- Maeneo ya ‘uswazi’ ndipo uhuni wa kila aina hufanyika kama vile ngono holela, lugha chafu za matusi, madisko bubu maarufu kama ‘vigodoro’, ulevi, wizi, uvutaji wa sigara na bangi na hata utumiaji wa dawa za kulevya.
Kutokana na mchezo wa ngumi kuonekana kuwa mgumu na kuhitaji watu wakakamavu, wenye
Katika Jiji la Dar es Salam maeneo kama Tandale, Temeke, Magomeni, Manzese, Keko, Kinondoni ni baadhi ya maeneo yenye sifa hizo. Maeneo ya Morogoro na baadhi ya sehemu za Mkoa wa Mbeya nazo zimesheheni sifa hizo.
Katika hali isiyo ya kawaida mabondia wanaofanya vizuri na kujizolea umaarufu nchini wamekuwa wakitokea kwenye maeneo hayo ya uswazi, hii inawezekana inachangiwa na aina ya mchezo.
Mchezo huo wa ndondi huhitaji watu wakakamavu, wenye stamina na uvumilivu ambao ni vigumu sana kuwapata maeneo ya ‘Kishua’ kama Mbezi Beach, Mikocheni na Masaki.
Kauli ya Miyeyusho kuhusu bangi
Alipoulizwa kuhusu shutuma kuwa mabondia wengi wanajihusisha na uvutaji wa bangi, Bondia Francus Miyeyusho alisema, “Unajua mabondia wengi tunatokea uswahilini ambako hayo mambo ndio yanafanyika. Ndiyo maana utakuta baadhi ya mabondia wanatumia vitu hivyo.”
“Hili siyo la mabondia tu ila hata wanaocheza michezo mingine kama soka, riadha na kikapu wanaotokea maeneo yetu haya ya uswahilini utakuta wanatumia.” Aliongeza Miyeyusho anayeishi Kinondoni Mkwajuni jijini Dar es Salaam.
Miyeyusho anadai kuwa malengo ya kutumia vitu hivyo yanatofautiana, ambapo wengine hutumia kama starehe wakati wengine hutumia ili iwasaidie kupata hamasa ya mchezo.
Mkali wa ‘Knockout’
Katika mapambano 47 aliyopigana Miyeyusho, 32 yalimalizika kwa ‘knockout’. Kati ya mapambano hayo 32, mapambano 23 alishinda kwa knockout na kupoteza tisa kwa knockout akiwa ndio bondia pekee wa Tanzania mwenye rekodi ya kushinda michezo mingi kwa ‘knockout’ na kushindwa mingi kwa staili hiyo hiyo. Katika michezo kumi aliyopoteza tisa amepoteza kwa ‘knockout’
“Mimi huwa napenda kuimaliza michezo yangu kwa ‘knockout’ kwa sababu mara nyingi ushindi wa pointi humalizika kwa utata. Wengine huona kama bondia amependelewa ushindi kitu ambacho siyo sahihi.”
“Nimepoteza mapambano mengi kwa ‘knockout’ kwa sababu ya kuwa na maandalizi duni, kutokana na hali ndogo ya kipato likitokea pambano hata kama sina mazoezi huwa nakubali ili nipate fedha japo ninajua sitaweza kushinda.
Jina Miyeyusho kumbe si lake
“Niliingizwa kwenye masumbwi na bondia Ramadhani Miyeyusho hivyo watu wengi walizoea kuniita Miyeyusho mdogo, baadaye alipostaafu Ramadhani mimi ndio nikawa nimebaki na jina la Miyeyusho.”
“Ramadhani yeye alikuwa ni ‘Miyeyusho’ wa ukweli (yaani tapeli) na ndiko alikopatia jina ila mimi sio miyeyusho wa kweli ila ni jina tu.” Aliongeza Miyeyusho ambaye hupendelea kuitwa ‘Chichimawe’.
Atamba mwaka 2013
Francis Miyeyusho alipata mafanikio makubwa kwenye ndondi mwaka jana baada ya kushinda michezo minne yote aliyocheza huku mitatu akishinda kwa ‘knockout’.
Michezo aliyoshinda mwaka jana ni dhidi ya Shadrack Machanje kwa knockout raundi ya kwanza, Fidelis Lupupa kwa ‘technical knockout’ raundi ya nane, Sadick Momba kwa pointi na Joshua Amukhulu kwa ‘knockout’ raundi ya tatu.
Anampenda Cheka, Matumla
Katika ngumi za kulipwa, Miyeyusho anavutiwa sana na bingwa wa dunia wa zamani wa WBU, Rashid Matumla ‘Snake Man’ pamoja na Francis Cheka. Kimataifa anavutiwa na Flyod Mayweather.
Apanga kustaafu bila kupigwa na bondia wa Bongo
Miyeyusho hajawahi kupigwa na bondia mwingine wa Tanzania zaidi ya Mbwana Matumla, hataki kupigwa na bondia mwingine.