Waziri wa fedha: Serikali haitarudi nyuma matumizi ya mashine za EFD
MY TAKE.Leo 22/02/2014 Waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya amesema kuwa Serikli haitarudi nyuma kwenye matumizi ya mashine za kielectroniki, EFD. Aliyasema hayo katika mahafali ya chuo cha TRA.
Waziri amesema wafanyaabiasha waache visingizio vinavyotokkana na wao kutokuelewa vizuri juu ya mashine hizo, pia amesisitiza kuwa sisi walaji tunaponunua biadhaa tudai risiti.
WATANZANIA inabidi tuelewe kwamba HATUWEZI kuendelea bila kuwa na mifumo dhabiti ya KODI!
TUJIULIZE,
Hivi kweli mfumo wa kulipishana kodi kwa kukadiriwa kwa kutumia busara na utaalamu wa mkadiriaji wa TRA uko sahihi au umepitwa na wakati?. Nadhani umepitwa na wakati na kuchochea kushamiri kwa vitendo vya rushwa.
Hivi endapo mfanyabiashara ananunua kwa gharama yake na anarejeshewa pesa yake kuipitia malipo yake ya kodi, si ni kama amepewa bure?, mathematically ni sawa na kusema umetoa nne ukapata nne mwisho wa siku unakuwa umetoa sifuri.
Hivi ELIMU ndugu zetu wa TRA si wamejitahidi kuitoa ya kutosha?. Katika baadhi ya mikutano ambayo TRA wamekuwa wakiifanya na wafanyabiashara, mahudhurio ya wafanyabiashara yamekuwa ni hafifu sana kiasi cha kusikitisha, je hapo TRA watalaumiwa hawajatoa elimu ya kutosha?, je lawama hii inawatendea haki TRA?, au wangewafuata kwenye biashara zenu kuwapa elimu huko?
Matengezo ya mashine, je si ilishafahaishwa na TRA kwamza matengenezo ya mashine ni BURE walau kwa mwaka wa kwanza wa matumizi ya mashine?, na baada ya mwaka wa kwanza kupita gharama ya matengezo ya mashine endapo itaharibika italipwa na mfanyabiashara na katika kipindi ambacho mfanyabiashara analipia kodi atarejeshewa kiasi alichotengeneza mashine ile kwani kimsingi mashine hizo ni za TRA.
UONGO UNAOENEZWA, kuna wanaoeneza uongo kuwa mashine hizi zinakata asilimia 18, hiyo siyo kweli. HAZIKATI KIASI CHOCHOTE. Kimsingi ni kuwa badala ya kutumia VITABU sasa tunkwenda kidigitali unabofya na risiti inatoka. Tafuteni majedwali ya KODI kwenye ofisi za TRA. Kwa kuwasaidia tu wanaotaka kujua.
Mfanyabiashara akiuza chini ya shilingi 0 na shilingi milioni 4 hakatwi KODI. Huyu anahitaji kukua kwa kutumia senti zake zote kujikuza kibiashara.
Kati ya shilingi 4Million na 7.5Million kodi ni shilingi 100,000/= kwa mwaka.
Kati ya shilingi 7.5Million na 11.5Million kodi ni shilingi 212,000/= kwa mwaka.
Kati ya shilingi 11.5Million na 16Million kodi ni shilling 364,000/= kwa mwaka.
Kati ya shiling 16Million na 20Million kodi ni shilling 575,000/= kwa mwaka.
Kiasi kinachozidi 20M, hairuhusiwi kukadiriwa ila mfanyabiashara atatakiwa na sheria aandae audited accounts, hapa mfanyabiashara atatozwa kodi kulingana faida aliyoipata, namna hii kitu inavyofanyakazi wasiliana na hii namba ya bure ya TRA 0713800333 au wasiliana na ofisi y TRA iliyo karibu nawe.
Kama tuliweza kuhama ANALOGIA na kuingia DIGITALI tunashindwaje KUHAMA kutoka kwenye kwenye VITABU na kuhamia kwenye EFD machine kwa ajili ya kutolea risiti?
WAFANYABIASHARA TUACHE UJANJA UJANJA, TULIPE KODI!