Mkasa wa Ostaz Juma na PNC linaweza kutajwa kuwa moja kati ya matukio yaliyozungumzwa zaidi kwa wiki iliyopitwa kupitia mitandao ya kijamii na baadae kuwa topic kwenye radio na television wiki iliyopita.
Ingawa wasanii wengi walilaani kitendo hicho, rapper wa Manzese, Nay wa Mitego yeye aliiambia Bongo Dot Home ya 100.5 Times Fm kuwa kitendo alichokifanya Ostaz Juma kupost picha zinazomuoenesha PNC akimpigia magoti, kwa upande wake amemkosea yeye hata kuliko PNC mwenyewe.
“kumpigia mtu magoti kwa ajili ya kuomba msamaha ni sahihi. Lakini kuna upigiaji wa magoti mwingine ambao baadae unaweza kuonesha picha mbaya kuwa umedhamilia kumdhalilisha. Halafu Ostaz Juma hana nidhamu halafu ni mtu ambaye hajitambui. Vijisenti anavyovipata nadhani ndivyo vinampa jeuri ya kudhalilisha wasanii wenzetu, sio kitu kizuri.
"Mimi tangu nilipoona hizo picha nilisema siwezi kumpenda hata siku moja, hata salamu yangu siwezi kumpa. Siwezi kumheshimu hata kidogo. Nitamdharau kuliko kitu chochote, kuliko mtu yeyote aliyewahi kunikosea sana. Ila katika watu ambao waliowahi kunikosea, nafikiri mimi Ostaz Juma amenikosea kupita maelezo. Kuliko alivyomkosea PNC mwenyewe.” Nay wa Mitego