Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

BAADA YA ISHU YA POSHO KUZIMWA SASA BUNGE LA KATIBA DODOMA NI KIZAA ZAAA CHA NGUO ZA WAHESHIMIWA WAPYA ONA HAPA LIVE!!

$
0
0


Mfanyabiashara wa nguo za mitumba katika soko la Sabasaba mjini Dodoma, Mikidadi Kivina, maarufu kwa jina la ‘Micky’, akipanga nguo kwa ajili ya kuziuza kwa wateja wake walio wengi wakiwa ni wageni wanaohitaji nguo nadhifu kwa ajili ya kuhudhuria vikao vya Bunge la Katiba. Kawaida huuza suruali moja kwa Sh12,000 na shati kwa Sh8,000. Picha na Emmanuel Herman 


Mwananchi juzi lilishuhudia baadhi ya wajumbe hao wakiwa wamevalia suruali za `jeans’, kaptula na vipedo wakiruhusiwa kuingia ndani, huku wageni wengine wakikataliwa kuingia na walinzi haohao.

Wakati kanuni za uvaaji wa wajumbe wa Bunge la Katiba zikiandaliwa, mavazi kwa wageni na watumishi bado ni kizungumkuti baada walinzi kuwaruhusu waliovaa suruali aina ya `jeans’, kaptula na vipedo huku wengine wakizuiwa kuingia na nguo hizo.
Mwananchi juzi lilishuhudia baadhi ya wajumbe hao wakiwa wamevalia suruali za `jeans’, kaptula na vipedo wakiruhusiwa kuingia ndani, huku wageni wengine wakikataliwa kuingia na walinzi haohao.
“Unaruhusiwa kuingia lakini hiyo nguo uliyovaa, tumeambiwa tusiruhusu kuingia ndani ya Bunge hadi litakapomalizika,” alisikika askari mmoja wa Bunge akimwambia mmoja wa waandishi aliyekuwa amevaa suruali ya `jeans’.
Hata hivyo, kwenye vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano, siku za mwisho wa wiki na sikukuu, watu wamekuwa wakiruhusiwa kuingia ndani ya viwanja hivyo wakiwa wamevalia mavazi yasiyo rasmi bila bugudha za walinzi.
Hali hiyo ilimfanya mwandishi kurejea nyumbani kwenda kubadilisha nguo baada ya walinzi hao kukataa kumruhusu kuingia ndani ya viwanja hivyo. Hata hivyo katika viunga vya Bunge, Mwananchi lilishuhudia baadhi ya wajumbe, watumishi na wageni wakiwa wamevalia suruali za ‘jeans’, vipedo na kaptula.
Tangu kuanza kwa Bunge hili, wajumbe wamekuwa wakivaa mavazi yasiyo rasmi zikiwemo fulana, viatu vya wazi, suruali za `jeans’ na mavazi ya kiasili.
Kanuni ya mavazi iliyoandaliwa inapendekeza wajumbe kuvaa mavazi nadhifu na yenye kuhifadhi heshima na yasiwe na alama au rangi inayoashiria chama chochote cha siasa.
Hayo yamo katika kanuni ya 107(1) ya rasimu za kanuni za uendeshaji wa Bunge Maalum, zinazopendekezwa zitajadiliwa na wajumbe wa bunge hilo kuanzia keshokutwa.
Kanuni hiyo inapendekeza mjumbe yeyote anayeingia katika ukumbi wa Bunge au ukumbi wowote ambao kikao cha kamati kinafanyika, kuvaa mavazi yanayohifadhi heshima ya Bunge na utamaduni wa nchi.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>