Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

GAZETI LA MWANANCHI LATAKA MBUNGE ALIYEFOJI KUINGIA NA MKEWE BUNGE LA KATIBA AONDOLEWE MARA MOJA!!

$
0
0

Mwenyekiti wa Chama cha National League for Democracy (NLD), Dk Emannuel Makaidi akichangia jambo kwenye kongamano siku za hivi karibuni 

  • Tanzania imekuwa taifa la ajabu na masikitiko yetu ni kwamba mporomoko wa maadili katika jamii yetu umeziba mitima na dhamira za viongozi wetu na jamii nzima kwa jumla kiasi cha kuyaona matendo hayo kama mambo ya kawaida.

Uzoefu wetu wa
muda mrefu umetuonyesha pasipo shaka kwamba mambo mengi yanayotendeka Tanzania hayawezi kutendeka katika nchi nyingine.
Tanzania imekuwa taifa la ajabu na masikitiko yetu ni kwamba mporomoko wa maadili katika jamii yetu umeziba mitima na dhamira za viongozi wetu na jamii nzima kwa jumla kiasi cha kuyaona matendo hayo kama mambo ya kawaida.
Tunayo mifano ya matukio lukuki ya ajabu na ya kushtusha yaliyowahi kutokea hapa nchini lakini yakaonekana kama ya kawaida.
Fikiria wafanyabiashara walioiba mabilioni ya fedha za Epa ambao muda mfupi kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2005 walikwenda Benki Kuu ya Tanzania (BoT) wakati wa siku za mapumziko na kukwapua mabilioni hayo kwa njia za udanganyifu. Fikiria wezi hao walivyoahidiwa kwamba iwapo wangezirudisha wasingechukuliwa hatua yoyote.
Ebu fikiria nchi ambayo kiongozi wake anakwenda ughaibuni na kutangaza kuwapo kwa majangili mapapa 40 na kusema kiongozi wao yuko mikoa ya Kaskazini, badala ya kusema hayo akiwa nchini, ikiwa ni pamoja na kuyakamata majangili hayo na kuyachukulia hatua.
Ebu fikiria matukio haya mawili ambapo Waziri Mkuu anatamka bungeni kwamba ni sawa tu kwa Jeshi la Polisi kuwapiga wananchi ‘wakorofi’, huku mkuu wa nchi akikiagiza chama chake cha siasa ambacho yeye ni mwenyekiti kuwapiga wapinzani anaodai wanafanya vurugu dhidi ya wafuasi wa chama chake. Ni nchi gani ambayo viongozi wake wakuu wanaweza kutoa amri hizo za hatari?
Tumesema yote hayo kutokana na kitendo cha ajabu na aibu kilichofanywa na Mwenyekiti wa Chama cha National League for Democracy (NLD), Dk Emannuel Makaidi cha kufanya ulaghai na kujiwezesha yeye na mkewe kuteuliwa kuingia katika Bunge la Katiba.
 Katika utetezi wake, ametoa hoja za kuchefua na kughadhabisha kuwa, kwa vile mke wake naye ni mwanachama wa chama hicho alikuwa na haki ya kuteuliwa kama ilivyo kwa Rais Kikwete na mke wake ambao wote ni wajumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM.
Tunasema uteuzi huo haukubaliki hata kidogo kutokana na kukiuka taratibu zilizowekwa kisheria kwamba vyama vya siasa lazima viwe na sura ya Muungano katika mfumo na uendeshaji wake.
Ni ujasiri na uthubutu wa kiwango cha juu kujiteua yeye na mkewe kama vile NLD ni mali ya kifamilia. Kudai kwamba aliteua majina ya wanachama wanne na Rais akamchagua yeye na mkewe ni uongo wa kupitiliza.
Hii inaonyesha kwamba zilikuwapo mbinu chafu katika mchakato wa uteuzi huo, vinginevyo wanachama wa Zanzibar wangenyimwa vipi uwakilishi? Hatua ya chama hicho upande wa Zanzibar ya kumtaka Rais Kikwete atengue uteuzi wa Dk Makaidi na mkewe lazima iungwe mkono.
Tatizo hapa ni hatua ya Serikali kuendelea kuvibeba kwa sababu za kisiasa vyama vya siasa vilivyokufa siku nyingi. Ukweli ni kwamba NLD na vyama vingine vingi ambavyo kwa mujibu wa sheria ya vyama ya 1992 vinapaswa kufutiwa usajili wa kudumu bado vinatambuliwa kiasi cha viongozi wake kuingizwa katika Bunge Maalumu la Katiba bila kuwa na sifa stahiki.
 Hivyo, wananchi wawe tayari kushuhudia vitimbi vya viongozi wa vyama hivyo ndani ya Bunge. Ndiyo maana tunasema mambo mengi yanayofanyika Tanzania hayawezi kufanyika katika nchi nyingine.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>