilivyoanzisha mpango wa kugawa dawa hizi bure, mi nilijikubali mapema na walipoanza tu,mi nilikuwa wa kwanza kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kliniki”
Lucy kwa sasa ni mjasiriamali wa kutengeneza bidhaa za mikono kama batiki, vikoi, sabuni za kufanyia usafi akishirikiana na wanachama wenzake wanaoishi na VVU wa Twangoma .Kazi hiyo inamuwezesha kumudu maisha yake na familia yake yenye mtoto moja na wajukuu watatu,japo anakiri kikundi chao kinakabiliwa na changamoto ya masoko
“Sasa hali ya unyanyapaa imebadilika,watu wengi wanaufahamu kuhusu virusi vya ukimwi na ukimwi kwa ujumla na hata waathirika wenyewe wengi wameikubali hali yao na wamekuwa wawazi,hiin nadhani imechangia kwa kiasi kikubwa kupunguza kasi ya maambukizi mapya”. Anasema kuwa na VVU haiondoi hali ya ubinadamu wa mtu,hivyo anawataka wale wachache ambao bado wana Imani potofu, kuwaona waathirika ni binadamu kamili ambao wana mchango katika shughuli za maendeleoa ikiwemo haki ya kuajiriwa.
“Tukiwezeshwa tunaweza,kuathirika haimaanishi kuwa ombaomba,tunahitaji ushirikiano wa wanajamii wote katika kupambana na janga hili”
Hali ya Ukimwi hapa nchini
Hali ya maambukizi mapya katika maeneo ya mijini bado ni kubwa na kwa mujibu wa takwimu za 2011/12 kutoka Taasisi ya Taifa ya Takwimu(NBS) hali ya maambukizi ilikuwa wastani wa asilimia5.7 kwa nchi nzima kwa mwaka na mijini ni 7.2 na 4.3 kwa maeneo ya vijinini. Mkoa wa Njombe ndio unaongoza kwa kuwa na maambukizi makubwa ya Ukimwi kwa asilimia 14.8 ikifuatiwa na Iringa kwa asilimia 9.1. Mkoa wa Mbeya una asilimia tisa ukifuatiwa na Ruvuma (7.2), Shinyanga (7.4), Dar es Salaam (6.9) Rukwa (6.2), Katavi (5.9), Pwani (5.9),Tabora (5.1), Kagera (4.8) na Geita (4.7) na wa mwisho ukiwa Zanzibar yenye maambukizi chini ya asilimia moja.