Hii ni show aliyofanya msanii Basket Mouth kutoka Nigeria, jamaa ni mkali sana wa kuchekesha. Tiketi zilianza kuuzwa wiki moja kabla na zilishambuliwa kama utituli. Maajabu ya show hii ni kua mwanzo ilitarajiwa kua show hiyo ingezuliwa na wanigeria tu lakini siku ya show walijichanganya hadi wasio wanigeria.
Team nzima ya Bongoclan ikajiuliza je wachekeshaji wa Bongo wanashindwa kufanya kama jamaa huyu??? Kwa Bongo sijawahi kusikia kwamba Masanja, Joti, Kiwewe na wachekeshaji wengine wameandaa show Mlimani City au sehemu yoyote ile na wakatoza pesa jambo ambalo linaweza kuwapatia mshiko mrefu. Namalizia kwa kuwapa ushauri wachekeshaji wengine kua WAKAMATE FURSA.