Jumapili ya jana ilikua jumapili mbaya sana kwa msanii Diamond kwani ni kama vile karibu watu wote waliojiunga instagram walimuona mtu mbaya kwake. Ishu ilianza ivi, kupitia akaunti moja huko Instagram inayotumia jina la TeamKiba iliandika ujumbe unaosemekana umeandikwa na Diammond ukisema "Unajua kua kuna watu hawataki kabisa kukubali kua mimi ni zaidi yao kuanzia mziki wangu mpaka maisha yangu, mtu anaulizwa twitter hivi mkiamua kufanya nyimbo na Diamond hamuoni kwamba itapendeza sanaa. Et never eve haiwezi kutokea mimi kuimba na Diamond, badala angekubali apate kick nimrudishe katika mziki analeta dharau wakati anipati kimziki wala kipesa. Muziki wake hauna tena soko nasikia sasa hivi kajiunga na taasisi ya mkopo inaitwa FAIDIKA NA PRIDE kakopeshwa kujenga nyumba. Sitaki kua mnafiki ni Ali Kiba"
Mwandishi wetu aliendelea kufatilia picha linaendaje na baada ya mda mfupi akaunti hiyo iliendelea kupost ujumbe mwingine kwa njia ya picha unaodaiwa kua umetolewa katika page ya Rafiki mkubwa wa AliKiba anaefahamika kwa jina la Bonge la Nyau ukisema "Hivi huyo msanii Domo Diamond anamtaka kitu gani msanii Ali kiba? Tokea juzi amekua akimzungumzia katika media kwa wale mliofatilia katika interview yake baada ya kusamehewa na kituo cha chanel ten aliropoka maneno haya kuhusu Ali Kiba kujiunga Pride akakopeshwa ndio tatizo? Kuna matajiri kibao humu mjini wana maisha mazuri kwa ajili ya mikopo. Zote chuki Diamond kama na wewe unataka mikopo si ukajiunge?? Sio kumpiga majungu mwenzio watu kibao wamejiunga na mikopo washapata inawasaidia. Kama na wewe unataka tena usisusumbuke bofya hapa http://pri*****tanzania.wapka.mobi (tumeficha adress hiyo kwa sababu ni ya matapeli) utapatiwa mkopo na sio kumponda mwenzio.
Sasa movie linaanza hapaaaa, kupitia akaunti ya Bonge la nyau instagram, Bongo la nyau alikana kuandika ujumbe huo hapo juu na hichi ndo alichokisema " Jaman haya mambo yanayoendelea mm yanazidi kunisangaza cz napigowa simu sana na kutumiwa msg kwamba nimepost msg ya kumponda diamond kwa kusema alimponda ali kiba before... dah kweli nishai inshu iko iv iyo account hapo juu ilikuwa yangu miezi mitatu iliyopita bt kuna matapeli wa pride walinizidi ujanja wakai haki na kuchange password mpaka email ikawa chini yao wananisumbua sana cz wanapokea deal zangu zote wanawatapeli watu, watu wakijua wanawasiliana na bonge la nyau nshapokea cm ya kulaumiwa sana mpaka kutaka kupelekwa police kwaajiri ya matapeli hao cz iyo account ilikuwa kuwa kubwa sana na ina fans zangu wengi wanaojua kuwa ni mm uyo bt sio ivyo leo wamekuja na utapeli mwingine wa kuwachonganisha diamond na ali kiba ili kutangaza mambo yao ya pride sio poa kabisa cz wananiharibia mm naonekana naingilia mambo yasiyonihusu kabisa siwezi kukaa kuponda msanii mwenzangu yoyote wala kumuongelea kwa mabaya..... iyo sio peg yangu na siitumii so kama utamuitaji bonge la nyau hapatikani kwa page iyo ntwawapostia page yangu nnayatumia, hao ni matapeli wa pride wanaowaibia watu cz hata ukisoma story vizuri wameingia mambo ya kujengewa nyumba na pride akajidai eti mbona na mm bonge la nyau nimejenga kwa mkopa wa pride no no no no me sijajenga kwa pride na still niko kwa mama yangu ni uzushi tuu wa kutaka pride i kik kwa kupitia majina ya wasanii.."
Baada ya uchunguzi wetu uliofanya na mwandishi wetu tuligundua kweli kua akaunti ya Bonge la nyau ipo hacked na ndo ilitumiwa na matapeli kuchochea bifu hilo hapo juu.
Utapeli uliokua ukitumika katika akaunti feki kwa kutumia wasanii majina ya wasanii mbalimbalindo uliotumika na hapa katika bifu hili la Ali Kiba na Diamond. Matapeli hawa hujifanya wanatoa mikopo ya hadi zaidi ya milioni 20 kwa kujisajili kwa sh 80,000 tu. Sasa ukijidanganya ukatuma hiyo hela jua kua ndo umeshatapeliwa na hela yako haitarudi na hata ukiwapigia kwa namba uliyowatumia hela hutawapata.
Ukweli ni kwamba hakuna mikopo inayotolea mtandaoni bila ya dhamana na bila ya kuandikishiana mikataba sasa chunga sana usije ukaibiwa. Mwandishi wetu ataendelea kuwaletea habari zaidi kuusu bifu il na tunapanga kuwatafuta wasanii Diaamond na