Na Walter Mguluchuma,Mpanda Katavi
Mtu mmoja alitambulika kwa jina la Richald Clavery 35 Mkazi wa Kijiji cha Ikola Tarafa ya Karema Wilaya ya Mpanda anashikiliwa na jeshi la Polisi baada ya kukutwa akifukua kaburi la marehemu aliyefahamika kwa jina la Tabu Omera
Kwa mujibu wa kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Francis Maro tukio hilo lilitokea hapo Februari 22 majira ya saa nne usiku kijijini hapo nyumbani kwa Lenada Sakafu ambae alikuwa ni dada wa marehemu huyo
Siku hiyo ya tukio Lenada Sakafu alikuwa nyumbani kwake pamoja na majirani na ndugu na jamaa zake wakiomboleza msiba wa mdogo wake marehemu Tabu Omera aliyekuwa amefariki Dunia siku tatu kabla ya tukio hilo kutokana na kushindwa kujifungua nakuzikwa nyumbani kwenye eneo la nyumba ya Lenada
Alifafanua kuwa mtoto wa Lenada aitwaye Brandina alitoka nje ya nyumba kwa lengo la kwenda chooni kujisaidia ndipo aliposhituka kuona mtu akiwa anafukua kaburi la marehemu mama yake mdogo
Alisema hari hiyo ilimfanya Binti huyo arudi ndani ya nyumba na kutoa taarifa kwa mama yake pamoja na majirani na ndugu waliokuwa ndani ya nyumba hiyo
Watu waliokuwa msibani hapo walishitushwa na taarifa hiyo nakulazimika kutoka nje ya nyumba na waliweza kumkuta Richard Clavery akiwa anafukua kaburi hilo la marehemu Tabu huku akiwa uchi akiwa amevua ngu zake zote na kuzitundika kwenye msalaba wa kaburi hilo
Kaimu kamanda Francis Maro alisema baada ya watu hao kumuuliza anafanyanini hapo ghafla mtuhumiwa alishituka na akajifanya kupandisha mashetani hata hivyo watu hao waliokuwa msibani hawakujali walimkamata
Alisema mtuhumiwa anatajiwa kufikishwa mahakamani ili aweze kujibu shitaka la kufanya kosa la kufanya vitendo vya kishirikina.
via wajanja wa town