London, England. Waziri Mkuu, David Cameron amebatilisha uamuzi wa Wizara ya Mambo ya Ndani na kuamuru uongozi wake ufikirie upya wazo la kuruhusu baa kufunguliwa mapema kwa biashara ya pombe wakati wa mechi ya Kombe la Dunia dhidi ya Italia, Juni 14 mwaka huu.
Uamuzi wa Cameroon ni baada ya wamiliki wa baa kunyimwa kibali cha kubadili muda wa kufungua biashara zao katika mchezo huo unaotarajiwa kuanza saa 5:00 asubuhi.
Watu walio karibu na ofisi ya Cameroon wameeleza kuwa kiongozi huyo ameamuru pande zote zinazohusika wakiwamo wamiliki wa baa, polisi na mamlaka za miji wakae pamoja ili kuhakikisha baa zinafunguliwa wakati wa mchezo huo dhidi ya Italia.