Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

POSHO YA WABUNGE WAPYA YAFA KIFO CHA MENDE BAADA YA MTATIRO WA CUF KULETA KIZAA ZAA CHA KUKUSANYA SAINI ZA KUPINGA LIVE!!

$
0
0


  • Tangu kuanza kwa Bunge Maalum la Katiba, kumekuwa na hoja mbalimbali za posho.

Dodoma. Mjadala wa nyongeza ya posho kwa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, sasa umechukua sura mpya baada ya mmoja wa wajumbe hao, Julius Mtatiro kuanza kukusanya saini za wajumbe wote wanaopinga nyongeza hiyo na kumwandikia barua Rais Jakaya Kikwete, kumuomba asiongeze kiasi chochote cha fedha.


Akizungumza na gazeti hili mjini hapa, Mtatiro alisema ataanza leo. Saini hizo atakuwa akizikusanya wakati wajumbe wa bunge hilo, watakapokuwa mapumziko.
Tangu kuanza kwa mkutano wa bunge hilo Februari 18 mwaka huu, baadhi ya wajumbe wake wamekuwa wakishinikiza nyongeza ya posho wanazolipwa ambazo ni Sh300,000 kwa siku.
Wajumbe hao wanadai kuwa kiasi hicho cha fedha ni kidogo.

“Baadhi ya wajumbe wa Bunge la Katiba hatuko tayari kuharibu sifa yetu kwa kushinikiza kulipwa posho kubwa. Kwa kuwa Rais Kikwete ndiye aliyetuteua, sisi tutakusanya saini na kuziwasilisha kwake tukimuomba asiridhie nyongeza yoyote,” alisema Mtatiro na kuongeza;
“Rais ndiye mwenye mamlaka ya kukubali au kukataa nyongeza hiyo. Kwa mujibu wa kifungu cha 29(2) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011 (toleo la mwaka 2014), Rais Kikwete anayo mamlaka ya kuzuia njama zozote za kuongeza posho.”
Alisema wajumbe wa bunge hilo ni wawakilishi wa wananchi na kwa msingi huo, lazima wasimamie changamoto mbalimbali zinazolikumba bunge hilo kwa maelezo kuwa fedha wanazolipwa zinatokana na kodi ya wananchi.

“Tunahitaji kuzungumza na kutenda wakati huohuo, hoja hii ina hatari nyingi, hatuwezi kukubali kuharibu sifa tulizonazo katika jamii kwa sababu ya watu wachache wenye ubinafsi, “ alisema.
Aliongeza kuwa siyo haki kwa wajumbe wa bunge hilo kutaka walipwe posho ya Sh700,000 kwa siku wakati walimu na watumishi wengine wa Serikali wanalipwa chini ya Sh300,000 kwa mwezi.
“Wapo walimu hapa Dodoma wanalipwa chini ya Sh300,000 lakini wanaishi vizuri tu. Sasa leo hii wanaibuka wajumbe wa Bunge la Katiba na kutaka walipwe Sh700,000 kwa siku. Hii aingii akilini hata kidogo” alisema Mtatiro.

Mtatiro ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) alisema ameibua hoja hiyo na kamwe hatarudi nyuma. “Siyo kama natafuta umaarufu. Lengo langu ni kupigania maslahi ya walio wengi” alisema. Sakata la nyongeza ya posho lilizua mjadala mkali katika Bunge hilo na kusababisha Mwenyekiti wake wa muda, Pandu Ameir Kificho kuunda kamati ya watu sita kwa ajili ya kupitia maombi hayo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>