Wakati wa mechi ya jana Jumamosi usiku ambapo klabu ya Ac Milan ilikuwa inamenyena na Napoli FC , Mshambuliaji asiyehishiwa vituko anayechezea AC Millan, Mario Balotelli alioneana akilia na kujaribu kuficha hali hiyo ambapo hapo baadae ilimzidia na kujikuta akimwaga machozi.
Ikiwa zimebakia takribani dakika 15 kwa mchezo kuweza kumalizika, Balotelli aliyekuwa ametolewa muda huo alionekana akiwa benchi akilia licha ya kuficha uso wake kwa kutumia jacket, ila baadae alikuja konekana wazi akitoa machozi huku sababu zikitajwa kuwa ni kauli za kibaguzi zilizokuwa zinatolewa na mashabiki wa Napoli.
Tazama kipande cha VIDEO kinachomuonyesha mchezaji huyo akimwaga machozi baada ya kutolewa
http://www.youtube.com/watch?v=SBv-nFecFBU