Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

NA HAYA NDIO MAPATO YA MECHI YA JUZI YANGA NA MISRI SOMA HAPA LIVE!!

$
0
0


yangaMechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika iliyochezwa 01 March 2014 iliyohusisha timu ya Yanga na Al Ahly kutoka Misri kwenye  Uwanja wa Taifa Dar es salaam umeingiza jumla ya fedha za Kitanzania 448,414,000.

Mapato hayo yametokana na Kuingia watazamaji 50,202 waliokata tiketi kwa viingilio vya sh. 7,000, sh. 13,000, sh. 25,000 na sh. 35,000 na katika mchezo huo timu ya Yanga ilishinda kwa bao 1-0.
Mgawo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo;Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ni sh. 68,402,135.59, gharama za kuchapa tiketi ni sh. 10,343,219, waamuzi na kamishna sh. 14,665,930 na matangazo sh. 15,679,000.
Uwanja sh. 50,898,557.31, gharama za mchezo sh. 33,932,371.54, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)/Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 33,932,371.54 wakati Yanga ilipata mgawo wa sh. 220,560,415.01.
Upande wa mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Simba na Ruvu Shooting iliyochezwa jana Machi 2  imeingiza sh. 20,610,000 ambapo kila klabu ilipata mgawo wa sh. 4,402,492 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 3,143,898.31.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>